Ndio nimejikita huko kuwa Mbowe na familia yake waache udhulumaji na unyonyaji.hivi kweli Mbowe na familia yake wanashindwa kuwa na huruma kwa watu waliokuwa wanaacha familia zao na kuwahi kufanya kazi kwa Mbowe? Kama anashindwa kuwatendea haki watu kumi tu ni vipi anajinasibu kuwatetea watanzania mamilioni kwa mamilioni? Kama siyo unafiki ni nini? Kama siyo utapeli wa kisiasa na maneno ni nini?
Mwenyekiti mzima anawadhulumu watu waliotoa jasho lao? Mwenyekiti mzima anayesema anapigania haki anashindwa kuguswa na maisha ya watu kumi tu? Huu ni uhuni usiokubalika hata kidogo kwa jamii iliyostaarabika. Hili tu lilikuwa linatosha kumfanya ajiuzulu hata huo uenyekiti wake anaoutumia kukinyonya chama kama kupe. Mbowe na familia yake ni wanafiki sana .asivyo na aibu wala haya anajifanya eti anawatetea Watanzania? Watanzania wapi hao anaowatetea wakati nyuma ya pazia anapora haki zao? Mnafiki mkubwa