Mkono wa Mungu wa hasira utakuwa juu yake. Dhuluma ni kama giza tu haliwezi kushindana na nuru. Dhuluma ambayo Mbowe na familia yake wamezoea kuwatendwa watu wanaofanya kazi kwake basi sasa ni mwisho . tutaendelea kupaza sauti juu ya udhulumaji wa Mbowe na familia yake anaowafanyia watu.nitapaza sauti bila kuchoka mpaka kila mtu ndani na nje ya nchi atambue kuwa familia ya Mbowe ni nukusi linapokuja suala la pesa. amekula Ruzuku za chama ameona hazitoshi,amekula michango ya join the chain ameona tumbo lake halitosheki ,amekula pesa za akina sabodo ameona hajashiba mpaka ale na kumeza za waandishi hawa wanyonge waliokuwa wanawahi kila siku asubuhi kumfanyia yeye kazi ,halafu mwisho wa siku anawadhulumu bila aibu wala haya.