Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Formula; "ONDOKA" 'ACHA' NDIO MAANA HALISI YA KUPATA MAFANIKIO.
Anaandika, Robert Heriel
Mwanafalsafa
Nitakuambia ukweli na siri wala sitakuchaji hata sumni wala shilingi yoyote. Vitu tulivyopewa bure tunavitoa Bure. Wala usinipe sifa yoyote Kwa maana sistahili sifa. Wala usinishukuru Bali mshukuru Mungu wako aliyekuumba.
Niite Taikon Master, Mwalimu asiye wa Mshahara lakini asiyepungukiwa na chochote.
Kila mtu hupenda kufanikiwa Kwa kila Jambo alifanyalo. Binadamu wengi Kama sio wote hupenda mambo mazuri. Kwayo huyaita mafanikio. Hata hivyo kila mtu anamafanikio yake kulingana na Yale ayapendayo,
Lakini mafanikio ili kuyafikia kunahitaji mchakato Fulani. Leo Taikon atajadili Jambo moja nyeti katika Mafanikio ambalo ni kanuni ya "ONDOKA" au "ACHA" na ili uondoke au uache itakupasa usiwe na UOGA. Ukiwa muoga huwezi kuondoka au kuacha baadhi ya vitu au mambo. Utaishi Kwa mazoea na kuogopa vitu ambavyo havipo.
Huwezi kufanikiwa katika Jambo lolote Kama hujaitumia kanuni hiyo. Kanuni hiyo ni moja ya nguzo muhimu ya mafanikio.
Kuondoka au kuacha ni Kama kanuni moja niliyowahi kuielezea iitwayo kujipachua, hata hivyo katika kanuni ya kujipachua nilijikita zaidi katika kuelezea mfumo mzima wa kuunda Uhusika bandia Kwa kuji-matrix(kujipachua). Kujipachua kunamaanisha huwezi kufanikiwa katika maisha ukiwa na uhusika mmoja(uleule) lazima uwe na uhusika mbalimbali.
Mfano, Mimi Taikon halisi nijipachue mara tatu. T¹, T², T³ na kila uhusika uwe na roles zake. Maadui zangu nihakikishe wanapambana na wahusika bandia niliowaunda huku Mimi mhusika OG nikiwa naendelea na mambo yangu. Hata hivyo hiyo sio mada ya Leo.
Kuondoka au kuacha ni kitendo cha kutoka au kubadilisha kitu au Hali au Jambo au Mazingira kwenda katika kitu au Hali au Jambo au Mazingira mapya.
Kwenye maisha hiyo ni kanuni namba moja ya mafanikio.
Aina za kuondoka au kuacha;
1. Kuondoka Kiakili
2. Kuondoka kimazingira
3. Kuondoka kimahusiano
4. Kuondoka Kiroho
1. Kuondoka Kiakili.
Hii ni Ile hali unaifanya akili yako isifikiri Kwa namna uliyozoea, Kwa kuwaza vitu vipya na kuvifanya Kwa vitendo.
Huwezi kufanikiwa kwa akili ya zamani uliyonayo hivi leo.
Lazima akili yako uweze kuifanya ifikiri vitu vipya kisha uvitekeleze.
2. Kuondoka kimazingira.
Huwezi fanikiwa katika Mazingira yaleyale uliyozaliwa, ni ngumu Sana.
Mafanikio ya watu wengi huchipuka pale wanapoondoka sehemu zao za Asili na kwenda Maeneo mageni.
Wazungu na mataifa ya Ulaya yalifanikiwa Kwa namna hii kipindi cha Mercantilism, ukoloni na sasa ukoloni mamboleo.
Wahindi, waarabu na sasa Wachina wote wanatumia kanuni hiyohiyo.
Kwa hapa Tanzania, Makabila kama Wachagga, wakinga, Wabaya, Waha na kidogo Wasukuma pia wanatumia kanuni hiyo.
Kidini, Biblia inatuambia Mungu alipomuumba Mtu Kwa mfano wake, alimpeleka katika Bustani ya edeni(yaani alimuondoa sehemu yake ya Asili alipomuumbia) kwa Adamu hayo yalikuwa mafanikio.
Lakini alipoasi alimrudisha Sehemu yake ya Asili Kwa kumfukuza kwenye Bustani ya Edeni.
Abrahamu pia aliambiwa aondoke kwenye Ardhi ya Asili yake,
Genesis 12:1
The LORD had said to Abram, “Leave your native country, your relatives, and your father’s family, and go to the land that I will show you.
Kwa wale wapenzi wa kiswahili,
Mwanzo 12:1
BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
Tafsiri ya kingereza imekaa Fresh mwakemwake kuliko ya Kiswahili.
Yaani hapo Abrahamu anaambiwa aondoke na kuiacha nchi yake ya Asili, ndugu na jamaa zake na Baba yake yaani awaache. Mpaka nchi atakayoonyeshwa na Mungu.
Aya hiyo lazima kabla haujaifanyie uchambuzi au ufafanuzi wowote lazima nchi anayoambiwa aiache ni nchi ipi na ilikuwaje, ujue jamaa na ndugu zake Abrahamu anaoambiwa awaache ni kina Nani na walikuwaje, huyo Baba yake Abrahamu ni Nani na Kwa nini Abrahamu anaambiwa amuache.
Ukishajua hayo sasa uje kwenye uchambuzi na ufafanuzi kadiri utakavyobarikiwa.
Nchi ya Uhuru wa ukaldayo ilikuwa ya waabudu sanamu, Baba yake Abrahamu aliyeitwa Tera alikuwa fundi wa kuchonga miungu ya sanamu. Ambaye kwenye Uislam alitambulika kama "Azar"
Quran inamtambua Baba yake Abrahamu kwa jina la kazi yake na sio jina lake halisi ambalo ni Tera ndio maana ameitwa "Azar" ambapo Kwa lugha ya Kiswahili humaanisha mchonga vinyago au masanamu.
Vitabu vyote viwili Biblia na Quran vinamtambua Baba wa Abrahamu kama mchonga vinyago vya sanamu na muabudu sanamu.
Hiyo ndio sababu ya Ibrahimu kuambiwa aachane na Baba yake na ndugu zake na Nchi hiyo ya waabudu miungu na masanamu.
Kisha aende katika nchi atakayoagizwa.
Kitu pekee cha Muhimu kuzingatia hapa ni sababu za kuondoka, kuacha au kuhama.
Unaweza ishi Eneo ambalo ni Asili yenu ambalo wazazi wako hawakukuwekea mifumo na eneo hilo unaweza ukahama kwani ni ngumu kufanya vizuri au kufanikiwa.
Lakini kama ni eneo ambalo wazazi wako walihamia na wakakuwekea mifumo yaani mifumo umeikuta basi unaweza endelea kupambana hapohapo na ukafanikiwa.
Eneo ambalo unatakiwa kuhamia linatakiwa Liwe na sifa zifuatazo;
1. Rasilimali za muhimu kama Ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha, Hali na tabia ya nchi nzuri, sio Mkondo wa Maji kupita au kutuama(mafuriko), sio Mkondo wa upepo mkali.
Hizo ni Rasilimali muhimu.
2. Mila na desturi ikiwemo miungu na mambo ya kishirikina.
Lazima uishi sehemu ambayo Mila na desturi zake sio za kipuuzi au kishetani.
Na Kama itakuwa sehemu yenye tija na unaihitaji Sana lakini kuna watu wa Aina hiyo. Fanya njama au hila watu HAO wahame au waue. Au tengeneza mazingira ambayo mfumo hautawasapoti kuishi pamoja nao, wao ndio wahame.
Kama mtaishi pamoja basi hakikisha watoto wako unawajengea misingi ya kuwaona jamii hiyo sio watu Bali ni mfano wa watu. Hivyo ndivyo wafanyavyo Wazungu, waarabu, wahindi, na Wayahudi na jamii zote zenye hadhi ya juu.
Kwa Mazingira ya sasa, Kijana ukitaka kufanikiwa kanuni hiyo ni muhimu na nyeti ambayo hutaambiwa na yeyote zaidi ya akili yako ndio itakuwa inakushauri uondoke kwenye mji wenu uende miji ya mbali.
Ni rahisi wageni kuja kuwatawala kama ninyi ni jamii isiyosambaa.
Yaani kama kwenye jamii yako ninyi sio watu wa kusambaa kwenda kwenye jamii zingine ni rahisi jamii zingine kuja kuwatawala karibu Kwa kila kitu katika Ardhi yenu.
Mfano, ni ngumu Kwa muafrika kutoboa kwenye nchi za Wazungu au waarabu Kwa sababu jamii hizo zilitangulia kusambaa Afrika kabla Sisi hatujaanza kwenda kwao.
Au hata hapahapa Bongo ni ngumu Kwa mtu kutoka Dar au Morogoro kutoboa akifika Moshi au Arusha, au akifika Mwanza au Iringa Ila ni rahisi Kwa watu wa Moshi au Arusha au Mwanza au Iringa kutoboa wakiwa DAR au Morogoro.
Unajua ni kwanini? Wengi watajibu kuwa ni ubaguzi, nop! Jibu lake nitatoa siku nyingine na tayari nimeshaligusia.
Chakuzingatia zaidi, unapoondoka na kuacha asili au kwenu basi kuwa Makini na huko uendako, lazima uchague mahali pazuri na sahihi pakwenda.
3. Kuondoka kimahusiano.
Ili ufanikiwe katika mahusiano yoyote Yale lazima uwe mahiri katika kuondoka na kuacha.
Biblia inasema;
Mwanzo 2:24
Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Uwezo wa kuacha na kuondoka ndio utaamua mahusiano ya wanandoa kuwa mazuri na thabiti au laa.
Ili ufanikiwe kwenye ndoa au mapenzi lazima uwe na uwezo wa kuacha baadhi ya mambo na vijitabia ambavyo havina Afya katika mahusiano yenu. Lazima ukubali kuacha watu wasio na tija katika mahusiano na mwenzi wako.
Kuacha wazazi sio Jambo Dogo, ingawaje ndio kafara juu ya ndoa. Hiyo ndio maana halisi ya Upendo. Kuacha wazazi wako kwaajili ya mwenza wako. Na hicho ndicho Adamu alifanya.
Aliamua kumuacha Mungu(mzazi na Baba yake) sababu ya Hawa Mkewe. Alikubali kubeba madhaifu ya mkewe na kukubali lawama za Mungu, ingawaje. Wengi wanamlaumu lakini Hakuwa na Option zaidi ya hiyo.
Kwenye upendo hakuna options mbili zaidi ya Moja tuu kujitoa kwaajili ya mtu umpendaye.
Uwe tayari kufa Kwa ajili ya mwenza wako. Ndio maana Mungu hakumlaumu Adamu hata hivyo haikumzuia kumpa adhabu Kwa kuasi kwake.
Umeoa alafu unaleta mambo ya Wazazi wako kwenye Familia yako, hiyo ni Dalili ya kushindwa.
Umeolewa unaleta mambo ya wazazi wako, huko ni kuteteresha ndoa. Na kutotambua maana ya familia.
Familia yako ni Ile ya wewe na Mumeo tuu, hata hao watoto wakikua wataondoka na kuanzisha familia zao na wengine kuolewa.
Yote hayo yanawezekana palipo na upendo WA kweli. Pasipo Upendo WA kweli hii itakuwa ni nadharia isiyowezekana kutekelezeka, lakini penye upendo hii ni nadharia halisi.
Watu wanashindwa kuacha Ma-Ex wao, wanaachana kimwili lakini kiroho bado wanapendana matokeo yake ni kupashana viporo.
Ndio maana inashauriwa Vijana waoe wanawake Bikra ili Kupunguza na wala sio kuondoa kabisa mambo ya Ma-ex.
4. Kuondoka Kiroho.
Huwezi kufanikiwa kiroho kama utashikilia kile tuu unachokiamini pasipo kuchunguza na kujifunza Imani zingine.
Imani sio kuwa na msimamo pekee yake pasipo kujifunza,
Imani ni kujifunza kila iitwapo leo habari za kiroho na ili kujua ukweli na uthabiti wa kike unachokiamini.
Kujifanya unamisimamo ya kijinga katika Imani ndio imepelekea mpaka hivi leo wapo wanaamini vitu visivyoeleweka ati kisa amekuta wazazi wanaamini katika Imani hiyo.
Kumbuka Ibrahimu mpaka anaitwa Baba WA mataifa au Baba wa Imani ni kutokana alizaliwa na kukulia Kwa jamii na wazazi wanaoabudu masanamu kama miungu yao, lakini Ibrahimu akajiongeza Kwa kuchunguza na kujifunza kuwa kile anachokiamini ni sahihi.
Lazima ufanye uhakiki wa kile unachokiamini. Jambo lolote ambalo utashikilia msimamo bila kufanya uhakiki litakutambulisha Kama mtu mjinga usiyejitambua.
Kufanya uhakiki sio dhambi, sio kosa. Bali ni kujithibitishia kuwa upo Njia sahihi.
Lazima ufanye utafiti, lazima ulinganishe ubora wa Imani utakazozikuta katika jamii yako.
Usipende kupelekwa pelekwa na wanadamu wenzako pasipo kutumia Akili yako vizuri kisa tuu labda hao binadamu wanamaneno matamu, au wanavaa au majoho, au kanzu, au sifa yoyote Ile.
Tumia akili, huwezi fanikiwa bila kutumia Akili yako vizuri.
Kisha uombe msaada Kwa Mungu aliyekuumba.
Lazima ujifunze kuacha na kuondoka katika tabia au mazoea ambayo yanakufanya usifanikiwe ili uweze kufanikiwa.
Nipumzike Sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Moshi,