Note the spelling,Watu wanaimba,wengine wana bana pua,wengine studio za kichina zinawashine suati zao...LAKINI..huyu jamaa... alikuwa mwanamziki kweli na kipaji kutoka kwa Mungu.Mfalme wa rhumba(Le grand maiter),mchawi wa gitaa(guitar sossuor).
Kwa upande wangu mimi ndio chaguo langu la kwanza dunian pamoja na kundi lake loooote la Le Tuitor Puisant (All Power)ok jazz,kuanzia Madilu,Sager essuso,Simaro lutumba masia,Sam Mangwana'KICHWA BALAA', josky kiambukata,Mavitukuvisi & much moreee!
Je wewe unamuelewaje Franco na TP Ok jazz nzima??????
Mkuu wewe umeniona nini nna headset hapa nasikilita Tangawusi. Huyu jamaa mungu alimtunuku hasa, nikisikiliza nyimbo zake nakumbuka miaka ya mwanzo ya themanini nikiwa mdogo kaka zangu walikuwa wakizisikiliza sana hizi nyimbo na mzee wangu! na hata quality ya nyimbo zake ni za hali ya juu sana zilirekodiwa kwenye mitambo ya kisasa sana tena mnoo! hebu sikiliza Tokabola sentiment aliyoimba Josky kiambukuta!
Nakumbuka mwaka 1984 nikiwa songea tulikuwa na kanda yake, moja ya wimbo uliokuwepo ni mbanda ako ti kikumbi, saa yale matamshi ukisikiliza ni km anaimba matakoni kivumbi, basi si nikajirekodi kweli hiyo chorus eti matakoni kivumbi eeeeh mwanamama hahaha sister angu alikuwa anacheka hana mbavu.
Wimbo wa Mario part 1 unanikumbusha sana bustani ya nyanya aliyolima kaka yangu mwaka 1984-85. nilikuwa nikirudi toka shule wakati huo nipo std 4 basi nakuta bro kauweka, nikiingia ndani tu mdingi anaamka ananiambia badirisha yuniform nenda kamwagie nyanya, wakati huo mie sina mpango kabsaa wa kwenda bustanini, natorokea kiwanjani kupiga chandimu, nikirudi tuu saa moja moja ni bakora kwa kwenda mbele!
Hebu sikiliza Matata ya mwasi basi kwa leo halafu uniambie Franco amekukuna vipi
Sikiliza Arzoni, hili ndo rhumba bana
..na kinshasa mama eeen arzonieee
Papa Wemba Jossart Nyoka longo, Bozzi Bozziana, Gina wa Gina, Evoloko Joker (le wuatro langa langa plus Un) ni wanafunzi wake...
Koffi na Tabu Ley, ni wafwasi wake pia... Franco the greatest of them all!
Papa Wemba Jossart Nyoka longo, Bozzi Bozziana, Gina wa Gina, Evoloko Joker (le wuatro langa langa plus Un) ni wanafunzi wake...
Koffi na Tabu Ley, ni wafwasi wake pia... Franco the greatest of them all!
Iliitwa Loningisa. Hapa nimepita tu. Lakini kuna zile nyimbo alizoimba na mdogo wake Bavon Marie Marie mmeshazisikia?Alikuwa anastudio ya kundi lake pekee inatwa LONGISA studio...BINA NA NGAI NA RESPECT...MISSILE....NGUNGI(ft tabulei)...MATATA NA MWASI(dali kimoko yupo..wimbo una dakika 15)....LAYLE..TOJOUR!!..MUONGO NA MULOSI NI WATU YA KUCHOMA..WAPI WADAUUU???
Iliitwa Loningisa. Hapa nimepita tu. Lakini kuna zile nyimbo alizoimba na mdogo wake Bavon Marie Marie mmeshazisikia?
Kama nilivyosema hapa nimepita tu.
Sikonge,'Mwali si kweli uliyoyaandika.
Hao wote wa mwanzo ni kundi la Zaiko Langa Langa na kama sikosei ni Papa Wemba ndiye alikuwa na harufu ya Franco.
Koffi Olomide huwa hataki kukubali ila wengi wanasema kuwa kwenye mziki alitambulishwa na Papa Wemba.
Inapokuja kwa Tabu Ley, ni BIG NO!. Tabu Ley alitoka kwenye mikono ya Dr. Nico Kassanda ambaye unaposema mchawi wa gitaa, huyu mzee alikuwa hawezekani. Ni Dr. Nico na Grand Kalle (siyo Pepe Kalle) walioandika wimbo maarufu wa Independe Chacha. Kuna kijana kaupiga tena na kutengeneza remix moja nzuri sana.
Franco na Luambo hata sijui kama walikuwa marafiki au kwa chini walikuwa maadui hasa Tabu Ley akijikakamua kufuata nyayo za Franco. Kumbuka Franco alianza zamani sana miziki. Nilishawahi kuona CD yake iliyorekodiwa mwaka 1956, jasho likanitoka.
Luambo walikuja baadaye kutengeneza Album na Ley na moja ya wimbo hadi leo unapendwa sana na watu waliokula chumvi nyinyi na vijana wanaopenda kutafuta miziki ya zamani. Huu hapa NGUNGI.
Sikonge,'
Franco alianza muziki mwaka 1952. Kuna album waliimba pamoja na Tabu Ley miaka ya 80 sikumbuki jina lake. Nikiiona kwenye maktaba yangu nitarudi hapa.
Sikonge,'
Franco alianza muziki mwaka 1952. Kuna album waliimba pamoja na Tabu Ley miaka ya 80 sikumbuki jina lake. Nikiiona kwenye maktaba yangu nitarudi hapa.
Wazee huyu Luambo hata mimi na mkubali kuwa wimbo Bina na Ngai na Respect, acha kabisa.Sikonge vipi Verkys nae namkubali sana.
Watu wanaimba,wengine wana bana pua,wengine studio za kichina zinawashine suati zao...LAKINI..huyu jamaa... alikuwa mwanamziki kweli na kipaji kutoka kwa Mungu.Mfalme wa rhumba(Le grand maiter),mchawi wa gitaa(guitar sossuor).
Kwa upande wangu mimi ndio chaguo langu la kwanza dunian pamoja na kundi lake loooote la Le Tuitor Puisant (All Power)ok jazz,kuanzia Madilu,Sager essuso,Simaro lutumba masia,Sam Mangwana'KICHWA BALAA', josky kiambukata,Mavitukuvisi & much moreee!
Je wewe unamuelewaje Franco na TP Ok jazz nzima??????