Pre GE2025 Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina

Pre GE2025 Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe kama kuambiwa ukweli kidogo tu anakimbilia mahakamani badala ajibu hoja na kujisafisha je siku akiwa Rais ataweza kuvumilia maneno? Au ndo atapeleka kila mwananchi mahakamani na ikiwezekana kuwa mtekaji pia
Mtekaji kama ninyi mnavyofanya sio
 
1 Kwamba anaiba pesa za chama kwa kutumia Mbowe Foundation
2. Amegeuza chama kuwa SACCOS yake
3. Chadema digital inamilikiwa na Mbowe kwa manufaa yake

My take: hilo nililitegemea and that is the right way to go!

=====


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa, kuomba radhi, asipfanya hivyo ajiandae kulipa kulipa fidia ya shilingi bilioni 5 Mahakamani kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake kutokana na matamshi ya Msigwa yaliyotolewa hadharani baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika barua (notisi ya madai) iliyotolewa Septemba 2, 2024 ikiwa na sahihi ya tarehe 4 Septemba, 2024, mawakili wa Mbowe ambao ni Hekima Mwasipu na wenzake kutoka Matwiga Law Chambers, Msigwa anadaiwa kutoa matamshi ya uongo na kumchafua Mbowe mbele ya umma.

“Msigwa alitumia majukwaa ya mikutano, vyombo vya habari, na hata mitandao ya kijamii kutoa madai ya kumkashifu mteja wetu,” ameleza Wakili Mwasipu.

Imeelezwa kuwa Msigwa alidai kuwa Mbowe ameanzisha "Mbowe Foundation," na anatumia chama cha CHADEMA kwa manufaa yake binafsi. Katika moja ya mikutano yake, Msigwa alinukuliwa akisema, "Mwenyekiti wa CHADEMA amegeuza chama kuwa SACCOS, fedha za chama zinaishia kwenye taasisi binafsi na si kwenye akaunti za chama.”

Mawakili wa Mbowe wameeleza kuwa matamshi hayo yameathiri sifa ya Mbowe ndani na nje ya Tanzania, hasa kutokana na nafasi zake mbalimbali kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia vya Afrika (DUA).

“Mteja wetu anaona maneno yote yanayozungumzwa na kunukuliwa hapo juu katika maana yake ya asili, muktadha na misemo kuwa ni kashfa, dharau na kudhuru sio tu sifa yake binafsi bali pia kwa familia yake yote, marafiki, taaluma (Siasa), Jumuiya ya Biashara, Jumuiya ya Kidini, marafiki na rika. Maneno haya si chochote lakini ushahidi dhahiri wa nia mbaya dhidi ya mteja wetu”, imeelezwa na mawakili.

Mbali na hilo, Msigwa alidai kuwa CHADEMA Digital ambayo ni huduma ya usajili wa wanachama, inamilikiwa na kampuni binafsi na kwamba Mbowe anatumia fedha za chama kwa manufaa binafsi.

“Hali hii imeleta hasara kubwa kwa mteja wetu kwani sifa yake ya kiongozi wa kisiasa, mfanyabiashara na mwanafamilia imeathirika sana,” alisema Mwasipu.

Kwa mujibu wa notisi hiyo, Msigwa anatakiwa kuomba radhi kupitia machapisho katika magazeti mawili; moja lenye kuweza kufikia nchi nzima na lingine ambalo linaweza kuwafikia watu walau wa kanda, na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5, la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Pia soma

View attachment 3088476View attachment 3088473View attachment 3088474View attachment 3088475
Uchaguzi wa TAMISEMI upo mlangoni mjue
 
Mbowe kama kuambiwa ukweli kidogo tu anakimbilia mahakamani badala ajibu hoja na kujisafisha je siku akiwa Rais ataweza kuvumilia maneno? Au ndo atapeleka kila mwananchi mahakamani na ikiwezekana kuwa mtekaji pia
inafikirisha🤔
 
Ni jambo jema ili mambo haya yawekwe sawa kwenye vyombo vya kisheria. Lakini, kwanini barua imesainiwa na Wakili mmoja ikiwa mwanzoni inawatambulisha Mawakili wengi na kuonyesha kuwa barua hiyo inaandikwa na hao wote? Just curious...
 
KALIA LIA... Au mpaka uone machozi yamelowanisha shati lote?

Kwamba?

IMG_20240906_122236.jpg


IMG_20240906_122258.jpg


Mpaka hapo mbona ngoma inogile?

imhotep au nasema uongo ndugu yangu?
 
Ni jambo jema ili mambo haya yawekwe sawa kwenye vyombo vya kisheria. Lakini, kwanini barua imesainiwa na Wakili mmoja ikiwa mwanzoni inawatambulisha Mawakili wengi na kuonyesha kuwa barua hiyo inaandikwa na hao wote? Just curious...
Wewe si "learned brother" mwenzao, unataka kusema hao jamaa wamekosea? Nadhani "Entity" hapo ni hao Matwiga Law Chambers. Au siyo wakili msomi!!

Nadhani wanamaanisha kuwa yeyote kati ya hao ataweza kusimama mahakamani. Mtazamo wako wa kisheria katika hili ukoje?
 
Huwa najiuliza hawa watu hawawezi kuhama kimya kimya na wakatulia kama alivyo fanya marehemu mzee Lowasa ? Au uchanga wa siasa nalo ni tatizo
Nakumbuka hata Kitila Mkumbo na Zitto wakati wanatoka CHADEMA hawakuwahi kutoa shombo kama hizi za Msigwa.

Nadhani walijua kwamba Kwenye Siasa unaweza ukahama CCM na kwenda CHADEMA na wakati mwingine ukarudi CCM pia.

Hopefully Mchungaji Msigwa hajajua namna ya kufanya Siasa zake
 
Hopefully Mchungaji Msigwa hajajua namna ya kufanya Siasa zake
Kinachomponza ni kwamba anamtumikia kafiri apate mradi wake, wakati huo huo CCM nao wanafunika kombe mwanaharamu apite.

Siyo kwamba hajui namna ya kufanya siasa zake, bali amesetiwa kama roboti. Anafanya wanachotaka kina Makalla.
 
Back
Top Bottom