Pre GE2025 Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
JPM alikuwa hataki mtu amkosoe, ukimkosoa tu, uko polisi kisha mahakamani kqa kesi ya jinai. Mbowe yeye hana mapolisi wa kumkamata na kumfungulia jinai Msigwa, ila ametumia njia ya madai kumziba mchungaji Msigwa ambaye anayajua ya ndani na uvunguni mwa Chadema
Hunaga jema na chadema 😂 nikama vile maadui wetu tulio aminishwa tangu uhuru ambao ni UJINGA, UMASKINI, MARADHI wewe umeongezea na CHADEMA 😂
 
JPM alikuwa hataki mtu amkosoe, ukimkosoa tu, uko polisi kisha mahakamani kqa kesi ya jinai. Mbowe yeye hana mapolisi wa kumkamata na kumfungulia jinai Msigwa, ila ametumia njia ya madai kumziba mchungaji Msigwa ambaye anayajua ya ndani na uvunguni mwa Chadema
Think tank ya chama chawala iko hoi bin taaban
 
Lissu anajua mengi kuliko hata huyo msigwa, na alianza kukemea hayo mambo kabla hata msigwa hajahamia mbogamboga.
Alikemea kuwa Mbowe anachukua hela za CHADEMA? Au hata tunachojadili hukijui?
Kuuliza Abduli ni nani ni kupoteza muda
Kwa nini ni kupoteza muda. Yaani unabagua wa kushughulika naye!! Sheria ya nchi hii mtoa na mpokea rushwa wote ni sawa. Abdul ni nani?
 
Msigwa siyo mwanasiasa ndio sababu aligomea Uteuzi Kwa Shujaa Magufuli

Wasomi kama Prof Kitila na Protabas Katambi na yule Kafulila aka Tumbiri ndio Injini ya Serikali ya CCM Kwa sasa Awamu hii ya 6 😂😂😂
 
Alikemea kuwa Mbowe anachukua hela za CHADEMA? Au hata tunachojadili hukijui?

Kwa nini ni kupoteza muda. Yaani unabagua wa kushughulika naye!! Sheria ya nchi hii mtoa na mpokea rushwa wote ni sawa. Abdul ni nani?
Alikemea matumizi mabaya ya mali za chama, na chama kipo chini ya mwenyekiti.

Ukitaka kumjua Abdul ni nani rudia kusikiliza maneno ya Lissu utajua vizuri.
 
anaushahidi ,siasa haifanywi kwa kumtukana mtu binafsi
kama ni deformations Mbowe mwenyewe ndio alipaswa kupelekwa mahakamani KWA kuwahadaa wananchi na ndugu waliopotelewa na jamaa zao kwamba yeye anajua walipo na mpaka leo hajawaonyesha ndugu zao, akaishia kusingizia polisi na serikali dah...

Baada ya ile kiki kubumba ndio kaibuka na hili ambalo credit zote zinamuendea Tundu Antipas Lisu 🐒
 
Lissu anajua mengi kuliko hata huyo msigwa, na alianza kukemea hayo mambo kabla hata msigwa hajahamia mbogamboga.
Lisu alikemea rushwa kwenye uchaguzi baada ya kupewa taarifa na abdul, siyo kwa vile alikuwa nalo rohoni siku nyingi, by necessary deduction!
 
1 Kwamba anaiba pesa za chama kwa kutumia Mbowe Foundation
2. Amegeuza chama kuwa SACCOS yake
3. Chadema digital inamilikiwa na Mbowe kwa manufaa yake

My take: hilo nililitegemea and that is the right way to go!

=====

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa, kuomba radhi, asipfanya hivyo ajiandae kulipa kulipa fidia ya shilingi bilioni 5 Mahakamani kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake kutokana na matamshi ya Msigwa yaliyotolewa hadharani baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika barua (notisi ya madai) iliyotolewa Septemba 2, 2024 ikiwa na sahihi ya tarehe 4 Septemba, 2024, mawakili wa Mbowe ambao ni Hekima Mwasipu na wenzake kutoka Matwiga Law Chambers, Msigwa anadaiwa kutoa matamshi ya uongo na kumchafua Mbowe mbele ya umma.

“Msigwa alitumia majukwaa ya mikutano, vyombo vya habari, na hata mitandao ya kijamii kutoa madai ya kumkashifu mteja wetu,” ameleza Wakili Mwasipu.

Imeelezwa kuwa Msigwa alidai kuwa Mbowe ameanzisha "Mbowe Foundation," na anatumia chama cha CHADEMA kwa manufaa yake binafsi. Katika moja ya mikutano yake, Msigwa alinukuliwa akisema, "Mwenyekiti wa CHADEMA amegeuza chama kuwa SACCOS, fedha za chama zinaishia kwenye taasisi binafsi na si kwenye akaunti za chama.”

Mawakili wa Mbowe wameeleza kuwa matamshi hayo yameathiri sifa ya Mbowe ndani na nje ya Tanzania, hasa kutokana na nafasi zake mbalimbali kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia vya Afrika (DUA).

“Mteja wetu anaona maneno yote yanayozungumzwa na kunukuliwa hapo juu katika maana yake ya asili, muktadha na misemo kuwa ni kashfa, dharau na kudhuru sio tu sifa yake binafsi bali pia kwa familia yake yote, marafiki, taaluma (Siasa), Jumuiya ya Biashara, Jumuiya ya Kidini, marafiki na rika. Maneno haya si chochote lakini ushahidi dhahiri wa nia mbaya dhidi ya mteja wetu”, imeelezwa na mawakili.

Mbali na hilo, Msigwa alidai kuwa CHADEMA Digital ambayo ni huduma ya usajili wa wanachama, inamilikiwa na kampuni binafsi na kwamba Mbowe anatumia fedha za chama kwa manufaa binafsi.

“Hali hii imeleta hasara kubwa kwa mteja wetu kwani sifa yake ya kiongozi wa kisiasa, mfanyabiashara na mwanafamilia imeathirika sana,” alisema Mwasipu.

Kwa mujibu wa notisi hiyo, Msigwa anatakiwa kuomba radhi kupitia machapisho katika magazeti mawili; moja lenye kuweza kufikia nchi nzima na lingine ambalo linaweza kuwafikia watu walau wa kanda, na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5, la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Pia soma
View attachment 3088571View attachment 3088572View attachment 3088573View attachment 3088574View attachment 3088575View attachment 3088576View attachment 3088577
Misigwa ameandika kwenye mtandao wa X kwa kudondoa huo wito kwamba 'political issues need political solutions'. Sijui ana maana gani kwa kuandika hivyo.
 
Kumbuka Lissu alisema alishangaa kuona chama kinasema hakuna pesa za mikutano, hata ile mikutano yake tuliona akipanda kwenye majukwaa ya miti na mbao.
 
Kumsema mbowe hadharani ni sawa na kuisema CHADEMA hadharani, hoja za msigwa zijibiwe kwa hoja na sio kuendekeza ushabiki wa hisia za kisiasa.
Kumsema mbowe hadharani kwa hoja za uongo kwa mtu mwenye acces yajukwaa lakuongea lolote unataka na mbowe naye afanye hivyo.Uko kutakua kupoteza muda.nchi bado ina changamoto nyingi za wananchi zakuzisemea kuliko kusikiliza porojo za majukwaani zakusemana ambazo badae watatuambia ilikua siasa.naona mbowe kaamua kua smart.siasa zilenge mahitaji ya wananchi sio mambo ya kijinga yasiyo na ukweli.ndo maana kaamua kujitofautisha na mpiga porojo.mwisho tutajua mbivu na mbichi.
 
Sasa mwanaccm atishike na kuburuzwa mahakamani na Mpinzani ilhali anao ushahidi?

Sasa wewe waona huyu katishika?

IMG_20240906_122258.jpg

Hapo si unaweka kambi kuufaudu mpambano?
 
Kesi za kisiasa hizo zitaisha kisiasa. Msigwa aendelee kupiga spana huyo Mbowe.
Unamponza mwenzio, kesi za kisiasa sio hizi kusingiziana uongo na kashfa, hizi ni defamation per se na Msigwa atajuta maana ndio ataijua ccm.
Pamoja na mengi aliyokuwa anasema majukwaani alikuwa anaandikiwa na Makalla ila sasa hata muona tena
 
Yale yale kama ya kinana na Msigwa hadi akaomba poo... ndilo linaloenda kutokea... Msigwa fanya uungwana mapema kabla mambo hayajawa mambo... kuomba msamaha nayo ni heri, sijui kama unazo hizo billion tano, labda kama mpango ni kukufilisi hadi nyumba....
Kwanini unataka aombe msamaha wakati hujui hayo madai yake kama yana ukweli
 
Kumsema mbowe hadharani kwa hoja za uongo kwa mtu mwenye acces yajukwaa lakuongea lolote unataka na mbowe naye afanye hivyo.Uko kutakua kupoteza muda.nchi bado ina changamoto nyingi za wananchi zakuzisemea kuliko kusikiliza porojo za majukwaani zakusemana ambazo badae watatuambia ilikua siasa.naona mbowe kaamua kua smart.siasa zilenge mahitaji ya wananchi sio mambo ya kijinga yasiyo na ukweli.ndo maana kaamua kujitofautisha na mpiga porojo.mwisho tutajua mbivu na mbichi.
Mtu respectable kama Mbowe hawezi kujibizana na Msugwa kwenye majukwaa, that will be below his diginity!
 
Misigwa ameandika kwenye mtandao wa X kwa kudondoa huo wito kwamba 'political issues need political solutions'. Sijui ana maana gani kwa kuandika hivyo.
THIS IS NOT POLITICAL, IT IS DEFERMATION PER SE! useme kwenye jukwa kuwa Mbowe ni mwizi, anakwiba hela za Chadema, anakula rushwa halafu useme hiyo ni political, not at all!
 
1 Kwamba anaiba pesa za chama kwa kutumia Mbowe Foundation
2. Amegeuza chama kuwa SACCOS yake
3. Chadema digital inamilikiwa na Mbowe kwa manufaa yake

My take: hilo nililitegemea and that is the right way to go!

=====

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa, kuomba radhi, asipfanya hivyo ajiandae kulipa kulipa fidia ya shilingi bilioni 5 Mahakamani kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake kutokana na matamshi ya Msigwa yaliyotolewa hadharani baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika barua (notisi ya madai) iliyotolewa Septemba 2, 2024 ikiwa na sahihi ya tarehe 4 Septemba, 2024, mawakili wa Mbowe ambao ni Hekima Mwasipu na wenzake kutoka Matwiga Law Chambers, Msigwa anadaiwa kutoa matamshi ya uongo na kumchafua Mbowe mbele ya umma.

“Msigwa alitumia majukwaa ya mikutano, vyombo vya habari, na hata mitandao ya kijamii kutoa madai ya kumkashifu mteja wetu,” ameleza Wakili Mwasipu.

Imeelezwa kuwa Msigwa alidai kuwa Mbowe ameanzisha "Mbowe Foundation," na anatumia chama cha CHADEMA kwa manufaa yake binafsi. Katika moja ya mikutano yake, Msigwa alinukuliwa akisema, "Mwenyekiti wa CHADEMA amegeuza chama kuwa SACCOS, fedha za chama zinaishia kwenye taasisi binafsi na si kwenye akaunti za chama.”

Mawakili wa Mbowe wameeleza kuwa matamshi hayo yameathiri sifa ya Mbowe ndani na nje ya Tanzania, hasa kutokana na nafasi zake mbalimbali kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia vya Afrika (DUA).

“Mteja wetu anaona maneno yote yanayozungumzwa na kunukuliwa hapo juu katika maana yake ya asili, muktadha na misemo kuwa ni kashfa, dharau na kudhuru sio tu sifa yake binafsi bali pia kwa familia yake yote, marafiki, taaluma (Siasa), Jumuiya ya Biashara, Jumuiya ya Kidini, marafiki na rika. Maneno haya si chochote lakini ushahidi dhahiri wa nia mbaya dhidi ya mteja wetu”, imeelezwa na mawakili.

Mbali na hilo, Msigwa alidai kuwa CHADEMA Digital ambayo ni huduma ya usajili wa wanachama, inamilikiwa na kampuni binafsi na kwamba Mbowe anatumia fedha za chama kwa manufaa binafsi.

“Hali hii imeleta hasara kubwa kwa mteja wetu kwani sifa yake ya kiongozi wa kisiasa, mfanyabiashara na mwanafamilia imeathirika sana,” alisema Mwasipu.

Kwa mujibu wa notisi hiyo, Msigwa anatakiwa kuomba radhi kupitia machapisho katika magazeti mawili; moja lenye kuweza kufikia nchi nzima na lingine ambalo linaweza kuwafikia watu walau wa kanda, na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5, la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Pia soma
View attachment 3088571View attachment 3088572View attachment 3088573View attachment 3088574View attachment 3088575View attachment 3088576View attachment 3088577
Sikuwahi kujua ya kwamba watu huwa wanaumia wakituhumiwa mitandaoni!
 
Back
Top Bottom