carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Naibu waziri kivuli wa kilimo, mifugo na uvuvi kutoka ofisi ya wasemaji wa kisekta wa chama cha act wazalendo, frank ruhasha, amesema kuwa mauaji na ukatili uliotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa oktoba 2025 havikulenga kudhibiti maandamano, bali vyombo vya dola vilifanya mauaji ya makusudi kwa kuwalenga raia kwenye sehemu za uhai.
akizungumza leo, oktoba 31, 2026, katika mahojiano maalum na kituo cha royal tv plus, ruhasha amesema kuwa matukio hayo yameacha simanzi nzito kitaifa kwa sababu raia walipigwa risasi za kichwani na kifuani badala ya kuchukuliwa hatua za kawaida za kudhibiti ghasia.
"matukio ya tarehe 29 mwaka jana ni matukio ambayo yanaumiza sana na yanasikitisha sana. sisi hatujazoea kwamba sisi kwa sisi tunaweza tukapigana risasi za kichwani... risasi yenye lengo la kudhibiti inaweza ikapiga chini au miguuni ili mtu asiweze kusonga mbele, lakini inapotokea watu wanapigwa risasi kichwani na vifuani kwa namba hizo tunazosikia, ni mambo ya kuhuzunisha sana,"amesema ruhasha.
aidha, ruhasha ameongeza kuwa ukatili huo haukuwaumiza tu wale waliopoteza wapendwa wao, bali umemjeruhi kisaikolojia kila mtanzania.
amemalizia kwa kusisitiza kuwa njia pekee ya kuponya jeraha hilo si kutumia maneno matupu au kauli za kisiasa kama “never again”, bali serikali lazima ichukue hatua za dhati za kiutendaji na kuziba nyufa zote zilizosababisha maafa hayo ili kurejesha utulivu wa kweli nchini.
Soma Pia : Askofu Emmaus Mwamakula: Tume ya Jaji Lila imekwepeshwa mambo muhimu juu ya Mauaji ya Oktoba 2025
Chanzo : Royal Tv