Pre GE2025 Freeman Mbowe amtaka Mchungaji Peter Msigwa kumuomba radhi kwenye Magazeti na kulipa fidia ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumkashifu na kumchafua jina

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwanini unataka aombe msamaha wakati hujui hayo madai yake kama yana ukweli
Yana ukweli gani? Au labda alinyofoa nyaraka za kiofisi ambalo ni kosa lingine pia…haya mambo ya kupayuka payuka sio poa, ilikuwa Hivyo Kwa Kinana mwishowe Aibu…
 
1 Kwamba anaiba pesa za chama kwa kutumia Mbowe Foundation
2. Amegeuza chama kuwa SACCOS yake
3. Chadema digital inamilikiwa na Mbowe kwa manufaa yake

My take: hilo nililitegemea and that is the right way to go!

=====

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa, kuomba radhi, asipfanya hivyo ajiandae kulipa kulipa fidia ya shilingi bilioni 5 Mahakamani kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake kutokana na matamshi ya Msigwa yaliyotolewa hadharani baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika barua (notisi ya madai) iliyotolewa Septemba 2, 2024 ikiwa na sahihi ya tarehe 4 Septemba, 2024, mawakili wa Mbowe ambao ni Hekima Mwasipu na wenzake kutoka Matwiga Law Chambers, Msigwa anadaiwa kutoa matamshi ya uongo na kumchafua Mbowe mbele ya umma.

“Msigwa alitumia majukwaa ya mikutano, vyombo vya habari, na hata mitandao ya kijamii kutoa madai ya kumkashifu mteja wetu,” ameleza Wakili Mwasipu.

Imeelezwa kuwa Msigwa alidai kuwa Mbowe ameanzisha "Mbowe Foundation," na anatumia chama cha CHADEMA kwa manufaa yake binafsi. Katika moja ya mikutano yake, Msigwa alinukuliwa akisema, "Mwenyekiti wa CHADEMA amegeuza chama kuwa SACCOS, fedha za chama zinaishia kwenye taasisi binafsi na si kwenye akaunti za chama.”

Mawakili wa Mbowe wameeleza kuwa matamshi hayo yameathiri sifa ya Mbowe ndani na nje ya Tanzania, hasa kutokana na nafasi zake mbalimbali kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia vya Afrika (DUA).

“Mteja wetu anaona maneno yote yanayozungumzwa na kunukuliwa hapo juu katika maana yake ya asili, muktadha na misemo kuwa ni kashfa, dharau na kudhuru sio tu sifa yake binafsi bali pia kwa familia yake yote, marafiki, taaluma (Siasa), Jumuiya ya Biashara, Jumuiya ya Kidini, marafiki na rika. Maneno haya si chochote lakini ushahidi dhahiri wa nia mbaya dhidi ya mteja wetu”, imeelezwa na mawakili.

Mbali na hilo, Msigwa alidai kuwa CHADEMA Digital ambayo ni huduma ya usajili wa wanachama, inamilikiwa na kampuni binafsi na kwamba Mbowe anatumia fedha za chama kwa manufaa binafsi.

“Hali hii imeleta hasara kubwa kwa mteja wetu kwani sifa yake ya kiongozi wa kisiasa, mfanyabiashara na mwanafamilia imeathirika sana,” alisema Mwasipu.

Kwa mujibu wa notisi hiyo, Msigwa anatakiwa kuomba radhi kupitia machapisho katika magazeti mawili; moja lenye kuweza kufikia nchi nzima na lingine ambalo linaweza kuwafikia watu walau wa kanda, na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5, la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Pia soma
View attachment 3088571View attachment 3088572View attachment 3088573View attachment 3088574View attachment 3088575View attachment 3088576View attachment 3088577

Tatizo la uchawa ni kuropoka ropoka sasa kashikwa pabaya alete ushahidi wa wazi, aombe radhi au alipe hii ni loose, loose situation
 
Msigwa kesi hii itamlamba (vijana wa mjini wanasema) , atashindwa kwa sababu report za CAG ziaonesha financial management ya chadema haina shida ndiyo maana wanapata hati safi!
Kweli CAG akute hela za Join the chain zinakwenda Kenya atoe hati safi?
 
Mahakamani sio sehemu sahihi ya kujibu hizo hoja, Mnyika na ofisi yake ndyo wanapaswa kujibu hoja za msigwa na hoja za Lissu.
Msigwa anadata akajibu mahakamani ,ccm waliogopa kumpeleka LISu mahakamani enzi za lowasa alipotamkwa mana walikuwa na ushahidi kwasasa msigwa nae akajibu akamwage ugali mahakamani
 
mambo ya aibu kabisa. Msigwa amemuandama Mboe sana. kwa hilo namuunga mkono Mbowe.
Kati ya wachungaji wa hovyo ni huyo jamaa. Dini zote zinafundisha kutosingizia,kutosema uongo,kuheshimu wenzako nk. Hilo kwake halipo.
 
kama ni deformations Mbowe mwenyewe ndio alipaswa kupelekwa mahakamani KWA kuwahadaa wananchi na ndugu waliopotelewa na jamaa zao kwamba yeye anajua walipo na mpaka leo hajawaonyesha ndugu zao, akaishia kusingizia polisi na serikali dah...

Baada ya ile kiki kubumba ndio kaibuka na hili ambalo credit zote zinamuendea Tundu Antipas Lisu 🐒
Hata wewe mpeleke silazima iwe polisi peleka kwaniaba ya jeshi la polisi
 
Msigwa anadata akajibu mahakamani ,ccm waliogopa kumpeleka LISu mahakamani enzi za lowasa alipotamkwa mana walikuwa na ushahidi kwasasa msigwa nae akajibu akamwage ugali mahakamani
Akiweza kuwasilisha ushahidi mahakamani basi hata wanachama wa CHADEMA watapata mwanga kuhusu hali halisi ya mambo ambayo yanahitaji ufafanuzi wa kina.
 
1 Kwamba anaiba pesa za chama kwa kutumia Mbowe Foundation
2. Amegeuza chama kuwa SACCOS yake
3. Chadema digital inamilikiwa na Mbowe kwa manufaa yake

My take: hilo nililitegemea and that is the right way to go!

=====

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa, kuomba radhi, asipfanya hivyo ajiandae kulipa kulipa fidia ya shilingi bilioni 5 Mahakamani kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake kutokana na matamshi ya Msigwa yaliyotolewa hadharani baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika barua (notisi ya madai) iliyotolewa Septemba 2, 2024 ikiwa na sahihi ya tarehe 4 Septemba, 2024, mawakili wa Mbowe ambao ni Hekima Mwasipu na wenzake kutoka Matwiga Law Chambers, Msigwa anadaiwa kutoa matamshi ya uongo na kumchafua Mbowe mbele ya umma.

“Msigwa alitumia majukwaa ya mikutano, vyombo vya habari, na hata mitandao ya kijamii kutoa madai ya kumkashifu mteja wetu,” ameleza Wakili Mwasipu.

Imeelezwa kuwa Msigwa alidai kuwa Mbowe ameanzisha "Mbowe Foundation," na anatumia chama cha CHADEMA kwa manufaa yake binafsi. Katika moja ya mikutano yake, Msigwa alinukuliwa akisema, "Mwenyekiti wa CHADEMA amegeuza chama kuwa SACCOS, fedha za chama zinaishia kwenye taasisi binafsi na si kwenye akaunti za chama.”

Mawakili wa Mbowe wameeleza kuwa matamshi hayo yameathiri sifa ya Mbowe ndani na nje ya Tanzania, hasa kutokana na nafasi zake mbalimbali kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia vya Afrika (DUA).

“Mteja wetu anaona maneno yote yanayozungumzwa na kunukuliwa hapo juu katika maana yake ya asili, muktadha na misemo kuwa ni kashfa, dharau na kudhuru sio tu sifa yake binafsi bali pia kwa familia yake yote, marafiki, taaluma (Siasa), Jumuiya ya Biashara, Jumuiya ya Kidini, marafiki na rika. Maneno haya si chochote lakini ushahidi dhahiri wa nia mbaya dhidi ya mteja wetu”, imeelezwa na mawakili.

Mbali na hilo, Msigwa alidai kuwa CHADEMA Digital ambayo ni huduma ya usajili wa wanachama, inamilikiwa na kampuni binafsi na kwamba Mbowe anatumia fedha za chama kwa manufaa binafsi.

“Hali hii imeleta hasara kubwa kwa mteja wetu kwani sifa yake ya kiongozi wa kisiasa, mfanyabiashara na mwanafamilia imeathirika sana,” alisema Mwasipu.

Kwa mujibu wa notisi hiyo, Msigwa anatakiwa kuomba radhi kupitia machapisho katika magazeti mawili; moja lenye kuweza kufikia nchi nzima na lingine ambalo linaweza kuwafikia watu walau wa kanda, na kulipa fidia ya Shilingi bilioni 5, la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Pia soma
View attachment 3088571View attachment 3088572View attachment 3088573View attachment 3088574View attachment 3088575View attachment 3088576View attachment 3088577
Hivi Mbowe anaposema anataka alipwe billion tano anamaanisha au ndio ile kauli kuwa mwansiasa akiuambia ni saa mbili usiku toka nje ukathibishe. Anyway wacha Waarabu wa Pemba wapambane wenyewe. Kwa sababu wanajuana kwa vilemba
 
Msigwa ana historia ya kuropoka hovyo kisha akishitakiwa kwa defamation anakosa Cha kulipa.

Aliwahi kumdhalilisha Kinana kwa uongo mahakamani akashindwa ikabidi atoke hadharani kumuomba msamaha Mzee Kinana.
 
Angalia akina Kafulila wametulia kabisa!
Hizo ni kazi kama kazi zingine ilimradi wote tunaenda chooni.kuanzia mfagiaji hadi mkurugenzi.jambo la msingi ni je umetumiaje nafasi uliyokua nayo kuwasaidia wanyonge na maskini wa nchi yako.ila kwakua wewe unawaza ubinafsi basi unaona huo ubunge au U dc ni bonge ya dili.
 
Huyo ndio dawa yake! Atafunga mdomo wake Kama musiba. Udc autafutwi kwa kumtukana Mbowe
 
Back
Top Bottom