Freeman Mbowe ajilaumu kwa yanayomkuta - Absalom Kibanda


Huyu naye ni mjinga .
Katiba iliyompa Mbowe Uenyekiti ilimtaka akae madarakani miaka 10 tu.
Kwa maana kubwa 2014 mbowe alitakiwa aondoke na kumwachia mtu mwingine chama.
Kwa hiyo chadema haikujengwa na Mbowe bali ni chama kilichokuwa kutokana na makosa ya muda mrefu ya CCM. Chadema imejijenga kwa wakati na majira ya uongozi mbali mbali .
Kupuuza watu wengine na vyama vingine ni kuua chama . Haiwezekani karne hii ujenge chama kwa kufukuza watu na kuhodhi chama kama mali binafsi eti una uchungu kama Nyerere na Mandela . Hawa walikua wapigania uhuru lakini pia nguvu iliyokua nyuma yao ilikua kubwa . Afrika kusini palikua na nguvu kubwa ya Askofu Desmond Tutu. Nyerere numa yake lilikua kanisa Katoliki na Tanu iliyojengwa muda mrefu.

Nguvu ya Chadema ilikua ni uchaguzi wa 2015 chini ya Edwadi Lowasa aliyekua na nguvu kubwa ya wananchi ndani na nje ya CCM .. Nje ya CCM palikua na nguvu ya taasisi za dini ambazo kiukweli Lowasa alijijengea umaarufu huko kutokana na fedha zake nyingi alizokua anatoa kusaidia taasisi hizo.
Kama CCM ingemsimamisha Liwasa ni wazi kuwa CCM ingepata kura nyingi sana na CUF ingeendelea kubwa chama kikuu cha upinzani. Mbowe alikua ameanza kupata upinzani mkali ndani ya chama tangu mwaka 2014 .Mbinu alizotumia ni hizi hizi za kuwatuhumu wapinzani wake kuwa wanataka kuua chama . Unauaje chama unachokiongoza. Chama kinakufa kwa kung'ang'ania madaraka.
Zito angeongoza chama mpaka leo angeendelea mwingine ,Wanachama wote waliotoka CUF wangehamia chadema na Chadema kingekua ni sehemu ya maridhiano ya serikali . Lakini kwavm sasa hakuna maridhiano ya serikali na Chadema ndio maana waliokua wanaridhiana ni viongozi wa CCM na Wa chadema yaani Kinana na Mbowe . Hakuna maridhiano ndio maana hakuna uchaguzi wa kukubali ushindi wa chadema popote kwenye uchaguzi . Maridhiano yapo kule Zanzibar na yapo kikatiba sio usanii wa Mbowe.
Anaanzisha maridhiano kwa Hadaa na anayaondoa mwenyewe kwa kutaka kufanya uhaini wa kumtoa rais madarakani kwa maandamano . Huu ukawa mwisho wa maridhiano ya Hadaa.
Huu ndio umahiri wa Mbowe unaoweza kumlinganisha na Mandela?
2014 hata angegombea Rwekatare na kupata Uenyekiti angafikia ukomo mwaka 2025 na kumwachia mwingine na chama kingekua na wabunge na madiwani wengi .
JPM aligoma kupingwa na dikteta asiye na dola. Yaani Mbowe hana ukomo wa uongozi halafu anataka katiba ya Warioba tena kwa maandamano !! Huu ni uhuni ! Mbowe hataki kupingwa halafu anataka vyama vya upinzani viipnge serikali !! ,Huu ni upumbavu.
Mbowe anataka uchaguzi wa huru na haki halafu yeye hataki uhuru ndani ya chama chake. Uhuru kwake ni usaliti na kutumiwa . Hizi ni kauli za madikteta duniani kote.
Mbowe hana sifa tena za kuwa kiongozi wa chama cha kupigania demokrasia . Mbowe ni mbaya kuliko Mwenyekiti yeyote Wa CCM aliyewahi kutokea.
 
LIssu anafurumusha matusi kwa kila mtu.
Hana sifa ya kuwa kiongozi yule
 
Propaganda za ku keep busy huku mtifuano was wagombea urais ukiendelea Chaka kikuu!!
 
Tofauti na unavyosema, hakuna aliyepinga Lissu kuchukua fomu. Hata Mbowe hajawahi kutamka hivyo hadharani. Tunachopinga ni:
1. Juhudi za kutaka kumlazimisha Mbowe asigombee. Na zilianza kabla hajatangaza nia.
2. Kampeni chafu inayoendeshwa dhidi ya Mbowe. Ilianza pale Lissu alipochukua fomu. Kwa kiasi kikubwa Lissu ameshiriki ama kwa kuzinyamazia, kuziunga mkono kimafumbo au kwa uwazi kabisa.

Wengi wetu tungefurahia ushindani ambao ungejikita katika kuhakikisha chama kinabaki salama tofauti na huu unaoendelea.

Mshindi hapa ni wapinzani na washindani wa Chadema.

Amandla...
 
Nililiona andiko hili nikawa nalipita bila kusoma nikijipa muda wa kutafakari kwanza heading ili niweze kuja kusoma na kujadili. Kimsingi nimeona hoja ya Kibanda imejikita kwenye kampeni zaidi na imejielekeza kwenye destructive politics.

  1. Kibanda anamlaumu Mbowe kwa kumjenga Lisu ambaye leo amesimama kupingana naye katika uwaniaji nafasi ya uenyekiti CHADEMA Taifa.
  2. Absalom Kibanda haamini katika siasa za ushindani. Anajenga hoja kuunga mkono usultani kwenye siasa ambapo tija yake ni ubakaji wa demokrasia na michakato yake
  3. Absalom Kibanda ana turufu yake kwenye uchaguzi huu wa CHADEMA, na katika hoja yake ameonesha anamuunga mkono mgombea yupi.
  4. Mimi binafsi kama Msanii ninaona wazi kwamba injini zote chafu za CCM akiwemo Kibanda wameinuka kutetea uenyekiti wa Mbowe badala ya yeye Kibanda kuweka uchambuzi wa wazi kwa kila mgombea. Nakumbuka kalamu yake ilivyotumika kujenga ule MTANDAO uliomuweka Kikwete madarakani kwa kuwachafua wengine, ndicho anachikifanya sasa.
Mbowe mpaka sasa hajasema wala kuanika sababu zake zinazomsukuma kugombea uenyekiti kwa mara nyingine tena. Anapaswa kupumzika kwa heshima ili asomeke kama baba wa demokrasia nchini. Ameshatia doa historia aliyoijenga kwa muda mrefu...
 
Achukue fomu, agombee lakini aache kumdhihaki Mbowe kwenye majukwaa. Kuna maisha baada ya 21, Januari
 

Bush Dokta ni huyu ndugu?
 
Siasa za Afrika haziwezi kuwa na tija mpaka kwanza zitoke kujadiki watu ziende kujadili issues.

March 14 1995, kuelekea uchaguzi mkuu wa 1995, Mwalimu Nyerere katika mkutano wake na waandishi wa habari pale Kilimanjaro Hotel, alitoa somo kubwa ambalo mpaka leo karibu miaka 30 baadaye, Watanzania wengi hawajajifunza bado.

Mwalimu aliulizwa kuhusu mgombea aliyekuwa anazungumwa na watu wengi sana kipindi kile, Augustine Lyqtonga Mrema, aliulizwa atie maoni yake kuhusu Mrema.

Mwalimu alisema hayuko tayari kumzungumzia mtu, yuko pale kuzungumzia sifa za mgombea anayefaa kuwa rais. Kuingelea issues, si watu.

Mpaka leo naona watu wengi wanajikita kwenye siasa za kuzungumzia watu sana zaidi ya issues.
 
Mzee wangu absalom nakuheshimu sana tena saana, lakini kwa hili umepotea na nimekusamehe bure kwa umri wako
 
Ubunifu gani anaongelea wa kuitisha maandamo na kutoka,yeye na binti yake?
 

vifo vya wanachama freeman anahusika
 
Hivi kuna watu wanayaamini haya maridhiano kwamba yanakwenda popote pa maana?

Unafanyaje maridhiano na mtu ambaye bado anateka na kuua watu wako?
hapo sasa. Kuwafanya waTz wote ni wajinga huleta maudhi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…