January 2023
Mwanza, Tanzania
Mahojiano exclusive/maalum na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Ajenda ya CHADEMA kuanzia sasa 2023 na kuendelea kuelekea mbele
Freeman Mbowe akiongea katika kipindi cha Kinaga Ubaga juu ya safari waliyoanza ya mikutano ya hadhara na pia CHADEMA kutimiza miaka 30 tangu kuasisiwa na kusajiliwa kama chama cha siasa.
Mtangazaji nguli nchini Bw. Dotto Bulendu anafanya mahojiano rasmi na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
Itikadi ya ujamaa ili feli chini ya CCM ya Mwalimu Nyerere na sisi mapema kabisa CHADEMA tuliona hilo hivyo tukaja na itikadi ya mrengo wa kati kulia siasa za uhuru wa soko na utu wa binadamu unaozingatia uhuru na haki ya kujiletea maendeleo ya watu na uchumi wa nchi ulio mikononi mwa watu huku nchi ikiwa na serikali ndogo isiyowagharimu pakubwa walipa kodi.
Miaka 30 ya vyama vingi imekuwa na mchanganyiko wa changamoto nyingi hasi ambazo zilifanya baadhi kukimbia vyama vinavyobainishwa kama vyama vya upinzani.
Akijibu swali la Dotto Bulendu kwamba CHADEMA kama chama kinara kinachotamani kushika dola, je kuna uwezekano wa tena kuunda ushirikiano na vyama vingine? Freeman Mbowe, "inawezekana lakini inategemea kama kuna mazingira pia makubaliano na misingi inayofanana yanayoruhusu hilo kutokea."
Freeman Mbowe anajibu swali la Propaganda ya vyama vya kijamaa kama CCM kwamba kuna dhana ya kuwa vyama vingi vitaharibu amani, umoja na utaifa kupitia ukabila, dini, ukanda n.k ili kuwagawa raia wasiamini vyama kama CHADEMA.
"Jambo la faraja katika miaka 30 ya vyama vingi ni kuwa, sisi CHADEMA ni mkusanyiko wa itikadi halisi tofauti na CCM ambayo ni kikundi cha watu wasio na ujamaa bali wamejikusanya kujitafutia fursa, kupata ulinzi wa dola kikundi hicho kujineemesha binafsi lakini kwa CHADEMA tumeweza kuwa na watu wenye imani ya uhuru na haki katika chachu ya ustawi wa maendeleo ya kweli ya watu na haki zao kulindwa kisheria na kikatiba," Mbowe.
Mwendesha kipindi Dotto Bulendi anauliza swali lililobeba mahojiano exclusive na mwenyekiti wa Freeman Mbowe kuhusu Ajenda ya CHADEMA kuanzia sasa 2023 na kuendelea baada ya milango ya mikutano kufunguliwa ni ......
Freeman Mbowe kwa niaba ya CHADEMA anadadavua kwa kina KATIBA umuhimu wa kuchukua mapendekezo ya Katiba ya Warioba, Katiba Mpya, Bunge Huru, Madaraka makubwa ya Rais, Mkutano wa Kitaifa wa Makundi yote kujadili mustakabali wa taifa tofauti na bunge maalum la katiba kama lile la 2014 lililosheheni na kuelemewa na wingi wa wajumbe wa CCM hivyo kuogopa kumaliza zoezi la katiba mpya, uchaguzi wa 2025 ....
Kuhusu Maendeleo ya Watu ambayo ni sera ya CHADEMA Mwenyekiti Freeman Mbowe anasema hakuna ujanja Maendeleo ya Watu yapo kwenye sekta ya kilimo, biashara, uvuvi, mifugo na viwanda ambapo CCM imeshindwa anabainisha kwanini na sababu ya CCM pamoja na miaka yote ...
Maendeleo ya Vitu na athari zake kwa mfano hai kabisa Asilimia 95 ya sekta ya ujenzi wa madaraja, barabara na miundo mbinu ya matrilioni ya shilingi tena ktk fedha ngumu ya kigeni wanalipwa makampuni ya nje huku fedha hizo zotezinakwenda China na Uturuki ...... badala ya fedha hizo kuingia ktk mzunguko wa fedha ndani ya Tanzania na katika mifuko na pochi za watanzania .... si ajabu watu wanalia fedha imepotea mtaani na vijijini ..... mwenyekiti Mbowe anafafanua CHADEMA itafanyaje fedha hizo matrilioni ya shilingi zibaki ndani ktk mzunguko utakaofaidisha kampuni za ujenzi na watanzania kuziona zikiingia ktk maisha yao ya kila siku ....
Mikopo na deni la taifa inagusiwa iliyochukuliwa kulipa miradi inayoendelea ya kampuni za ujenzi ya miundo mbinu fedha ambazo zinaenda nje ya nchi .......
TOZO, KODI, MISAADA ...... kwa ajili ya Maendeleo ya Vitu, lazima tujifunze kushona nguo kwa kulingana na ukubwa wa kitambaa chetu anasema mwenyekiti wa CHADEMA taifa ......
Serikali imeangazia zaidi Matumizi / Expenditure badala ya Uzalishaji / Production na hilo ni kosa kubwa hivyo sisi CHADEMA tunasema .... ukimkuta mzazi anasisitiza familia ile kwa kukopa kwa jirani badala ya kufikiria uzalishaji basi watazidiwa na madeni na ndicho serikali ya CCM .....
Deni Himilivu siyo kigezo inabidi kubadili mtizamo katika kukopa, CHADEMA ina shauri serikali ....
Matumizi Makubwa ya Uendeshaji wa serikali CHADEMA tumelalamika sana kuhusu hilo ... ofisi ya mkuu wa mkoa, ofisi ya mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa wilaya huko kote ni msisitizo wa matumizi badala ya kuchochea uzalishaji ktk sekta za kilimo n.k ....
Source : SAUT Digital