Pre GE2025 Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe kang'ang'ania uwenyekiti ili apige hela za ruzuku gari ya Lissu ni mbovu kutengeneza tu hadi achangiwe na ccm
 
From law technical side, tujadili

Mbowe ataweza kuthibitisha defermation?

sheria inasemaje? soma hapa

A crucial question arising from this line of argument is, who between the appellant and the respondent had a duty to establish the falsity or truthfulness of this allegation? In Uhuru Muigai Kenyatta v Baraza Limited [2011] eKLR Rawal J (as she then was) it was held that the information that causes the defamation, will be assumed to be untrue until the defendant proves otherwise. The onus to prove that the statement is true does not rest on plaintiff; it rests on the defendant.
 
Ingependeza iwapo angeenda Mahakamani kumshataki kabisa badala ya kutoa hilo agizo lake kiSiasa.

Manake hajatoa maelekezo kwamba huo msamaha aombe Kwa njia ipi

Lakini pia hizo 5B anazomdai zilipwe Kwa muda gani
Tajiri Freeman Mbowe amekomaa na hana roho mbaya wala mentality za kimasikini ndio maana amempa nafasi ya kuomba msamaha.

Msigwa njaa inamsumbua bado anaishi kwa kuchumia tumbo.

Kama amenunuliwa ni wazi hana uwezo wa kulipa fidia.
 
Yale yale kama ya kinana na Msigwa hadi akaomba poo... ndilo linaloenda kutokea... Msigwa fanya uungwana mapema kabla mambo hayajawa mambo... kuomba msamaha nayo ni heri, sijui kama unazo hizo billion tano, labda kama mpango ni kukufilisi hadi nyumba....
 
1 Kwamba anaiba pesa za chama kwa kutumia Mbowe Foundation
2. Amegeuza chama kuwa SACCOS yake
3. Chadema digital inamilikiwa na Mbowe kwa manufaa yake

My take: hilo nililitegemea and that is the right way to go!

----

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa, kuomba radhi na kulipa fidia ya shilingi bilioni 5 kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake kutokana na matamshi ya Msigwa yaliyotolewa hadharani baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika barua (notisi ya madai) iliyotolewa Septemba 2, 2024 ikiwa na sahihi ya tarehe 4 Septemba, 2024, mawakili wa Mbowe ambao ni Hekima Mwasipu na wenzake kutoka Matwiga Law Chambers, Msigwa anadaiwa kutoa matamshi ya uongo na kumchafua Mbowe mbele ya umma.

“Msigwa alitumia majukwaa ya mikutano, vyombo vya habari, na hata mitandao ya kijamii kutoa madai ya kumkashifu mteja wetu,” ameleza Wakili Mwasipu.

Imeelezwa kuwa Msigwa alidai kuwa Mbowe ameanzisha "Mbowe Foundation," na anatumia chama cha CHADEMA kwa manufaa yake binafsi. Katika moja ya mikutano yake, Msigwa alinukuliwa akisema, "Mwenyekiti wa CHADEMA amegeuza chama kuwa SACCOS, fedha za chama zinaishia kwenye taasisi binafsi na si kwenye akaunti za chama.”

Mawakili wa Mbowe wameeleza kuwa matamshi hayo yameathiri sifa ya Mbowe ndani na nje ya Tanzania, hasa kutokana na nafasi zake mbalimbali kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia vya Afrika (DUA).

“Mteja wetu anaona maneno yote yanayozungumzwa na kunukuliwa hapo juu katika maana yake ya asili, muktadha na misemo kuwa ni kashfa, dharau na kudhuru sio tu sifa yake binafsi bali pia kwa familia yake yote, marafiki, taaluma (Siasa), Jumuiya ya Biashara, Jumuiya ya Kidini, marafiki na rika. Maneno haya si chochote lakini ushahidi dhahiri wa nia mbaya dhidi ya mteja wetu”, imeelezwa na mawakili.

Mbali na hilo, Msigwa alidai kuwa CHADEMA Digital ambayo ni huduma ya usajili wa wanachama, inamilikiwa na kampuni binafsi na kwamba Mbowe anatumia fedha za chama kwa manufaa binafsi.

“Hali hii imeleta hasara kubwa kwa mteja wetu kwani sifa yake ya kiongozi wa kisiasa, mfanyabiashara na mwanafamilia imeathirika sana,” alisema Mwasipu.

Kwa mujibu wa notisi hiyo, Msigwa anatakiwa kuomba radhi kupitia machapisho katika magazeti mawili; moja lenye kuweza kufikia nchi nzima na lingine ambalo linaweza kuwafikia watu walau wa kanda, na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5, la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

View attachment 3088476View attachment 3088473View attachment 3088474View attachment 3088475
Kaingia 18 mbowe, hivi Chadema wakifunguliwa Kesi za kuwaita maneno machafu watu wa CCM Kuna ataepona?
 
Akalipie kesi ya ugaidi ama

Pia soma

View attachment 3088476View attachment 3088473View attachment 3088474View attachment 3088475

Pi
 
Kudadadadeq
 
Attachments

  • FB_IMG_1719903252490.jpg
    FB_IMG_1719903252490.jpg
    26.2 KB · Views: 2
Mbowe kama kuambiwa ukweli kidogo tu anakimbilia mahakamani badala ajibu hoja na kujisafisha je siku akiwa Rais ataweza kuvumilia maneno? Au ndo atapeleka kila mwananchi mahakamani na ikiwezekana kuwa mtekaji pia
Unaniambia mwizi halafu nikuache? Utakuwa jinga la kutupa! Wezi wanapigwa petrol, hivyo unataka na yeye apigwe petroli? Msigwa atafilisiwa.
Namshauri Mbowe aweke zuio la maliza Msigwa asije kuzificha Erythrocyte mtonye Mbowe weke zuio mali za Msigwa kesho zije kumlipa fedha zake
 
Mbona huyu mbowe ni mtu wa madili sana.
Lisemwalo lipo,na Bado zile dili zao na akina J.thirty.
Vipi dili lake la 10% kubuma na kuamua kuwafukuza uvico 19.
 
Wakati Mbowe na wenzake wa CHADEMA na CHADEMA Digital wakidhihaki familia na kumnanga Hayat Rais John Pombe Magufuli pamoja na kashfa zisizo kuwa na vichwa wala miguu, mie nilikuwa bize nakusanya hela, ushahidi na mashauri mengine tayari kuwapeleka mahakamani wale wote, waliowezesha kashfa hizo kusambaa for Defamation.

Hatahivyo Wanasiasa wasitumie Mahakama kwa ajili ya siasa zao chafu.

Siku zinawadia. Karma is a Bitch.
==========
Mbowe must go.
 
Back
Top Bottom