Freeman Mbowe alalamikia Uhamiaji uwanja wa ndege Nyerere kwa kumsumbua Mtoto wake ambaye ni raia wa Marekani kuingia nchini

Freeman Mbowe alalamikia Uhamiaji uwanja wa ndege Nyerere kwa kumsumbua Mtoto wake ambaye ni raia wa Marekani kuingia nchini

Kumbe kuwa na mtoto raia wa Marekani by birth kumeanza kitambo.

Nakumbuka Nasari yeye alitelekeza bunge ili ahakikishe mwanae anazaliwa Marekani.
Kabisa
 
Mwaka 2014 Freeman Mbowe gari yake yake akiwa kiongozi mkuu bungeni ya Bunge ikikamatwa Mombasa na huyo mwanawe mmarekani baada ya kushindikana kupitia Airport ya Mwalimi Nyerere Dar kaingikia Mombasa kuingia Tanzania kuna mtu aweza connect dots?

Habari ya 2014 hii hapa

"GARI la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, limekamatwa na kuendelea kushikiliwa mjini Mombasa nchini Kenya, kutokana na kuwa na namba mbili.

Taarifa kutoka Kenya zilizolifikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa polisi nchini Kenya walipata taarifa za kuwepo kwa gari hilo na watu ambao walionekana kutokuwa na kazi maalumu.

Baada ya kupata taarifa hizo, Polisi hao walio katika msako wa wageni na magari yanayotiliwa shaka kuhusika katika uhalifu na ugaidi, walianza kulifuatilia na kubaini wahusika wa gari hilo.

Ufuatiliaji huo kwa mujibu wa taarifa hizo, ulibaini wahusika wa gari hilo walipofika Mombasa kutokea Tanzania, hawakuonekana kupokewa na mwenyeji yeyote, hali inayomaanisha wenyewe ni wenyeji wa mji huo.

Taarifa za Polisi zilibainisha kuwa uchunguzi wao ulibaini kuwa gari hilo liliwabeba Mbowe, Mbunge wa Mwanza Mjini, Ezekiah Wenje na dereva Ibrahim Nguzo.

Polisi hao inadaiwa walitilia shaka gari hilo kutokana na kuwa na namba za usajili STK 8146, ambazo zilipandishiwa juu ya nambari halisi za gari hilo ambazo ni KUB.

Uchunguzi wa Polisi hao ulibaini kuwa Mbowe na Wenje waliwasili Mombasa, Kenya kwa gari wakitokea Tanzania kupitia mpaka wa Horohoro/Lungalunga na kwenda moja kwa moja hotelini.

Mashaka kwa Polisi hao yaliongezeka baada ya Mbowe na Wenje Aprili 26 mwaka huu kusafiri kwenda Nairobi kwa ndege, na kumwacha dereva pamoja na gari hotelini.

Kutokana na hali hiyo, Jumatatu wiki hii saa 5.00 asubuhi askari Polisi wa Mombasa walimkamata Ibrahim pamoja na gari hilo, baada ya kuonekana amekaa hotelini muda mrefu bila ya shughuli zozote.

"Hapo ndipo alipotoa habari kwamba alikuwa akiwasubiri wakubwa zake ambao walikwenda Nairobi tangu Aprili 26 na hawakuwa wamerejea," ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ibrahim alipoulizwa kwa nini gari lilikuwa na nambari za kupandishiwa, alijibu huo ulikuwa ni uamuzi wa bosi wake Mbowe.

Polisi hao waliamua kukamata gari hilo na kulipeleka katika kituo cha Polisi cha Kati kwa mahojiano zaidi na baada ya mahojiano, aliachiliwa Ibrahim huru lakini gari limeendelea kuzuiliwa kituoni hadi Mbowe na Wenje watakapofika kwa ajili ya kuhojiwa.

Juhudi za kumtafuta Mbowe na Wenje hazikufanikiwa baada ya simu zao kutokupatikana."

CHANZO: Gazeti la Habarileo la wakati huo
 
Hahaha hivi Dkt Magufuli hana watoto wao si walisherehekea kifp chake. Hata sisi watanzania hakuna kuwasamehe mpaka siku wakija kuomba msamaha kwa hilo jambo. Tena kama mbowe gaidi anapaswa awe jela akisubiri kunyongwa mpaka kufa. Kosa lao kubwa kabisa ndiyo hilo, mbowe gaidi ataendelea kuwa gaidi na hiyo NGO ili ipone inahitaji kubadili uongozi ila chini ya gaidi mbowe nina kuhakikishia hata vyombo vya ulinzi na usalama havina kabisa imani na huyu gaidi kama ilivyo kwa mlamba asali Zitto. Kwa chuki iliyopo juu ya mbowe na genge lake ni kubwa mno na kosa lao ndiyo hilo la kuendelea kusherehekea kifo cha Dkt Magufuli mtu ambaye aliwapenda sana na kuwathaminisha
Hapa hujamchanganya Mbowe na mzee Makamba kweli? Halafu hiyo sentensi ya mwisho, fikiri tena.
 
Mtoa maada hapa lengo lake ni kufikisha ujumbe ambao wengi hamkumuelewa. Kiufupi mkae mkifahamu hao mnao wapigania siku kikiwaka wanao wa kuwapokwa huko ughaibuni.

..tatizo ni kwanini tupigane?

..tunapaswa kuondokana na imani kwamba siasa ni ugomvi au mapigano.
 
Kuna jambo pengine wengine hamfahamu. Ukiwa na mwanao anasoma nje ya Tanzania hasa ulaya na marekani wakati anaingia huko akiwa na miaka chini ya 18 anakuwa minor hibyo yupo kwa uraia wa mama. Akifikisha miaka 18 anauwezo wa kubadili uraia wake. Na watu wengi wamekuwa wakifanya hivyo kwa lengo la kupata favour ya wenyeji mfano unafuu wa ada na utafutaji wa kazi.

Hivyo sio jambo la kushangaza tumeona hata mtoto wa Rais wa George Weah wakati wa kombe la Dunia akiichezea marekani badala ya taifa la baba yake.
Katiba yetu bado haitambui uraia pacha hivyo lazima afuate sheria iliyopo sasa ina uzuri wake pia. Lasivyo wahindi watafaidika sana na uraia pacha na watahamisha resources za nchi yetu bila kizuizi chochote lazima tuwe makini sana na uraia pacha.
 
Akiwa Marekani akiongea na Watanzania waishio Marekani akisema mtoto wake wa kumzaa aliyezaliwa Marekani na mwenye uraia wa Marekani alisumbuliwa Airport Dar kwa saa sita na kuzuiwa kupewa visa ya kuingia nchini hadi ikabidi aondoke aende Kenya ambako aliingia nchini kupitia Mombasa.
Kwa hiyo hoja yako ni nini hasa..?

Je, unatupa taarifa kuwa Freeman Mbowe ana mtoto raia wa Marekani..?

Halafu ili iweje..?
 
Kumbe watoto zenu wako huko mbele halafu mnawaambia wetu waandamane
Shangaa na wewe. Kila siku wanatuhamasisha tuingie barabarani sisi watoto wa makapuku, kumbe wao watoto wao wako unyamwezini!
Hamunioni kwenye mandamano ng'oo.
Ujinga mimi siupendi
 
Akiwa Marekani akiongea na Watanzania waishio Marekani akisema mtoto wake wa kumzaa aliyezaliwa Marekani na mwenye uraia wa Marekani alisumbuliwa Airport Dar kwa saa sita na kuzuiwa kupewa visa ya kuingia nchini hadi ikabidi aondoke aende Kenya ambako aliingia nchini kupitia Mombasa.
Vibaraka hawa wanaona fahari watoto wao ni wamarekani ndio wanaotumika kuyumbisha na kuhujumu mataifa yetu. Sasa analalamika nini na mwanae kaja kama mmarekani bila visa?

Lissu nae katamba juzi eti watoto wake ni wamarekani. Tusije logwa watanzania tukakabidhi nchi yetu kuongozwa na hawa vibaraka wa mabeberu. Wanachojali wao na kuona fahari ni kulishwa makombo na kuhongwa na wazungu mradi wao na mafamilia zao waende chooni kwa urahisi.
 
Kuna yule waziri wa ccm mstaafu tuliambiwa mwanaye ni mfanyakazi wa TRA ya UK. Natumaini siyo raia wa UK hata kama Malkia alimpa zawadi
Huyo story yake inachekesha,alijifanya eti mzalendo akarudi bongo kulisaidia taifa lake kwenye mambo ya kodi,cha kwanza TRA wakampangia kituo cha kazi kigoma huko na huko kigoma akapelekwa wilaya ya kasulu huko..mbona aliondoka kurudi Uingereza mwenyewe bila hata kuaga..nadhani hana hamu na wabongo hadi leo.
 
Wacha uzwazwa unabishana na Mbowe mwenyewe anaesema ni wa kuzaliwa Marekani. Mimba inataka kufikisha kishindo mama mtoto anaenda kwa J1 visa or any visa ili tu atage kule then arudi. Wanasiasa kibao wanawarubuni huku wao wakitengeneza futures na opportunities za familia zao., The list is long hadi mawaziri wenu na wakuu wengi wa vitengo, akina Mbowe waliwafundisha hadi akina Nassary michezo hiyo. A list is long tusitafutane kushikana mashati humu tukiitoa

Hiyo ya minor ya kusoma usiiongee kama kutufanya sie zwazwa humu. Tunafahamu taratibu na utaratibu sio rahisi kama unavyotaka kuiaminisha nzengo,
Unakurupuka na kutoa povu bure bado kitu ni kilekile. Hata ukizaliwa leo US kama baba na mama sio Raia utabakia kuwa na uraia wa mama mpaka 18yrs. Period. Mimi sina shida na mtoto wa Mbowe kuwa au kutokuwa raia
Katiba yetu bado haitambui uraia pacha hivyo lazima afuate sheria iliyopo sasa ina uzuri wake pia. Lasivyo wahindi watafaidika sana na uraia pacha na watahamisha resources za nchi yetu bila kizuizi chochote lazima tuwe makini sana na uraia pacha.
Mkuu uraia pacha hapa unatoka wapi? Huyo mtoto amekuja kama raia wa kigeni mwenye asilivyake Tanzania. Sasa kwanini azuiwe wakati alistahili kupewa visa kama wageni wengine. Ni hivyo tu
 
Document gani Raia wa Marekani anatakiwa kuwa nazo anapoingia Tanzania?
Unauhakika na hiyo sababu kukosa umaana. Immigration LAZIMA wajiridhishe na documents zako zote.
 
Back
Top Bottom