TANZIA Fr. Privatus Karugendo amefariki dunia

TANZIA Fr. Privatus Karugendo amefariki dunia

Nimesoma makala zako kwenye magazeti mbalimbali tangu ningali kijana mdogo. Sehemu ya uandishi wangu leo ni yale niliyojifunza kwa kusoma maandiko yako. Kudadavua hoja, kutafuta ushahidi (facts &evidence), kufafanua takwimu, kupangilia lugha etc.

Maandiko yako yalinijenga kifikra. Japo kuna baadhi ya mitizamo yako sikukubaliana nayo lakini niliiheshimu. Nakumbuka mgogoro wako na Kanisa mwanzoni mwa miaka ya 2000. Nakumbuka uliposimamishwa kufanya huduma za kitume. Nakumbuka kitabu chako kiitwacho "Wito wangu, Imani yangu" ambacho ulielezea kiini cha mgogoro huo.

Nakumbuka mwaka 2008 ulivuliwa rasmi daraja la upadri baada ya miaka 8 ya kusimamishwa na ukaondoa neno "Padri" mwanzoni mwa jina lako. Nakumbuka miaka 9 baadae (mwaka 2017), Vatican ilikubali ombi lako la kuoa na ukafunga ndoa na mama Rose Birusya. Nakumbuka namna mlivyokua mkipishana mara kwa mara na mdogo wako Prudence Karugendo ambaye amefariki majuzi.

Nakumbuka misimamo yako ya kisiasa na jinsi ulivyosimamia hoja bila kujalisha ni wangapi wanakuunga mkono. Yote kwa yote umepigana vita njema na umeimaliza safari. Kwaheri Padri Privatus Karugendo. Maisha yako ni hadithi yenye kufunza mengi. Until we meet again. Pole nyingi kwa kanisa na familia.!

Malisa GJ
 
RIP big man 🙏 mwendo umeukamilisha, hakika mavumbini sote tutarudi.
 
Baba Privatus #Karugendo amefariki dunia usiku huu.

#RIPFrKarugendo

Baadhi ya maandishi yake kwenye mitandao ya kijamii.

14/6/2021
“Kutafakari na kuhoji ni dalili Za uhai. Maiti haiwezi kutafakari wala kuhoji! Twaweza kuamua kuishi kama maiti au viumbe hai wenye uwezo wa kuutiisha ulimwengu na kujiletea maendeleo! Maendeleo uletwa na watu hai, si maiti”.

18/3/2021
“Mama Samia, pole sana kwa msiba huu mkubwa. Wengi tulikufahamu na kukupenda wakati wa Bunge la katiba. Simamia katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, uzalendo, umoja na mshikamano. Tanzania ni yetu sote”.

19/11/2020
“Hawa wanawake 19 wa Chadema, ninawafahamu vizuri, ninawaheshimu saaaana kwa msimamo wao na uaminifu mkubwa kwa chama chao na taifa lao. Ni kitu gani kimewapata?. Fedha? Hapana! Ubunge? Hapana! Hawa ni wapambanaji, watiifu na wazalendo! Wamejikwaa wapi? Halima! Niambie!”.

19/9/2020
“Mama Samia, ana sifa nyingi, mbali na upole, huruma, umakini na busara hana siasa za chuki na ushabiki, anaiangalia Tanzania, kwa ujumla wake, ni mzalendo wa kweli! Tujifunze kwake! Tanzania ni yetu sote!”.

Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ampokee katika ufalme!
 
Ni miongoni mwa viongozi wa chache wa dini waliochagua kuendelea kusema kweli na kuikosoa mamlaka wakati Tanzania inapitia kipindi kigumu cha uminywaji wa haki za kiraia, uhuru wa habari na demokrasia.

Pumzika kwa amani Father Karugendo 😭😭
 
Back
Top Bottom