SI KWELI Freeman Mbowe asitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23

SI KWELI Freeman Mbowe asitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Mbowe maandamano.png

Nimeona video ikizunguka kwenye mitandao ya Kijamii ikonesha kuwa jioni ya leo, mwenyekiti wa CHADEMA amesitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23


 
Tunachokijua
Freeman Mbowe ni ni mwanasiasa maarufu nchini Tanzania. Yeye ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu Ally Mohamed Kibao kilichotokea Septemba 8, 2024, chama cha CHADEMA kiliweka azma ya kufanya maandamano Septemba 23, 2024 kupinga utekaji na mauaji yanayoendelea nchini (Soma Hapa). Baada ya azma hiyo tukio siku ya September 13, 2024 Jeshi la Polisi lilifanya Mkutano na Waandishi wa Habari kukikataza chama hicho kufanya maandamano hayo (Soma hapa).

Kama alivyodokeza mdau mleta mada hii leo kupitia mtandao wa X (Twitter) katika akaunti hii na hii kumechapishwa taarifa iliyoambatana na video ikimuoonesha Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akitangaza uamuzi wa chama hicho kusitisha mpango wa Maandamano ili kutoa nafasi ya Viongozi wa dini kutafuta suluhu. Katika video hiyo yenye sekunde 33 Freeman Mbowe anaonekana akisema:

Tunaomba na kuwatangazia Viongozi wa ngazi zote za CHADEMA pamoja na Wanachama, Wabunge wakiwemo, Madiwani, Wafuasi na Mashabiki wetu Watanzania wote popote pale walipo, kwamba tunaahirisha mikutano na maandamano ya amani yaliyopanga kufanyika nchi nzima ili kutoa nafasi kwa viongozi wetu wa kiroho kutafuta suluhu ya jambo hili kwa kukutana na rais na serikali yake
Upi ukweli wa Video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao wa JamiiCheck kupitia mtandao wa YouTube kwa kutumia maneno CHADEMA yasitisha Maandamano tumepata majibu kuwa video hii si ya mwaka huu wala haihusiani na mpango wa Maandamano ya CHADEMA ya mwaka huu. Video hii ilichapishwa kwenye mtandao huo mara ya kwanza Agosti 31, mwaka 2016 (tazama hapa na hapa) huku ikieleza uamuzi wa CHADEMA kusitisha kwa mwezi mmoja maandamano ya UKUTA waliyoyapanga kuyafanya Septemba 1, 2016.
Maandamano yapo pale pale. Mashetani watekaji na wauaji mnahangaika sana, lakini hambadili chochote.
kwahiyo gentleman,
unampinga chairman wako Taifa,ambae ndie alietangaza kuwapo kwa maandamano hayo haramu ya Samia must go, na ndio huyo huyo alie yasitisha?🐒

Nasisitiza kwamba chadema kuona ombwe la uongozi. Kwasababu hakuna muunganiko baina ya wanachama, mashabiki na uongozi...

Mfano,
Mwenyekiti kasitisha maandamano hayo, mwanachama kaidi unakuja unasisitiza maandamano haramu yako pale pale 🤣

sasa nani ni nani hapo chadema?
 
OGOPA MATAPELI NA WAPOTOSHAJI MAANDAMANO YA AMANI KUDAI TAARIFA JUU YA WALIOPOTEA NA KUTEKWA YAPO PALEPALE.

NAOMBA TUZITUMIE HIZI SIKU MBILI ZILIZOBAKI KATIKA KUJIANDAA NA MLIO MBALI YA DAR ES SALAAM BASI MUWEZE KUSOGEA ILI IFIKAPO 23rd Sep 2024 TUWEZE KUTEKELEZA KILICHOPO MBELE YETU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU MBARIKI RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSANI! AMINA.
 
Ilikua ni suala la muda tu tangazo la sitisho la maandamano yaliyopigwa marufuku na polisi nchini kutolewa, hasa baada ya hotuba nzito na bora zaidi ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa Taifa, na jumuiya ya kimataifa,
Hii habari jf walikanusha. Tokea jana kwenye kile kitengochap cha kufuatilia oama ni za ukweli or lah.
 
Kwa hiyo uongozi wa CHADEMA ungekuwa bora, maandamano haramu yangefanyika, au sio?
kwanza,
yasingekuepo kabisa,

Lakini pili yasingekua ya kuvuruga Demokrasia mathalani kwa slogan kama Samia must go, halafu eti yakaitwa ni maandamano ya Amani..

Lakini tatu na muhimu zaidi yasingekuepo wakati huu na kwahivyo viongozi visionary politically, wangeketi chini pamoja, na kutafuta majawabu muafaka ya kutatua changamoto zilizoko,

na kisha baada ya kupata suluhu na majawabu muafaka yaliyofanyiwa kazi na kubaini ukweli..

ndipo sasa,
viongozi makini huandaa maandamano ya kupongeza juhudi za kupatikana ukweli, kuliunganisha taifa na kuiimarisha umoja, amani na utulivu wa wananchi 🐒
 
Hii habari jf walikanusha. Tokea jana kwenye kile kitengochap cha kufuatilia oama ni za ukweli or lah.
ni muhimu sana, na ni vizuri zaidi wakajiridhisha na kumtafuta chairman Mbowe ambae alisema vizuri sana kwamba wameamua kusitisha maandamano yao na kwahivyo hayatakuapo 🐒

au alikua anawafurahisha wanahabari na wajumbe wa TCD nje ya mikutano? na akaamua kunipotosha na mimi?🐒
 
Atoke tu hatufai.
kwa sisi wanadiplomasia waandamizi makini, tunasema na kushauri kwamba, kama kuna yeyote ambae haifai uongozini, basi aondolewe kwa njia za kidemokrasia katika sanduku la kura, lakini sio hiyo ya MBOWE MUST GO, hiyo ni fujo 🐒
 
OGOPA MATAPELI NA WAPOTOSHAJI MAANDAMANO YA AMANI KUDAI TAARIFA JUU YA WALIOPOTEA NA KUTEKWA YAPO PALEPALE.

NAOMBA TUZITUMIE HIZI SIKU MBILI ZILIZOBAKI KATIKA KUJIANDAA NA MLIO MBALI YA DAR ES SALAAM BASI MUWEZE KUSOGEA ILI IFIKAPO 23rd Sep 2024 TUWEZE KUTEKELEZA KILICHOPO MBELE YETU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU MBARIKI RAIS WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSANI! AMINA.
hebu eleza vizuri gentleman kwa faida ya wadau 🐒

hayo maandamano haramu yaliyopigwa marufuku,

ni kwajili ya kuleta fujo, maafa na kuharibu demokrasia na Samia Must Go?

au ni hiyo ingine ya mwanzo umetaja?🐒
 
Back
Top Bottom