TANZIA Fr. Privatus Karugendo amefariki dunia

TANZIA Fr. Privatus Karugendo amefariki dunia

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Baba Privatus #Karugendo amefariki dunia usiku huu.

#RIPFrKarugendo
7208ABDE-DB1B-45DC-A87E-060ACEB9D904.jpeg


Baadhi ya maandishi yake kwenye mitandao ya kijamii.

14/6/2021
“Kutafakari na kuhoji ni dalili Za uhai. Maiti haiwezi kutafakari wala kuhoji! Twaweza kuamua kuishi kama maiti au viumbe hai wenye uwezo wa kuutiisha ulimwengu na kujiletea maendeleo! Maendeleo uletwa na watu hai, si maiti”.

18/3/2021
“Mama Samia, pole sana kwa msiba huu mkubwa. Wengi tulikufahamu na kukupenda wakati wa Bunge la katiba. Simamia katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, uzalendo, umoja na mshikamano. Tanzania ni yetu sote”.

19/11/2020
“Hawa wanawake 19 wa Chadema, ninawafahamu vizuri, ninawaheshimu saaaana kwa msimamo wao na uaminifu mkubwa kwa chama chao na taifa lao. Ni kitu gani kimewapata?. Fedha? Hapana! Ubunge? Hapana! Hawa ni wapambanaji, watiifu na wazalendo! Wamejikwaa wapi? Halima! Niambie!”.

19/9/2020
“Mama Samia, ana sifa nyingi, mbali na upole, huruma, umakini na busara hana siasa za chuki na ushabiki, anaiangalia Tanzania, kwa ujumla wake, ni mzalendo wa kweli! Tujifunze kwake! Tanzania ni yetu sote!”.

=====

Aliyekuwa mchambuzi DW katika masuala ya mbalimbali ya kisiasa na kijamii nchini Tanzania Padri Privatus Karugendo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko Dar es Salaam baada ya kuugua katika kipindi kifupi. Kabla ya kuasi upadri, Karugendo aliwahi kuwa paroko Msaidizi wa Parokia ya Buziku Jimbo Katoliki la Rulenge. Sudi Mnette amezungumza na mchambuzi Gwandumi Mwakatatobe.
 
Back
Top Bottom