Huyu alishastaafu kazi cia mwaka 2007 na akarudi hong kong kufanya shughuli zake binafsi. Akiwa huko akafuatwa na intelligence officers wa kichina na kumuahidi watampa pesa ya kutosha awaibie siri ya cia operations nchini china.
Hii ilishtukiwa mwaka 2012 baada ya informants wengi wa cia kuuwawa wakiwa china tena wengine mchana kweupe kwa kupigwa risasi ndio fbi wakaanza uchunguzi, mwisho wakafanya kitu kinaitwa ikawa zeroed kwa huyu mshikaji, wakaanza kumchunguza kuanzia hongkong, virginia, siku moja wakavamia chumba chake cha hotel bila yeye kujua, wakakagua begi lake na kukuta ana note book ya majina ya watu waliokua anafanya nao kazi kabla hajaacha kazi cia, majina yao halisi na contacts zao na locatio, usb na vitu kadhaa ambavyo aliposaafu hakuvikabidhi cia, fbi walimhoji kuhusu hizo mambo akakataa kua hana information yoyote.
Mbaya zaidi akawa anakutana na washkaji zake wa zamani wa cia ambao bado wanafanya kazi huku akijua alishahongwa na wachinana hakuwaambia chochote.
Huyo alitakiwa kunyongwa, alisaini plea deal asamehewe kifo kwa kifungo kirefu kwa kukiuka kitu kinaitwa life time non disclosure agreements alizosaini mwaka 1994 alipoajiriwa cia .