-Hivi Mpendazoe ktk kuhitimisha mjadala wa Richmond alisimamia upande gani?
-Ni jambo la busara kama amejitoa,kama kajiunga na CCJ pia ni uamuzi wa Busara, na kama wapambanaji walioko CCM watajiunga na CCJ, basi wadhihirishe dhamira yao ya kweli kwa kuunganisha nguvu yao na vyama vya upinzani vyenye nguvu
Ila pia kwa sasa ina mana wananchi wa kishapu hawana mbunge,anyway kuna majimbo mengine yako wazi tangu 2005 hayana wabunge .
Kuna ambao wanasema kafanya uamuzi mbaya just because hajasubiri marupurupu yaani inasikitisha sana tuna watu wa aina hii,yaani mawazo ya watu walio wengi yamejaa unafiki na ubinafsi tu.Nasema kafanya jambo jema ikiwa kweli lengo ni kupigania maslahi ya taifa,angalao atapata muda wa kushirikiana na wenzake kuujenga au kuuandaa upinzani imara mapema kabla ya uchaguzi
Mtu kutoka CCM si uhaini,subiri uone jinsi watakavyompaka aonekane kama vile kafanya uhaini.Mpendazoe umeonyesha Moyo wa ujasiri,hii ndiyo aina ya siasa ninayoitaka,lakini bado swali langu nauliza,ktk hitimisho la RICHMOND alisimamia upande gani?