Fred Vunja Bei aongoza kura za maoni matokeo ya awali kumrithi Lukuvi. Awatupa wenzake mbali kama mshale

Fred Vunja Bei aongoza kura za maoni matokeo ya awali kumrithi Lukuvi. Awatupa wenzake mbali kama mshale

Kwa hiya mtatifikilo pamoja cv yake kubwa kwa matokeo haya ccm itamuacha na kumchukua fred?
Uongozi unatoka kwa Mungu. Ubunge ni Utumishi kwa wananchi na kujua shida na kero zao na majawabu kwa kero zao na siyo suala la cv . Wananchi wanaangalia nani atakuwa na uwezo wa kuwasilisha kero zao mahali husika na kuwasaidia. Lakini pia huangalia nani amekuwa karibu nao katika maisha yao ya kila siku
 
Ndugu zangu Watanzania ,

Habari ndio hiyo ya kuwa Mfanyabiashara Vunjabei ameibuka kinara katika kura za maoni za kumtafuta mrithi wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Isimani, Lukuvi, huku akiongoza katika kata nyingi zilizopigwa kura.
Kwa mujibu wa matokeo ya awali, Vunjabei ameonyesha nguvu kubwa ya ushindani akiwazidi wapinzani wake katika maeneo mengi ya jimbo hilo la Iringa.

Matokeo kwa mujibu wa kata:
1. Kata ya Ilolo Mpya
Mhe. Mtatifikolo – 147
Vunjabei – 110
Festo – 71

2. Kata ya Itunundu
Vunjabei – 190
Kiswaga – 28
Arifu – 14
Mhe. Mtatifikolo – 12

3. Kata ya Idodi
Vunjabei – 226
Mhe. Mtatifikolo – 200

4. Kata ya Kihorogota
Vunjabei – 170
Kiswaga – 84
Mhe. Mtatifikolo – 74

5. Kata ya Mlenge
Vunjabei – 255
Kiswaga – 100
Mhe. Mtatifikolo – 31

6. Kata ya Izazi
Vunjabei – 181
Kiswaga – 41
Mtatifikolo – 15

7. Kata ya Mboliboli
Vunjabei – 119
Mhe. Mtatifikolo – 33
Kiswaga – 22

8. Kata ya Malenga Makali
Vunjabei – 216
Kiswaga – 116
Mhe. Mtatifikolo – 17

9. Kata ya Kising’a
Vunjabei – 287
Kiswaga – 24
Mhe. Mtatifikolo – 5

Kwa ujumla, mwenendo wa kura unaonesha Vunjabei kuwa mbele kwa tofauti kubwa katika kata nyingi, hali inayomuweka katika nafasi nzuri ya kuwania uteuzi wa kugombea ubunge wa Jimbo la Isimani.
Matokeo kamili yanatarajiwa kuthibitishwa rasmi na chama cha CCM baada ya kukamilika kwa mchakato mzima wa kura za maoni

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania Wanyonge wasio na Sauti.
Vipi mumeo hajachukua form?
 
The man has strong financial muscles,
He will carry the day sooner than later.
In ccm if u have no money never expect to win in these party primaries unless u are Samia's Political sycophant.
 
Je CV ya vunjabei umeona ni ndogo na ukiangalia na impact yake kwa jamii kutoa ajira n.k
Huyo hana anachojua huyo. Inaonyesha hajua kuwa Vunja Bei katoa ajira kwa vijana karibu kila mkoa hapa Nchini. Lakini pia Vunja Bei ni Mlipa kodi Mzuri tu anayechangia katika Mapato kwa kupitia Biashara Zake.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Matokeo ya Mwisho yametoka na kuonyesha Mfanyabiashara Maarufu Nchini kwetu na nje ya Tanzania Fred Vunja Bei akiibuka kidedea na kwa kishindo kikuu kwa kuvuna kura 2703

Soma hapa 👉Mfanyabiashara Fred Ngajiro almaarufu Fred Vunjabei, ameshinda kura za maoni katika uchaguzi wa ndani wa Jimbo la Isimani akipata kura 2,703 katika uchaguzi huo uliokuwa na jumla ya wagombea 18.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Festo Kiswaga aliyepata kura 873 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mkuu wa Wilaya (DC), Emmanuela Mtatifikolo, aliyepata kura 621.

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, William Lukuvi, kilichotokea wiki chache zilizopita.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania Wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Screenshot_20260419-203752_1.jpg
 
Back
Top Bottom