Fred Ngajiro aka Fred Vunjabei ni nani huyu jamaa?!

Fred Ngajiro aka Fred Vunjabei ni nani huyu jamaa?!

Kuna kampuni China aliingia nayo mkataba inamtumia nguo huko nyingine ni mali kauli.Mjanja sana kwa biashara na hata maduka ya Whazou, Tunda Chocokate ni ya kwake.Anajua kuiitangaza biashara yake
Usizidishe umbea khaa!

Whozu na Franknows ni mtu na kaka

Walikuwa fighter tangu kule uchagani akaanza Franknows kutoboa akaja Whozu.
 
huyo jamaa kwanza shuleni hesabu alikuwa anapiga AA++, pili mzee wake alikuwa na bado ana mashamba mengi sana ya miti huko mufindi, kwao wana asili ya pesa. Mtaongea yoote ila kijana ni mpambanaji and akili kubwa sababu familia yake ina access ya pesa since forever.

So mtasema yooote ila huyo kijana atakuwa tajiri maradufu,hakuna uchawi wala ndumba,pamoja na kuwa ni kweli mkinga,lakini ametumia fursa za nyumbani kufika hapo alipofika...kudos fred!
Ni wachache wenye hii akili
 
Coz utajiri ni wa masharti
Acha upumbavu wewe

Wabena na wakinga ni makabila yenye nidhamu kubwa ya pesa na usiri mkubwa Sana kuhusu pesa zao ni kwa Sababu sio watu wanaopenda kushow off kila kitu kwenye jamii ni watu wanapambana haswa na sio waoga kwa kitu chochote kwao mafanikio ni Jambo la muhimu. Ndiyo maana unaona leo hii kariakoo Wabena na wakinga wamejaa kibao .

Kama unasema ni masharti na nyie mkajaribu muone Kama mtafanikiwa kirahisi .

Popote walipo wananchi wenzangu wa Njombe ni mwendo wa kukazaa tu haina kufeli sikuhiz na vijana wetu wameenda shule mizigo tunanunua wenyewe direct kutoka nje ya nchi

Ukinidhulumu pesa/mali yangu mwisho wa mwaka nafunga hesabu na damu yako ili uzalishe zaidi upande mwingine
 
Hilo liko wazi mzee

Kisaikolojia mtoa mada huenda ni aina ya wale watu wenye hali ngumu ya maisha, pamoja na kupambana hasa lakini bado ugumu wa maisha unawaandama...

Baada ya mbilinge nyingi bila mafanikio wanafikia mahal wanahitimisha kuwa, "hakuna namna mtu anaweza kufanikiwa kihalali"...

Hawaishii hapo, kujustify hilo hitimisho la kujifariji wanaanza kupeleleza watu waliofanikiwa, "kutaka kujua ni kipi cha ziada na kisicho halali kimewafanikisha"...

Njia mojawapo ya kupeleleza, ndio kuanzisha nyuzi kama hizi...
 
Utajiri wa wa hilo kabila huwa siukubali kabisa maana ni kawaida kumuona wa mafanikio kabisa wa hilo kabila ila anakula Kande.
Mawazo ya kimasikini yapo mpaka jf aibu hii, nani kakwambia kila mkinga ni tajiri tuulize sisi tunaokaa nao hawa watu,Mazingira yao(makete) sio mazuri sana kwa uwekezaji hiyo iliwafanya watoke waende ugenini na ikawajengea nidhamu ya kufanya kazi,hawa watu wanaushirikiano na ni hard workers sana,endelea kuamini maneno ya walioshindwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom