Fred Vunja Bei aongoza kura za maoni matokeo ya awali kumrithi Lukuvi. Awatupa wenzake mbali kama mshale

Kwa hiya mtatifikilo pamoja cv yake kubwa kwa matokeo haya ccm itamuacha na kumchukua fred?
Uongozi unatoka kwa Mungu. Ubunge ni Utumishi kwa wananchi na kujua shida na kero zao na majawabu kwa kero zao na siyo suala la cv . Wananchi wanaangalia nani atakuwa na uwezo wa kuwasilisha kero zao mahali husika na kuwasaidia. Lakini pia huangalia nani amekuwa karibu nao katika maisha yao ya kila siku
 
Vipi mumeo hajachukua form?
 
The man has strong financial muscles,
He will carry the day sooner than later.
In ccm if u have no money never expect to win in these party primaries unless u are Samia's Political sycophant.
 
Je CV ya vunjabei umeona ni ndogo na ukiangalia na impact yake kwa jamii kutoa ajira n.k
Huyo hana anachojua huyo. Inaonyesha hajua kuwa Vunja Bei katoa ajira kwa vijana karibu kila mkoa hapa Nchini. Lakini pia Vunja Bei ni Mlipa kodi Mzuri tu anayechangia katika Mapato kwa kupitia Biashara Zake.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Matokeo ya Mwisho yametoka na kuonyesha Mfanyabiashara Maarufu Nchini kwetu na nje ya Tanzania Fred Vunja Bei akiibuka kidedea na kwa kishindo kikuu kwa kuvuna kura 2703

Soma hapa 👉Mfanyabiashara Fred Ngajiro almaarufu Fred Vunjabei, ameshinda kura za maoni katika uchaguzi wa ndani wa Jimbo la Isimani akipata kura 2,703 katika uchaguzi huo uliokuwa na jumla ya wagombea 18.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Festo Kiswaga aliyepata kura 873 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mkuu wa Wilaya (DC), Emmanuela Mtatifikolo, aliyepata kura 621.

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, William Lukuvi, kilichotokea wiki chache zilizopita.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania Wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…