Franco Luambo Makiadi

Franco Luambo Makiadi

POP-031-front1.jpg

Hizo zoote ni solo.....Gerry(au papa Noel) main solo.....Gege(bridge solo)....Decca(second solo na bass)....Babu mwenyewe(mid solo)
 
Mwali si kweli uliyoyaandika.

Hao wote wa mwanzo ni kundi la Zaiko Langa Langa na kama sikosei ni Papa Wemba ndiye alikuwa na harufu ya Franco.

Koffi Olomide huwa hataki kukubali ila wengi wanasema kuwa kwenye mziki alitambulishwa na Papa Wemba.

Inapokuja kwa Tabu Ley, ni BIG NO!. Tabu Ley alitoka kwenye mikono ya Dr. Nico Kassanda ambaye unaposema mchawi wa gitaa, huyu mzee alikuwa hawezekani. Ni Dr. Nico na Grand Kalle (siyo Pepe Kalle) walioandika wimbo maarufu wa Independe Chacha. Kuna kijana kaupiga tena na kutengeneza remix moja nzuri sana.



Franco na Luambo hata sijui kama walikuwa marafiki au kwa chini walikuwa maadui hasa Tabu Ley akijikakamua kufuata nyayo za Franco. Kumbuka Franco alianza zamani sana miziki. Nilishawahi kuona CD yake iliyorekodiwa mwaka 1956, jasho likanitoka.

Luambo walikuja baadaye kutengeneza Album na Ley na moja ya wimbo hadi leo unapendwa sana na watu waliokula chumvi nyinyi na vijana wanaopenda kutafuta miziki ya zamani. Huu hapa NGUNGI.


Sikonge umechambua kama karanga.
 
Last edited by a moderator:
Bakulutu,
Huyu rarely aliimba.......ila alitunga 80% ya nyimbo za TP OK Jazz......hizo nyimbo ulizotaja ziliimbwa na hawa...Testamente ya bowule(Malage),maya(malage),ebale ya zaire(carlito)

Safari nikupe siri moja ambayo niliipata kutokwa ndugu wa Franco niliwatemblea mwaka juzi..walisema kwenye enzi la TP kulikuwa kuna udikteta fulan hsa ktk uimbaji wa nyimbo hizo,alitunga hizo nyimbo nilizo kutajia ni simaro na aliimba ni simaro na malege kwan franco alikuwa anabana kila wimbo ubaki kwenye albamu zake hata kama cyo yeye akaimba ilimradi tuu iltengenezwa na loningisa studio,ilifika,wengi walikuwa wanatunga ila kuimba ndio alikuwa nawabania,hii check wikipedia hapo uangalie hizi nyimbo kaimba nani then u replay,hii ilileta tabu sana alipo kufa ndio maana ktk kuwanya uridhi famlia ya franco iliambulia kitu kidogo sana wengi walikuwa wanafidia nyimbo zao.
 
nimesikiliza wimbo wa MASU..nimemkumba Mama yangu nikaamua kumpigia simu na kumkumbusha amecheka sana..aliimba nyimbo hizi kwa ustadi mkubwa utafikili nae alikuwa muimbaji wa bendi hii hasa akiwa anafanya shughuli zake kama kufua na kuosha vyombo........
 
Mimi namkubali ingawa sikumbuki majina ya wimbo kuna mmoja kama wanafanya conversation via the phone na demu sijui jina la wimbo ila nauzimikia
 
Mimi namkubali ingawa sikumbuki majina ya wimbo kuna mmoja kama wanafanya conversation via the phone na demu sijui jina la wimbo ila nauzimikia


hiyo kitu inaitwa Mamou..na yule si demu bali ni mwanaume mpiga gitaa.. ....wimbo upo hapo juu we gonga utasikia....
 
Mimi namkubali ingawa sikumbuki majina ya wimbo kuna mmoja kama wanafanya conversation via the phone na demu sijui jina la wimbo ila nauzimikia

nenda page ya 3 post # 58 ndo huo wimbo upo hapo..anagalia na utajua kuwa yulle si demu ni mwanaume kamili ila aliigiza sauti ua kike
 
Mi naikubali sana "Mobutu" lakini sielewi nalizimia tu lile rhumba lake. Alikuwa anamponda au anamfagilia Mobutu?
 
JF members mnajua mambo, wengine tulikuwa watoto those days,
 
Back
Top Bottom