Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

Huyu anachemka tu, akawaulize akina Njelu Kasaka, think before you leap!

Kachemsha.
Hayo ya akina Njelu kasaka ndio yamewapa watu funzo. Ukiona wanachukua hatua kama hizi basi ujue kuwa wameshafikiria hayo yote na kujua wafanye nini. I dont tnk that Mpendazoe is such a fool kuchukua uamuzi ambao utamuumiza. labda kama maamuzi haya anayachukua kwa shinikizo fulani maana hawa ndugu ztu huwezi kujua njama zao zote
 
Wadanganyika bwana...hao wazee wapo kwa ajili ya kupigania timbua vyao jamani walikuwa wapi miaka yote hadi nchi kuwa mshipa?..wakimeguka ndio balaa zaidi kwa walalahoi au mahututi, maana focus haitakuwa kwenye maendeleo tena...bali kubuni mbinu za kuzidiana kete.....hawa wazee sasa wanajua kuwa ukitaka kuwa star bongo nikupiga mkwala mafisadi...bongo bila ubongo tutaendelea kuingizwa mjini na kila mwanasiasa na vyombo vya habari kwa sababu ya ushabiki tu, no brain, no substance and no action, just slogans will that work?
 
Pamoja mkubwa. Mkapa wa kipindi cha Nyerere siyo yule wa miaka mitano ya mwisho. Hata hii sisiemu ilikuwa imekwishaanza kufanya ujinga ndiyo maana Mwalimu aliamua kutundika madaruga (Kurudi Butiama) Tunahitaji mabadiliko, whether Fred atakuwa mamluki (Of which sidhani ni sahihi kutokana na msimamo wake kwa kipindi nilichosikia hoja zake) or atakuwa na dhamira ya kweli, kile kitendo cha kunyoosha kidole na kusema no, enough is enough inatosha kuonyesha njia kwa watu wenye dhamira ya kweli. Mambo ya Chama chajenga nchi yametufikisha pabaya sana. Nchi inajengwa na sisi wenyewe Watanzania na inatafunwa na chama..By the way naona correlation kati ya fund rising ya uchaguzi huu 40 Billion na ile iliyokwapuliwa BOT kipindi kile kwa kutumia kampuni ya kastuli ambayo hadi leo haiguswi. Hapa chama kilijenga nini na hiyo 40 Billion zaidi ya kubomoa nchi?Bravo Fred.

Unachekesha kweli eti alitundika madulaga .

Uamuzi mzuri kafanya. Mie nampongeza sana kwa sababu hakuhamia ktk vyama vikongwe vya upinzani hapo mie nimempa 100%

Watu tusidanganyike.
KWa vyovyote vile jinsi vyama vinavyoongezeka muathirika mkuu wa kupungukiwa ni CCM , vyama vingine vinaathirika kidogo sana. Wanaosema vinginevyo wanajifariji tu.
 
Mwanasiasa yeyote wa maana anapoikimbia CCM anatusogeza mbele katika mapambano yetu ya ukombozi dhidi ya nduli CCM. Nampongeza sana Ndugu Mpendazoe. Nampongeza zaidi kwa kutobabaishwa na vijisenti hata akaamua kuacha ubunge wake kabla ya kupata hiyo inayoitwa pensheni.

Nawakemea kwa jina la JF wote wanaojaribu kumkatisha tamaa. Katika kipindi hiki cha materialistic Tanzania hatuhitaji sauti za kukatisha tamaa watu wenye ujasiri na moyo wa kupambana. Bravo Mpendazoe and welcome to the club.
 
bado shoo lingine ni kupigana chini kwenye kura za maoni ,,,,hahaaaaa.........ngoja niweke order ya pop corn pale mlimani city for the coming 6 months

Kaka tuombe uhai, kweli big screen tu mwaka huu maana ticket wengine tumezikosa, utamu utamu tu, nimepata tetesi kuwa watu wanapima upepo huenda midubwana zaidi ikapendazoe vile vile.
 
Frederick Mpendazoe ameonyesha njia huyu ni mpambanaji kweli kweli.

Nafikiri ametuma signal kuwa hana mzaa kabisa. Uwezi kuwa na adui yako nyumba moja.

FISADI ni adui wa maendeleo ya watanzania na fisadi huyo yuko CCM, utakaa naye vipi bila kuwa mpinga maendeleo?
 
Kama wabunge na vigogo wengine wanasoma JF, nadhani watapata nguvu ya kuchukua uamuzi kama wa Fred. jitokezeni, hakuna cha kuogopa tena.
 
Kazi kubwa naona hata mwananchi gazeti wamesha weka kama breaking news . Ila sitaki kuamini kwamba chama cha upinzani wa kweli utatoka CCM . Naamini Chadema ni sahhi na mengine ni ongezeko la Vyama .

Kumekucha mwaka 2010
 
KUMEKUCHA .... Kumbe CCJ sio ya kubezwa jamani. Vigogo waanza kujiweka wazi na kujiunga!.... Lisemwalo lipo....!!

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga, (CCM), Fred Mpendazoe, amekihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Jamii (CCJ), ambacho ni kipya kikiwa bado katika hatua za kujipatia usajili wa kudumu.

Mbunge huyu, ambaye anatambulika kuwa ni mmoja kati ya wapambanaji dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga, (CCM), Fred Mpendazoe, amekihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Jamii (CCJ), ambacho ni kipya kikiwa bado katika hatua za kujipatia usajili wa kudumu.

Mbunge huyu, ambaye anatambulika kuwa ni mmoja kati ya wapambanaji dhidi ya ufisadi ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari leo asubuhi jijini Dar es Salaam.
ufisadi ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari leo asubuhi jijini Dar es Salaam.
SOURCE: http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18853
 
Hii habari kubwa.

Hongera Mpendazoe. Wala usikatishwe tamaa na yeyote. Unaweza ukawa legend katika taifa letu huko mbeleni.

Mwanakijiji ulikuwa unajua kitu kuhusu hii CCJ. Ila ulikuwa unabania bania. Any more hints?
 
Kama wabunge na vigogo wengine wanasoma JF, nadhani watapata nguvu ya kuchukua uamuzi kama wa Fred. jitokezeni, hakuna cha kuogopa tena.

Umenena HH. Ingawa karibu 97% ya wanaJF wanasupport hatua ya ujasiri wa Mpendazoe, asilimia kubwa ya Watanzania, hasa wale wa vijijini walio chini la blanketi la umasikini bado wanasapoti CCM. Uduni wa hali yao unasababishwa na utashi wa CCM ili waendelee daima dumu kukisapoti na kukiona ndiyo mkombozi, hasa wakati wa uchaguzi wanapojisikia wametajirika kwa TShirt (bila bottoms).

CCM wanajua fika kwamba hawa wakianza tu kupata maendeleo, hasa elimu, basi wamekwisha!
 
Huu ni unafki hakuna lolote

huyu jamaa tangu awali alikuwa anajua kwamba kule jimboni hapati kitu kabisa

sasa anahaha kwa maana ya kuona namna ya kurudi kwenye jimbo
 
Umenena HH. Ingawa karibu 97% ya wanaJF wanasupport hatua ya ujasiri wa Mpendazoe, asilimia kubwa ya Watanzania, hasa wale wa vijijini walio chini la blanketi la umasikini bado wanasapoti CCM. Uduni wa hali yao unasababishwa na utashi wa CCM ili waendelee daima dumu kukisapoti na kukiona ndiyo mkombozi, hasa wakati wa uchaguzi wanapojisikia wametajirika kwa TShirt (bila bottoms).

CCM wanajua fika kwamba hawa wakianza tu kupata maendeleo, hasa elimu, basi wamekwisha!

Sure. Tanzania ina-lack middle class ya kuweza kufikiri na kupiga kura kwa busara kwa mustakabali wa taifa lao, kwani kwa hali ya umasikini wao wa sasa wanachojua ni CCM tu kama vile wamageuzwa kuwa ma-zombie!
 
Kama wabunge na vigogo wengine wanasoma JF, nadhani watapata nguvu ya kuchukua uamuzi kama wa Fred. jitokezeni, hakuna cha kuogopa tena.

Ndiyo hayo wanayodai "Kupima upepo" hao wapimaji upepo kama watachelewa basi sina imani nao kwasababu "there is a difference btn doing the right thing vs the thing right"

Kama ni kweli wana uzalendo basi wanatakiwa wafanye whats right and not neccessarily whats popular.....

Inaweza kuwa its unpopular kujitoa ccm,wengine wanakuja na mifano ya kina Mrema.

Na wale wenye mwelekeo wa mawazo ya kifisadi watatoa sababu pia,na wengine wanafananisha na kina Njelu Kasaka et al.

However this time around ni tofauti sana....Mpendazoe keshaanza na kama kuna wenye nia hiyo wafanye sasa kwani wakichelewa watakuja kuwaponza wale wenye nia nzuri na chama hicho cha ccj,wenye kuweka uzalendo mbele na si wenye kufuata whats popular,watu kama kina Mpendazoe,kwani hawaoni tayari amegain exctra credit machoni pa wengi wetu kwa kuamua kuachana na mafao yake ya ubunge?Kwa tabia za wengi wetu watanzania,hilo tu ni la kumpongeza.

Wengine wakiwa hawaamini kabisa kwamba ameyaacha mafao yake ya miezi kadhaa,na pia wanajiuliza kwanini kafanya hivyo!?Hapo utashangazwa na wengi wetu wanavyofikiri....Yani kuna mashabiki wa maslahi binafsi wazi wazi kabisa hata hapa JF,inawezekana mafisadi tumo nao humu ndani....Haiwezekani ujiulize eti kwanini kayaacha mafao yake ya miezi kadhaa bila kujiuliza kama alichofanya yani kuhama ccm ni kwa maslahi binafsi ama ya wananchi!
 
Umenena HH. Ingawa karibu 97% ya wanaJF wanasupport hatua ya ujasiri wa Mpendazoe, asilimia kubwa ya Watanzania, hasa wale wa vijijini walio chini la blanketi la umasikini bado wanasapoti CCM. Uduni wa hali yao unasababishwa na utashi wa CCM ili waendelee daima dumu kukisapoti na kukiona ndiyo mkombozi, hasa wakati wa uchaguzi wanapojisikia wametajirika kwa TShirt (bila bottoms).

CCM wanajua fika kwamba hawa wakianza tu kupata maendeleo, hasa elimu, basi wamekwisha!

Zak,

Zikiambatana Mungu ndie muweza. Mjanja kuwa CCM, freed from TRA and elites
 
Mwacheni aende atuachie Chama Chetu.

Kama mtu anashindwa kushawiji hoja ndani ya vikao vya chama, na agenda zinapoamuliwa akatika bila kuridhika na kuishia kunung'unika kwenye vyombo vya habari, basi huyo si mwenzetu!

He was a liability, opportunistic and actually a spent force. Kama kuna wengine wenye mtazamo kama wa mwanasiasa huyu, ni bora wamfuate mapema kwani kwenye uchaguzi mkuu watachujwa na hawatapewa nafasi ya kugombea.
 
Ndiyo hayo wanayodai "Kupima upepo" hao wapimaji upepo kama watachelewa basi sina imani nao kwasababu "there is a difference btn doing the right thing vs the thing right"

Kama ni kweli wana uzalendo basi wanatakiwa wafanye whats right and not neccessarily whats popular.....

Inaweza kuwa its unpopular kujitoa ccm,wengine wanakuja na mifano ya kina Mrema.

Na wale wenye mwelekeo wa mawazo ya kifisadi watatoa sababu pia,na wengine wanafananisha na kina Njelu Kasaka et al.

However this time around ni tofauti sana....Mpendazoe keshaanza na kama kuna wenye nia hiyo wafanye sasa kwani wakichelewa watakuja kuwaponza wale wenye nia nzuri na chama hicho cha ccj,wenye kuweka uzalendo mbele na si wenye kufuata whats popular,watu kama kina Mpendazoe,kwani hawaoni tayari amegain exctra credit machoni pa wengi wetu kwa kuamua kuachana na mafao yake ya ubunge?Kwa tabia za wengi wetu watanzania,hilo tu ni la kumpongeza.

Wengine wakiwa hawaamini kabisa kwamba ameyaacha mafao yake ya miezi kadhaa,na pia wanajiuliza kwanini kafanya hivyo!?Hapo utashangazwa na wengi wetu wanavyofikiri....Yani kuna mashabiki wa maslahi binafsi wazi wazi kabisa hata hapa JF,inawezekana mafisadi tumo nao humu ndani....Haiwezekani ujiulize eti kwanini kayaacha mafao yake ya miezi kadhaa bila kujiuliza kama alichofanya yani kuhama ccm ni kwa maslahi binafsi ama ya wananchi!

What is genuinely a popular move must be the right one. How do you convince me that fred's move is not genuinely popular.
 
Back
Top Bottom