Sababu vijana watanzania wamelelewa katika ulimwengu wa upumbavu so vichwa vyao muda mwingi vinaprocess upumbavu, vinatafuta taarifa za mambo ya kipumbavu kama skendo za mastaa, ushabiki wa siasa kichawa, kutazama ngono na mengine yasiyo ya maana yaani upumbavu mtu. Wakija kwenye nyuzi za mambo ya msingi kitaifa kama hapa huwa wanachemka kuchangia au kuweza kutoa maoni sababu ni vichwa vyao kijawa na upumbavu zaidi.
Hawasomi mambo positive ya kilimo, uchumi, philosophy, psychology, sociology na science wao kazi kusoma upumbavu wa Manara kafanya nini, mandonga kafanya nini, Diamond kafanya nini, mbowe kamjibu nini Job ndugai. Yaani upumbavu ndio umewajaa vichwani.
Sisi wachache tunaopenda mambo positive wacha tuendelee na ratiba zetu na tujiimarishe kifikra. Hawa wapumbavu watavuna wanachokijaza vichwani mwao. Fikra tunazojaza vichwani ndio akiba ya hekima ya baadae. Sasa sijui watakuja wahadithia watoto wao maswala ya akina manara watakapowauliza mbona taifa letu ni masikini na tuna rasilimali tele na watu wengi.