Siyo Mbowe niliyesikia kuwa alishapata chanjo ya Covid? Sasa barakoa ya nini tena?
Sent from my 5033X_EEA using
JamiiForums mobile app
Kinga ya ziada.
Kuna baadhi ya waliopata chanjo ambao wamepata maambukizi, hata kama siyo wengi.
Kumbuka, ugonjwa huu bado mambo mengi hayajulikani, isitoshe, 'virus' anayesababisha ugonjwa ana uwezo wa kujibadilisha haraka.
Kwa hiyo, kama chanjo ilikuwa ni kwa aina fulani ya 'virus' huyo huyo miezi miwili iliyopita, na leo kawepo 'variant' aina nyingine ya virus huyo huyo, hakuna 'guarantee' ya kwamba huyo 'variant' mpya atakingwa na chanjo ile ile.
Kuvaa barakoa, na kufuata maelekezo mengine yanayotolewa kujikinga na maambukizi ni muhimu kwa yeyote yule.
Lakini, hata hivyo, nitumie mfano kueleza umuhimu wa chanjo: Ushahidi uliopo sasa hivi, chanjo zinafanya kazi ya kukinga maambukizi.
Maana yake ni kwamba, mtu aliyepata chanjo anayo nafasi kubwa zaidi ya kujikinga kuliko yule ambaye hana chanjo kabisa.