Inkoskaz
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 6,361
- 2,378
Naona kuna wigo mpana umesahaulika...hebu tujikumbushe
- Kodi kwa minara ya simu na yamatangazo ya redio na Televisheni,hakika hili ni eneo jingine ambalo mapato yake yanapotea na ukizingatia ni nyezo zinazoyaingizia makampuni mengi kipato kikubwa na pia wamiliki wa maeneo ya ilipojengwa wanapata mapato mazuri tu tax free.mfano mnara wa simu unaweza kuwa na mita ya kusoma talktime na message zilzotiririka na kutoa wastani wa matumizi iwapo wazo la flat rate lisipokubaliwa
- Kodi kwa nyumba za kupanga.Hili ni eneo ambalo limebaki likinufaisha wamiliki wa nyumba bila serikali kupata mapato.naona TRA inatilia mkazo pango la kibiashara lakini haya mapango ya nyumba za kuishi kunapotea mabillion mengi hebu pafanyiwe kazi fasta.majuzi tumesikia TRA wakanzisha mfumo kwa wafanyabiashara wa kipato cha 40,000 kwa mwezi sasa hapo wenye nyumba za kupanga wanawaweka wapi? Maana maapartment yanapangishwa kwa bei za ajabu tena dola mbona wapangaji hawapewi risiti na hao wapangishaji hawana leseni za biashara??
- Guest house zilizotapakaa kila kona za miji yetu hazitowi EFD receipt--kuna mapungufu hapo
- Bar na groceries everywhere mbona tukiagiza hizo redbull hatupewi EFD?
- Daladala tiketi zao pia zingekuwa katika mfumo wa EFD
- vilabu vya mpira makato ya viingilio na tiketi ziwe kwa mfumo wa kodi papo hapo
- Kumbi za STAREHE NA HARUSI hizi ziwe na kodi per function
na nyinginezo wadau tukumbushane.....
NB; Nimetaja EFD sehemu nyingi lakini ningeshauri mfumo wa EFD uzingatie CREdit SALES kwani ni moja ya huduma inayofanyika na pia pamoja na kuongeza mapato mianya ya matumizi mabaya izibwe kwa kuanzia na wafanyakazi wenyewe wa idara ya Kodi
Nawakilisha mjadala