John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Picha: Fredrick Lowassa
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa kupitia mtandao wake wa Instagram, ameandika kuwa jamii ya Wamasai kutoka Ngorongoro ni Watanzania na wana haki sawa Kama Watanzania wengine.
“Wamasai wa Ngorongoro ni Watanzania na wana HAKI sawa kama Watanzania wengine. Tofauti kubwa ni kabila letu kulinda utamaduni wetu ambao pia umekuwa kivutio kikubwa cha utalii ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.
“Naamini Watanzania wote tunafahamu heshima hii ya Ngorongoro Crater kama moja ya maajabu ya dunia na mtaji mkubwa sana kiuchumi kwa Nchi yetu.
“Nadhani ni muda sahihi sasa kwa Serikali KUIWEZESHA Mamlaka ya Hifadhi ya NgoroNgoro ili kulinda hifadhi yetu na kurejesha mahusiano mazuri ya wanyama na binadamu kama ambavyo imekuwa tangu kuanzishwa kwa hifadhi hii mwaka 1959.
“Hoja ya wingi wa mifugo na zozote zingine zinajadilika kukiwa na mahusiano mazuri na wananchi. Tunaiamini Serikali ya Mama Samia Saluhu Hassan ni sikivu,” ✍🏽 - Fred Lowassa.