SI KWELI Freeman Mbowe asitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23

SI KWELI Freeman Mbowe asitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Mbowe maandamano.png

Nimeona video ikizunguka kwenye mitandao ya Kijamii ikonesha kuwa jioni ya leo, mwenyekiti wa CHADEMA amesitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23


 
Tunachokijua
Freeman Mbowe ni ni mwanasiasa maarufu nchini Tanzania. Yeye ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu Ally Mohamed Kibao kilichotokea Septemba 8, 2024, chama cha CHADEMA kiliweka azma ya kufanya maandamano Septemba 23, 2024 kupinga utekaji na mauaji yanayoendelea nchini (Soma Hapa). Baada ya azma hiyo tukio siku ya September 13, 2024 Jeshi la Polisi lilifanya Mkutano na Waandishi wa Habari kukikataza chama hicho kufanya maandamano hayo (Soma hapa).

Kama alivyodokeza mdau mleta mada hii leo kupitia mtandao wa X (Twitter) katika akaunti hii na hii kumechapishwa taarifa iliyoambatana na video ikimuoonesha Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akitangaza uamuzi wa chama hicho kusitisha mpango wa Maandamano ili kutoa nafasi ya Viongozi wa dini kutafuta suluhu. Katika video hiyo yenye sekunde 33 Freeman Mbowe anaonekana akisema:

Tunaomba na kuwatangazia Viongozi wa ngazi zote za CHADEMA pamoja na Wanachama, Wabunge wakiwemo, Madiwani, Wafuasi na Mashabiki wetu Watanzania wote popote pale walipo, kwamba tunaahirisha mikutano na maandamano ya amani yaliyopanga kufanyika nchi nzima ili kutoa nafasi kwa viongozi wetu wa kiroho kutafuta suluhu ya jambo hili kwa kukutana na rais na serikali yake
Upi ukweli wa Video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao wa JamiiCheck kupitia mtandao wa YouTube kwa kutumia maneno CHADEMA yasitisha Maandamano tumepata majibu kuwa video hii si ya mwaka huu wala haihusiani na mpango wa Maandamano ya CHADEMA ya mwaka huu. Video hii ilichapishwa kwenye mtandao huo mara ya kwanza Agosti 31, mwaka 2016 (tazama hapa na hapa) huku ikieleza uamuzi wa CHADEMA kusitisha kwa mwezi mmoja maandamano ya UKUTA waliyoyapanga kuyafanya Septemba 1, 2016.
Issue sio maandamano, kinachoendelea nchini Bora maandamano yangekuwepo,ili ujue watu wanaongea nini.
nadhani kiongozi makini mwenye maono, ikitokea changamoto anaketi chini kutafakari kudeal na kutafuta majawabu muafaka ya kutatua changamoto husika, na sio kuzidisha na kuchochea changamoto zaidi ambazo ni useless zaidi, kwamfano akafa mtu kwenye maandamano haramu ya samia must go?

si kamanda Ally Mohamed Kibao atasahaulika kabisa kama aliwahi kuuawa kikatili?🐒
 
hebu eleza vizuri gentleman kwa faida ya wadau 🐒

hayo maandamano haramu yaliyopigwa marufuku,

ni kwajili ya kuleta fujo, maafa na kuharibu demokrasia na Samia Must Go?

au ni hiyo ingine ya mwanzo umetaja?🐒
Unatetea ugali wako 😆😆 time will tell
 
Ubalozi wa Germany, waichunguze hii radio ya . Kuna mamluki wa uvccm
 
Watanganyika,tunachofanyiwa na yule bibi ni sawa na kile kilichofanywa na waliotumwa na afande ,huku Dodoma.
 

Nimeona video ikizunguka kwenye mitandao ya Kijamii ikonesha kuwa jioni ya leo, mwenyekiti wa CHADEMA amesitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23


Chadema hawajawahipo kuandamana, tanganyika bado sana, mbowe ni coward sana, tundulisu aliwahi kutanganza maandamo baada ule uchaguzi walioibiwa siku iliyofuata ata yeye hakutoka, siku ya pili akakimbilia belgium
 
Aisee.

Mimi sio shabiki wa mambo ya kisiasa ila Mbowe ni mtu mmoja mstaarabu sana na muungwana sana,ni msikivu na mvumilivu,

Big up sana kwake.
Mbowe uliyekuwa unamjuwa ww sasaiv siye tena, hatoki ikulu na makoti yake nilijua tu watauchomoa, kwa sasaivi hasa kumjua nani ni chadema utapata tabu sana viongozi wote wanatumiliwa na kuendeshwa kama remote.
 
Back
Top Bottom