Ila tayari washaanza maneno, yaani Hamilton kushinda juzi watu hawapendi na wanatishia kususia mashindano, eti gari lake (Mercedes) ni bora sana hivyo hawa vilaza wengine waruhusiwe kufanya copy & paste ya technology ya Mercedes ili waweze kushindana nao.
Sikatai kuwa F1 inaboa flani hivi lakini hili halijaanza na Hamilton, Vettel kwa miaka minne mfululizo alikua anatuboa tu mpaka kuna time nilisusia kuangalia F1, kwanini hili halikua raised by that time ila wakati huu Hamilton anafanya vyema? Yaani ukilaza wa Honda, Renault, Ferrari ndio uwacost Mercedes? Tena yule boss mngese wa Redbull should be the last man to open his filthy mouth kuongelea hili, wakati wanatuboa na Vettel wao alikua wapi? Leo badala ya kugombana na Renault anaongea hizi shudu? Wameniboa sana
cc;
Kibunango,
Pazi,
Wacha 1,
RRONDO,
DMussa,
BAK,
Bulldog
"Asiyekubali kushindwa si mshindani"Msemo huu upo sahihi kabisa ukitizama kauli za Horner wa Red Bull. Inashangaza sana jinsi alivyoshindwa kuelewa lawama zake azipeleke wapi! Na inashangaza sana kuona kuwa ni kwa nini amekuwa mtu wa kijicho namna hii kwa Mercedes... Licha ya hapo awali kutupa shutuma kwa wazambazaji wao wa injini. Naona sasa amekusudia kwa makusudi kushinikiza kupunguzwa kwa kasi kwa Mercedes baada ya kumshirikisha Bernie Ecclestone.
Kuna timu kumi na wasambazaji wanne wa injini, ambao ni Ferrari, Mercedes, Honda na Renault.
Timu zinazotumia injini za Mercedes ni nne. Baada ya raundi ya kwanza sijasikia timu hizo zikilalamika kuhusu kuzungukwa kwa lap moja na Team Mercedes ambayo ndio iliyowapa injini hizo! Hii ina maana gani zaidi ya kujua kuwa ushindi hauletwi tu na injini pekee! Kuna vitu vingi vinachangia gari kwenda kasi kuanzia muundo wa
chassis,
wings n.k. Horner anajua hili zaidi yangu, ila bado namshangaa sana anapotaka kupunguzwa kwa uwezo wa injini za Mercedes.
Tunaweza kukumbuka mvutano mkubwa uliotokea kwa timu zilizokuwa zikitumia
double diffuser(Brawn,Toyota and Williams) na wale wa
KERS (Ferrari, Mclaren, Sauber na Renault) mwaka 2009, baada ya Brawn kuwa na speed kubwa. Tatizo hili lilikwenda hadi mahakamani na lilifika huko kutokana na sababu zilizokuwa wazi kabisa kwa timu hizo hazikufuata maelekezo ya FIA katika uboreshaji wa
aerodynamics. Hali ni tofauti kabisa na ubora wa timu ya Mercedes ya mwaka jana na mwaka huu, na Horner analijua hili na ndio maana analalamika peke yake!
Kwa ufupi ni kwamba Red Bull na wasambazaji wao wa injini wameshindwa kufanya homework yao vizuri na hawapaswi kutafuta mchawi, kwani mchawi wao wanamjua. Wajaribu kuiga mfano wa Ferrari ambao mwaka jana walikubali pasipo ubishi kuwa gari lao halikuwa na sifa ya kushinda dhidi ya Williams, Red Bull na Mercedes. Wakajipanga na sasa tunaanza kuona mafanikio kidogo na hapana shaka kuna tumaini la kuweza kushinda baadhi ya mbio.(japo moja).
[TABLE="width: 500"]
[TR]
[TD="align: center"]
No[/TD]
[TD="align: center"]
Timu[/TD]
[TD="align: center"]
Injini[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1.[/TD]
[TD]Williams[/TD]
[TD]Mercedes - PU106B Hybrid[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2.[/TD]
[TD]Force India[/TD]
[TD]Mercedes - PU106B Hybrid[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3.[/TD]
[TD]Lotus[/TD]
[TD]Mercedes - PU1068 Hybrid[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4[/TD]
[TD]Mercedes[/TD]
[TD]Mercedes - PU106B Hybrid[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5.[/TD]
[TD]McLaren[/TD]
[TD]Honda[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]6.[/TD]
[TD]Red Bull[/TD]
[TD]Renault Energy F1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]7.[/TD]
[TD]Toro Rosso[/TD]
[TD]Renault Energy F1[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]8.[/TD]
[TD]Ferrari[/TD]
[TD]Ferrari[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]9.[/TD]
[TD]Sauber[/TD]
[TD]Ferrari[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]10.[/TD]
[TD]Manor Marussia[/TD]
[TD]Ferrari - 059/3[/TD]
[/TR]
[/TABLE]