Unajua hapa utapigwa porojo za hapa na pale. Kiufupi hizi mambo ambazo zina vinasaba vya kamali vina hasara kibwa lakini pia unaweza ukapiga hela nyingi.
Uliyemkoti ametoa mfano wa tikiti, tikiti kuna tikiti lenyewe kama bidhaa na shamba kama kama bidhaa hivyo mtu hata akipata hasara hawezi akapata hasara mpaka shamba lako likapotea.
Sasa kwenye forex na kamali zingine kama betting ukiliwa unaweza ukapoteza hela yote wenyewe wanaita kuunguza.
Mfano huyu mleta mada kama aliweka $200 yote inakuwa imeenda sasa fikiria kama angewekeza kwenye shamba la tikiti je hiyo hasara ingesababisha kupotea mpaka kwa shamba?!
NB. Naiita forex kamali kwa sababu zifuatazo.
1. Hakuna bidhaaa wala huduma yoyote inayozalishwa.
2. Msingi wa forex ulikuwa na kwa ajili ya kufacilitate international trade.
3. Ili upate faida kwenye forex, mtu mwingine pia anatakiwa apoteze hela, na ukiona umepata hasara basi mtu mwingine amepata faida. Hizi ni sifa za kamali.