Fredwaa anapotea, ajitathimini upya, pesa si kila kitu

Clouds waligundua hilo ndio maana wakamsogeza aanze peke yake mapema.....ile staili ya PB ni ngumu kwa Fredwaa....

Yule ni jeshi la mtu mmoja....hawezi zile porojo za akina Hando.....
 
kweli kabisa Huyu sio fedwaa tuliyemzoea...mm nilikua namsikia nadhan ni mbwiga mpka pale nilipoambiwa ni fred ..mm nasugest apewe kipindi chake au ahame kabisa radio..
 
Miaka ile nimemaliza form six nipo tuu home nilikuwa sikosi kipindi cha Mr Vodacom RFA. Jamaa alikiwa anajua eti sasa hv ni kweli simuoni yule Fredwaa wa RFA.

Ingawa sio msikilizaji wa radio. Ni wapo kijiji nilikuwa sikosi kipindi cha vodacom na Fredwaa RFA.
 
Kiukweli siku hizi nikiisikia sauti yake nashindwa kuitambua,na hata nikiambiwa ni yeye nimekuwa nikiamini ni mgonjwa...amepooza sana..
 
Kipindi cha power breakfast kinahitaji watangazaji waongeaji sana na utani mwingi ndo maana hata akiwa fredwaa na babra bado utaona kuna mapungufu kwa style PB waachwe wakina hando ...fredwaa lazima abuni kipindi chake mwenyewe ili awe katika ile level yake otherwise anapotea
 

Nadhani aamue moja pale hatumiki anasindikiza wenzake amekuwa nyuma hata ya Babra
 
ni kweli kabisa, clouds wameshindwa kumtumia huyu jamaa. wakiendelea vile ni heri aondoke tu atafute sehem nyingine, tatizo na yeye apunguze ulevi, kunywa wote tunakunywa....lakini ulevi ni uzembe!
 
jamaa alipikuwa RFA alikuwa ni moto wa kuotea mbali,nashauri wampe kipindi cha reggae au old school,hapo tutapata pure hip hop.
PB awaachie wambea wambea wakina on na Hando .that guy is obove PB bana.
 
Kiukweli siku hizi nikiisikia sauti yake nashindwa kuitambua,na hata nikiambiwa ni yeye nimekuwa nikiamini ni mgonjwa...amepooza sana..

afadhali hata alivyokuwa times fm....
 
Hando na PJ wana - style tofauti na Fredwaa (Fred Fidelis)
Aanzishe kipindi kinachofanana na style yake!
Vinginevyo hawezi kucope!
 
Fredwaaa namkumbuka toka enzi za mambo mambo na RFA zikiwa combination kibao ktk kipindi hicho kama Lazaro matalange sauti ya simba,Godwin gondwin na fredwaa mwenyewe nilikuwa Bonge la kipindi pia kipindi cha regge ragga power ila ninachoona mm ni maslahi yanamponza Fred kabla ila nitakukumbuka kwa ubora wako pale RFA na Mr Vodacom na sindano tano za moto na vichekesho vyako.
 
Huna uwezo mkubwa wa kufikri nadhan humjui vizuri fredwaa ndo maana unabwabwaja tu maneno, ukabila umekujaje hapo fredwaa mtangazaji mzuri sana sema kipindi si type yake mwanza imetoa watu wazuri mbona kina Godwin Gondwe.

Fredwaa angekuwa ni mchezo wa mieleka tungesema kwa wapendao huo mchezo kuwa don't try this at school and don't try this at home ni hatari sana hujamaa ni Bonge ya mtangazaji na nihatari hata kwa watangazaji wengine sema pale clouds jamaa bado kuku mgeni kamba mguuni ila kadri cku zinavyozidi kusogea atafunika ile ya mapema nikupasha tu ila nikipaji mbunifu wa vipindi pia alikuwa meneja wa vipindi pale RFA acha wehu kijana.
 
fredwaa angekaa na baba la mababa hasa kipindi cha mchana baada ya xxl ebwana clouds ingetisha maana fredwaa ana unique fulani hivi mchovu naye ebwana acha
 
jamaa alipikuwa RFA alikuwa ni moto wa kuotea mbali,nashauri wampe kipindi cha reggae au old school,hapo tutapata pure hip hop.
PB awaachie wambea wambea wakina on na Hando .that guy is obove PB bana.

sure fredwaaa umbeya hajui awachie hao machoko wanaojiita watoto wa mjini mpaka leo wameajikiwa clouds fm nyambafu
 
Ni sawa na kumsajili mchezaji mkubwa na kumuweka benchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…