dindilichuma
JF-Expert Member
- Dec 19, 2015
- 1,736
- 2,699
Kwa Kanisa katoliki
Frateli ni mwanafunzi aghalabu aliemaliza kidato cha sita na kuanza mwaka wa kwanza Seminari kuu au nyumba za malezi au vyuo vikuu, Seminari kuu ni kama vile Peramiho, Kipalapala, Kibosho, Segerea, Kahama n.k.
Frateli anasoma kuanzia Mwaka wa kwanza falsafa mpaka wa 3 halafu Theolojia kwa miaka mitatu au minne.
Baada ya Theolojia atatumwa mwaka wa kichungaji kwenye Parokia Moja wapo kwa mwaka mmoja.
Baada ya hapo atarudi Major seminary tena na kuomba jimboni kwake kupewa Ushemasi.
Anaacha kuitwa Frateli baada ya kupewa daraja ya Ushemasi ambapo ushemasi umegawanyika katika makundi mawili
i. Ushemasi wa mpito- Kuelekea daraja Takatifu ya upadre
ii. Ushemasi wa kudumu - Anabaki milele shemasi.
Mara nyingi ndani ya mwaka mmoja Huwa shemasi wa mpito ikiwa sio shemasi wa kudumu anakua ameshapata daraja ya upadre.
Maeneo mengi ya majimbo ya Tanzania ila sio yote mafrateli hupata Ushemasi mwezi Desemba na upadre mwezi June mpaka Agosti mwaka unaofuata hivyo ndani ya miezi 9 Huwa frateli amepata daraja ya Ushemasi na upadre.
Mashemasi wanawekewa mikono sio kwaajili ya ukuhani Bali kwajili ya huduma ya utumishi.
Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app