The Boss heshima mbele mkuu,
mimi nadhani hujamuelewa Binamu, na sio kama watu wanamuhukumu bali yeye kaleta haoja ambayo tayari keshafanya maamuzi, sasa hapa watu watamshauri nini zaidi ya kumsema ali arudi kwenye mistari, nimekuwekea bandiko lake hapo chini na uchambuzi wangu hebu lipitie tena natumaini una uelewa mzuri tu
Habari zenu wanajf? hope mu wazima.
Jamani naombeni ushauri wenu kwa hili ninalofanya kama ni sawa au nakosea.
causen: "Mimi ni mdada ambaye bado cjaolewa ila nina mchumba ambae anakaa mbali na mimi sababu ya kazi,yani mikoa tofauti."
Me: hapa inaonekana hakuna ugomvi wowote na mchumba wake ni mambo ya maisha ndio yamewatenganisha
Causen: "Kampuni ninayofanya kazi nimetokea kuwa karibu sn na kijana mmoja ambaye pia ni mfanyakazi mwenzangu lakini sio ofisi moja,ukaribu umezidi na hatimaye tumejikuta in love,ukweli ni kwamba naweza kusema huyu kaka anajua kupenda, ananiheshimu and he real know how to care for a woman,kitu ambacho i always dream about,
Me: Hapa ndio tatizo lilipoanza, kwanza wapo ofisi tofauti ni ukaribu gani waliokuwa nao na nini walichokiongea mpaka wakaingia kwenye mambo ya mapenzi? sasa hapo kwenye Pink ndio mimi binafsi ninapomlaumu huyo dada, kumbe Pamoja na kuwa na jamaa/Mchumba wake yake lakini still alikuwa hajapata bado lile penzi ambalo alikuwa analiDream, alafu ni amkoasa makubwa kumlinganisha mume/mchumba wako na mtu mwingine, kutokana na maelezo haya huyo mchumba wake hamfai kwa sababu AJUHI kupenda, HaMheshimu and he real DONT know how to care for a woman
cAUSIN: yupo tayari kwa lolote na muda wowote nitakaomhitaji hasa kama nina shida,ukweli ni kwamba tumependana sn utafikiri wote tumekutana tukiwa single,wakati hata yeye ana mpenzi wake ambae pia anaishi mbali na yeye.
ME: Hapa dada yetu anaonyesha tofauti nyingine ya Mchumba wake na huyo jamaa yake mpya, kwamba yeye ni fimbo ya karibu na yupo muda wowote, lakini Causen hajuhi kama amejichanganya mwisho wa maelezo yake "ana mpenzi wake ambae pia anaishi mbali na yeye." kumbe ukaribu wote ni kwa sababu jamaa na mpenzi wake wako mbalimbali
Causen: Naombeni ushauri wenu kwa hiki ninachofanya,je ni sawa na kama sio sawa nitafanyaje?,
Me: kama ungeishia hapa ungeweza kupata ushauri, lakini kwa maelezo yako ya hapa chini
Causen: ukweli ni kwamba nampenda sana na siko tayari kumpoteza cause he made ma life wonderful,never knew it before.
Me: nimepitia maelezo yote ya Causen sijaona hata sehemu moja aliyosema nampenda sana huyo mchumba wake, lakini kinyume ni kuwa anampenda sana huyo jamaa yake mpya na hayuko tayari kumpoteza, kwa maana nyingine yupo tayari kumpoteza yule wa zamani, hii kauli pia inanipa wasiwasi "never knew it before". yaani ameonyehswa dunia mpya (Born again) ambayo mwanzo hakuiona, huo mwanzo ulikuwa ni upi?
Causen: Na ninaomba nieleweke niko na mchumba wangu kwa miaka miwili na nusu sasa na sijawahi kumsaliti kwa mwanaume yoyote zaidi ya huyu.
Me: Hapa nadhani ndio mwanzo wa mwisho wa haya maisha yao ya uchumba, kwa muda wote wa miaka miwili na nusu dada Causen alikuwa hajawahi kupata kuona hii dunia mpya ya huyo "kijana mmoja", hilo la kusema ndio mara yako ya kwanza kusaliti na sababu ya kusaliti ni kuwa mchumba wako yupo mbali na wewe, vipi na huyu jamaa yako wa sasa akiwa mbali na wewe kikazi?
I wish i could knew him before,cause its like i found a real love when its too late,hata yeye pia ana apprecite sana for this love.
Causen: Naombeni ushauri,nitaendelea hivi mpaka lini?
Me: hapo ushauri hakuna na huo uchumba wako hauwezi kuwork out na hata hiyo ndoa yako kama mkioana na huyo mchumba wako haitadumu, na sababu kubwa umesha mdharau kwa kila kitu na mbaya zaidi nadhani ulikuwa unamponda mchumba wako mbele ya "huyo kijana mmoja" na ndipo alipochukulia advertage ya kupretend na kuperform extra ili akuchote.
Na hata kama ukiforce kuolewa ili mradi umeshaonja nje na kuona tofauti, hauwezi kuacha hiyo tabia, nina uhakika utaisaliti ndoa yako na mwisho wa siku ni kuja kuwatesa watoto ambao hawana hatia yoyote