Freeman Mbowe alalamikia Uhamiaji uwanja wa ndege Nyerere kwa kumsumbua Mtoto wake ambaye ni raia wa Marekani kuingia nchini

Kumbe kuwa na mtoto raia wa Marekani by birth kumeanza kitambo.

Nakumbuka Nasari yeye alitelekeza bunge ili ahakikishe mwanae anazaliwa Marekani.
Kabisa
 
Mwaka 2014 Freeman Mbowe gari yake yake akiwa kiongozi mkuu bungeni ya Bunge ikikamatwa Mombasa na huyo mwanawe mmarekani baada ya kushindikana kupitia Airport ya Mwalimi Nyerere Dar kaingikia Mombasa kuingia Tanzania kuna mtu aweza connect dots?

Habari ya 2014 hii hapa

"GARI la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, limekamatwa na kuendelea kushikiliwa mjini Mombasa nchini Kenya, kutokana na kuwa na namba mbili.

Taarifa kutoka Kenya zilizolifikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa polisi nchini Kenya walipata taarifa za kuwepo kwa gari hilo na watu ambao walionekana kutokuwa na kazi maalumu.

Baada ya kupata taarifa hizo, Polisi hao walio katika msako wa wageni na magari yanayotiliwa shaka kuhusika katika uhalifu na ugaidi, walianza kulifuatilia na kubaini wahusika wa gari hilo.

Ufuatiliaji huo kwa mujibu wa taarifa hizo, ulibaini wahusika wa gari hilo walipofika Mombasa kutokea Tanzania, hawakuonekana kupokewa na mwenyeji yeyote, hali inayomaanisha wenyewe ni wenyeji wa mji huo.

Taarifa za Polisi zilibainisha kuwa uchunguzi wao ulibaini kuwa gari hilo liliwabeba Mbowe, Mbunge wa Mwanza Mjini, Ezekiah Wenje na dereva Ibrahim Nguzo.

Polisi hao inadaiwa walitilia shaka gari hilo kutokana na kuwa na namba za usajili STK 8146, ambazo zilipandishiwa juu ya nambari halisi za gari hilo ambazo ni KUB.

Uchunguzi wa Polisi hao ulibaini kuwa Mbowe na Wenje waliwasili Mombasa, Kenya kwa gari wakitokea Tanzania kupitia mpaka wa Horohoro/Lungalunga na kwenda moja kwa moja hotelini.

Mashaka kwa Polisi hao yaliongezeka baada ya Mbowe na Wenje Aprili 26 mwaka huu kusafiri kwenda Nairobi kwa ndege, na kumwacha dereva pamoja na gari hotelini.

Kutokana na hali hiyo, Jumatatu wiki hii saa 5.00 asubuhi askari Polisi wa Mombasa walimkamata Ibrahim pamoja na gari hilo, baada ya kuonekana amekaa hotelini muda mrefu bila ya shughuli zozote.

"Hapo ndipo alipotoa habari kwamba alikuwa akiwasubiri wakubwa zake ambao walikwenda Nairobi tangu Aprili 26 na hawakuwa wamerejea," ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ibrahim alipoulizwa kwa nini gari lilikuwa na nambari za kupandishiwa, alijibu huo ulikuwa ni uamuzi wa bosi wake Mbowe.

Polisi hao waliamua kukamata gari hilo na kulipeleka katika kituo cha Polisi cha Kati kwa mahojiano zaidi na baada ya mahojiano, aliachiliwa Ibrahim huru lakini gari limeendelea kuzuiliwa kituoni hadi Mbowe na Wenje watakapofika kwa ajili ya kuhojiwa.

Juhudi za kumtafuta Mbowe na Wenje hazikufanikiwa baada ya simu zao kutokupatikana."

CHANZO: Gazeti la Habarileo la wakati huo
 
Hapa hujamchanganya Mbowe na mzee Makamba kweli? Halafu hiyo sentensi ya mwisho, fikiri tena.
 
Mtoa maada hapa lengo lake ni kufikisha ujumbe ambao wengi hamkumuelewa. Kiufupi mkae mkifahamu hao mnao wapigania siku kikiwaka wanao wa kuwapokwa huko ughaibuni.

..tatizo ni kwanini tupigane?

..tunapaswa kuondokana na imani kwamba siasa ni ugomvi au mapigano.
 
Alafu hawa si ndo wanaotuhamasisha tuandamane,,, kumbe watoto wao wanyamwezi😮
 
Katiba yetu bado haitambui uraia pacha hivyo lazima afuate sheria iliyopo sasa ina uzuri wake pia. Lasivyo wahindi watafaidika sana na uraia pacha na watahamisha resources za nchi yetu bila kizuizi chochote lazima tuwe makini sana na uraia pacha.
 
Kwa hiyo hoja yako ni nini hasa..?

Je, unatupa taarifa kuwa Freeman Mbowe ana mtoto raia wa Marekani..?

Halafu ili iweje..?
 
Kumbe watoto zenu wako huko mbele halafu mnawaambia wetu waandamane
Shangaa na wewe. Kila siku wanatuhamasisha tuingie barabarani sisi watoto wa makapuku, kumbe wao watoto wao wako unyamwezini!
Hamunioni kwenye mandamano ng'oo.
Ujinga mimi siupendi
 
Vibaraka hawa wanaona fahari watoto wao ni wamarekani ndio wanaotumika kuyumbisha na kuhujumu mataifa yetu. Sasa analalamika nini na mwanae kaja kama mmarekani bila visa?

Lissu nae katamba juzi eti watoto wake ni wamarekani. Tusije logwa watanzania tukakabidhi nchi yetu kuongozwa na hawa vibaraka wa mabeberu. Wanachojali wao na kuona fahari ni kulishwa makombo na kuhongwa na wazungu mradi wao na mafamilia zao waende chooni kwa urahisi.
 
Kuna yule waziri wa ccm mstaafu tuliambiwa mwanaye ni mfanyakazi wa TRA ya UK. Natumaini siyo raia wa UK hata kama Malkia alimpa zawadi
Huyo story yake inachekesha,alijifanya eti mzalendo akarudi bongo kulisaidia taifa lake kwenye mambo ya kodi,cha kwanza TRA wakampangia kituo cha kazi kigoma huko na huko kigoma akapelekwa wilaya ya kasulu huko..mbona aliondoka kurudi Uingereza mwenyewe bila hata kuaga..nadhani hana hamu na wabongo hadi leo.
 
Unakurupuka na kutoa povu bure bado kitu ni kilekile. Hata ukizaliwa leo US kama baba na mama sio Raia utabakia kuwa na uraia wa mama mpaka 18yrs. Period. Mimi sina shida na mtoto wa Mbowe kuwa au kutokuwa raia
Katiba yetu bado haitambui uraia pacha hivyo lazima afuate sheria iliyopo sasa ina uzuri wake pia. Lasivyo wahindi watafaidika sana na uraia pacha na watahamisha resources za nchi yetu bila kizuizi chochote lazima tuwe makini sana na uraia pacha.
Mkuu uraia pacha hapa unatoka wapi? Huyo mtoto amekuja kama raia wa kigeni mwenye asilivyake Tanzania. Sasa kwanini azuiwe wakati alistahili kupewa visa kama wageni wengine. Ni hivyo tu
 
Document gani Raia wa Marekani anatakiwa kuwa nazo anapoingia Tanzania?
Unauhakika na hiyo sababu kukosa umaana. Immigration LAZIMA wajiridhishe na documents zako zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…