Fredwaa (Fredi Fidelis) forgive, forget and move on? PB imepoaaa

Fredwaa (Fredi Fidelis) forgive, forget and move on? PB imepoaaa

Sijawahi muelewa alipoendaga Clouds, sijui nani alimshauri aondoke radio free na kuacha upweke kwenye "SINDANO TANO ZA MOTO" na Ile jumapili kwenye " JE, HUU NI UUNGWANA ? "
Sahara Media wameondoka wengi tu, shida ya pale ni maslahi ndugu, wala usimshangae kuondoka, kabla ya hapo alikuwa Times way back
 
View attachment 1376753
Fred Fidelis aka Fredwaa

Kipindi cha Powe breakfast kimepwaya sana kama sio kupoa, kwa muda wa alfajiri kuanzia saa11 mpaka 12, amsha amsha za Fredwaa hazipo, Utabiri wa Hari ya hewa hamna, Paza Sauti pamoja na Ripoti ya Bonge ya alfajiri hakuna.

Pia zile reggae za alfajiri siku ya Ijumaa hakuna, sasa huyu jamaa ni likizo tu au kuna lingine nyuma ya pazia, imekuwa muda sana hayupo kwenye Kipindi, Inaleta shaka flani kama jamaa kapiga chini hivi, post yake kwenye akaunti ya Instagram siku mbili zilizopita inanipa mashaka, inasema: "FORGIVE, FORGET and move on, everyone got history in their life".

Pia kituo kiko kwenye kampeni ya siku ya mwanamke, na karibu asilimia 90 ya staff wameweka picha ambayo inatangaza kampeni hiyo ila yeye sijaona hiyo kitu.

PM Mr Shafii Dauda fanyeni mpango huyu jamaa arudi, tunajua kwenye riziki yoyote hapakosi husda kama ni hivyo basi weka sawa, kama ni likizo basi wasikilizaji wa kipindi wajuzwe, tumemiss sauti, jingle, drops za Mr Energy Man, hakuna kama yeye hapo.

Namkubali sana huyu mangi...ila tangu PB alivyo ondoka PJ na hando...na mimi nilihama nawo na kwenda E-fm...mpaka leo nipo huku...
Kule siku hizi hamna hamsha hamsha kama zamani wamekuwa double standard...kama wamepangiwa nini cha kuongea
 
Namkubali sana huyu mangi...ila tangu PB alivyo ondoka PJ na hando...na mimi nilihama nawo na kwenda E-fm...mpaka leo nipo huku...
Kule siku hizi hamna hamsha hamsha kama zamani wamekuwa double standard...kama wamepangiwa nini cha kuongea
Ile combo ilikuwa safi sana, Hando, PJ, Fredwaa, Barbra, hawa wote wakongwe, kipindi kilinoga alipoongezeka Masoud, ilivoondoka PJ tu hari ya hewa ikachange, SIZA sio mtangazaji
 
Back
Top Bottom