Mwali si kweli uliyoyaandika.
Hao wote wa mwanzo ni kundi la Zaiko Langa Langa na kama sikosei ni Papa Wemba ndiye alikuwa na harufu ya Franco.
Koffi Olomide huwa hataki kukubali ila wengi wanasema kuwa kwenye mziki alitambulishwa na Papa Wemba.
Inapokuja kwa Tabu Ley, ni BIG NO!. Tabu Ley alitoka kwenye mikono ya Dr. Nico Kassanda ambaye unaposema mchawi wa gitaa, huyu mzee alikuwa hawezekani. Ni Dr. Nico na Grand Kalle (siyo Pepe Kalle) walioandika wimbo maarufu wa Independe Chacha. Kuna kijana kaupiga tena na kutengeneza remix moja nzuri sana.
Franco na Luambo hata sijui kama walikuwa marafiki au kwa chini walikuwa maadui hasa Tabu Ley akijikakamua kufuata nyayo za Franco. Kumbuka Franco alianza zamani sana miziki. Nilishawahi kuona CD yake iliyorekodiwa mwaka 1956, jasho likanitoka.
Luambo walikuja baadaye kutengeneza Album na Ley na moja ya wimbo hadi leo unapendwa sana na watu waliokula chumvi nyinyi na vijana wanaopenda kutafuta miziki ya zamani. Huu hapa NGUNGI.