Anaandika Absalom Kibanda
Katika hili kundi lililofungiwa sina cha kuficha hata kimoja. Usitumie moyo au ulimi kufikiri.
Jeuri na nguvu ya CHADEMA leo ni matokeo ya kazi ya kutukuka ya Freeman Aikaeli Mbowe.
Mkwamo wa Chadema leo unatokana na Mbowe kukumbatia sana makosa ya Lissu na wasaidizi wake kwa manufaa ya Chadema, lakini leo yeye ndiye anapigwa. Chadema imejitoa katika maridhiano kwa sababu ya Mbowe kukubali kutekwa na akina Lissu. Yote haya ni matokeo ya makosa ya kujutia huyo huyo Freeman Aikaeli Mbowe.
Jeuri, kiburi na hata uzima wa Tundu Antipasi Lissu ni matokeo ya uongozi mahiri wa Freeman Aikaei Mbowe.
Mashabiki na maadui wa Freeman Aikaeli Mbowe leo walio ndani na nje ya CHADEMA leo ni zao la uongozi wa Freeman Aikaeli Mbowe.
Mbowe ni kiongozi shupavu na mjenzi, Lissu ni mwanaharakati machachari. Mbowe ni mbunifu, Lissu ni zao la ubunifu wa Mbowe.
Unaweza kumfananisha Mbowe na Mwalimu Nyerere katika kujenga chama au na Nelson Mandela kwa kujitoa kwa ajili ya watu wake.
Unaweza kumfananisha Lissu na Chris Hani kwa misimamo
Mikali au Christopher Mtikila kwa upambanaji na zaidi Augustine Mrema kwa kushabikiwa.
Unao uhuru wa kuchagua
..maridhiano kati ya serikali, Act, na vyama vingine vya siasa, nayo hayajafanikiwa. Serikali na Ccm imepuuza mapendekezo ya Tume ya Prof.Mukandala. Je, hilo nalo unamlaumu Tundu Lissu?