Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,207
- 17,674
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na swaiba wake Godbless Lema wameamua kumtukana hayati Magufuli kwenye ziara zao mikoa ya Tanga, Arusha na Kilimanjaro huku wakimwaga sumu hatari ya ukabila!
Mbowe amesikika mara kadhaa kwenye mikutano yake akiwaambia watu kuwa kipindi cha awamu ya tano kabila la wachaga walinyanyasika sana ikiwemo wote kufukuzwa kazi na kufilisiwa biashara zao. Mbowe anasema mchaga ili apate kazi kwenye kipindi cha Magufuli ilimlazimu kubadili jina lake kutoka la kichaga kwenda la kabila jingine!.
Kumbuka tuhuma hizi nzito na mbaya Mbowe anazimwaga bila ushahidi wowote na vyombo vya dola hazimchukulii hatua yoyote kama vile kumfungulia kesi ya ugaidi kwa kuwachonganisha watanzania.
Je, ni kweli kwa mjibu wa Mbowe kwamba wachaga wote walifukuzwa kazi?
Je, ni kweli kwa mjibu wa Mbowe kwamba wachaga wote walifilisiwa biashara zao?
Mwl Nyerere alishawahi kuonya kuwa mwanasiasa yeyote aliyefilisika sera kichwani huwa anatafuta uuwangwaji mkono kupitia ukabila, dini na rangi.
Je, kwa kauli hizi za Mbowe inashiria amefilisika kichwani? Kwamba akijibanza kwenye ukabila ndiyo atashinda ubunge tena? Yetu macho.