SI KWELI Freeman Mbowe asitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23

SI KWELI Freeman Mbowe asitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Mbowe maandamano.png

Nimeona video ikizunguka kwenye mitandao ya Kijamii ikonesha kuwa jioni ya leo, mwenyekiti wa CHADEMA amesitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23


 
Tunachokijua
Freeman Mbowe ni ni mwanasiasa maarufu nchini Tanzania. Yeye ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu Ally Mohamed Kibao kilichotokea Septemba 8, 2024, chama cha CHADEMA kiliweka azma ya kufanya maandamano Septemba 23, 2024 kupinga utekaji na mauaji yanayoendelea nchini (Soma Hapa). Baada ya azma hiyo tukio siku ya September 13, 2024 Jeshi la Polisi lilifanya Mkutano na Waandishi wa Habari kukikataza chama hicho kufanya maandamano hayo (Soma hapa).

Kama alivyodokeza mdau mleta mada hii leo kupitia mtandao wa X (Twitter) katika akaunti hii na hii kumechapishwa taarifa iliyoambatana na video ikimuoonesha Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akitangaza uamuzi wa chama hicho kusitisha mpango wa Maandamano ili kutoa nafasi ya Viongozi wa dini kutafuta suluhu. Katika video hiyo yenye sekunde 33 Freeman Mbowe anaonekana akisema:

Tunaomba na kuwatangazia Viongozi wa ngazi zote za CHADEMA pamoja na Wanachama, Wabunge wakiwemo, Madiwani, Wafuasi na Mashabiki wetu Watanzania wote popote pale walipo, kwamba tunaahirisha mikutano na maandamano ya amani yaliyopanga kufanyika nchi nzima ili kutoa nafasi kwa viongozi wetu wa kiroho kutafuta suluhu ya jambo hili kwa kukutana na rais na serikali yake
Upi ukweli wa Video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao wa JamiiCheck kupitia mtandao wa YouTube kwa kutumia maneno CHADEMA yasitisha Maandamano tumepata majibu kuwa video hii si ya mwaka huu wala haihusiani na mpango wa Maandamano ya CHADEMA ya mwaka huu. Video hii ilichapishwa kwenye mtandao huo mara ya kwanza Agosti 31, mwaka 2016 (tazama hapa na hapa) huku ikieleza uamuzi wa CHADEMA kusitisha kwa mwezi mmoja maandamano ya UKUTA waliyoyapanga kuyafanya Septemba 1, 2016.
Maandamano waachieni jirani zetu akina Njoroge, huku kwetu tukijitahidi Sana ni Simba na Yangu baasi!
 
Ulitarajia ufurahi watu wakiumizwa sasa utaumizwa na Mpango wa Kamanda wa Anga Mbowe.

Tumewajua nyote nyoyo zenu na mwemyekiti wenu Easily provoked and exposed every evil around. Hii nayo ni intelijensia makini.
Unasweat hagga😂😂😂
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ametangaza kuahirisha maandamano yaliyopangwa kuanza tarehe 23/9/2024 mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa TDC ili kupisha mazungumzo yatakayofanyika baina ya viongozi wa dini na Rais Samia.
Ni uamuzi wa busara, apewe maua yake.
 
Nchi unaiharibu mwenyewe samia.
Unawalea sana polisi wako.
Kulikuwa na umuhimu gani wa kumuua kibao?
mnakosea mkisema ivyo marangapi watu fake wanakuja madukani na kujifanya TRA kuchukua ushuru je hawa nao wanatumwa na Samia? mara ngapi muhimbili wanakamatwa watu fake wanaojifanya madr na kuchukua pesa kwa wagonjwa je hawa nao wanatumwa na Samia? muhimu Rais aharakishe uchunguzi na wambain muuaji huwezi kusema moja kwa moja ni fulani
 
Askari karibu alfu na kidogo kutoka mikoani wamewasili dar kungojea maandamano .
Mboe kapiga zuga kwel.
 
Nani amfunge paka kengele?
Siku hizi kuna technolojia , Panya hawahitajiki tena kumfunga Paka Kengele ili kujua movements zake, siku hizi wanafunga tu CCT Camera bila ya kuhitaji kumgusa Mr Paka, na lengo linakuwa limetimia wanabakia salama hao Panya wakimchekeal kutokea shimoni mwao.
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ametangaza kuahirisha maandamano yaliyopangwa kuanza tarehe 23/9/2024 mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa TDC ili kupisha mazungumzo yatakayofanyika baina ya viongozi wa dini na Rais Samia.
Viongozi wa dini watulie madhabahuni na majoho yao
 
Kwake kwa lile tamko lao la awali lilisaidia kuamsha mpaka nyoka toka pangoni. So kwa upande wake na chama chao nadhani lengo limefanikiwa kupaaza suati na kuwatoa nyoka pangoni . Kelele na misimamo yao kuhusu jambo walilokuwa wanalipigia kele at least limesikika kwa sauti kubwa na kuenea kwamba kweli kuna tatizo ambalo linahitaji kuwa addressed kwa maslahi na mustakabali mzuri wa Taifa. Siyo kunyamaza na kufumbia macho as if every thing is normal. Kwa hatua hiyo at least lengo limefanikiwa ngoja atoe fursa kwa wahusika kulishughulikia pasipokuwa na kisingizio cha uvurugaji wa amani. Ache Vyombo husika sasa vielekeze nguvu na nyenzo zote kwenye kutafuta chanzo cha tatizo na kuwachukulia hatua wahusika wa huo mchezo mchafu ambao umelichafua Taifa letu mbele ya macho ya dunia. Na sauti za nje nazo zimefikisha ujumbe mzito na hakuna wa kupinga mchango wao .
Na hata hayo maridhiano yenyewe Chadema inaenda kupigwa za uso
 
Back
Top Bottom