Freeman Mbowe elimu nzuri sio kuzungumza Kiingereza

Freeman Mbowe elimu nzuri sio kuzungumza Kiingereza

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mikutano imeruhusiwa na Mama lakini mchague kwa makini nini mtakwenda kuwaambia wananchi kwenye majukwaa ya kisiasa. Mbowe aliwaambia wananchi wanaomsikiliza kuwa Watanzania hawawezi kwenda kutafuta kazi nchi za nje zikiwemo Ulaya na Marekani kwakuwa hawajui kuongea Kiingereza kama ushahidi wa elimu yetu mbovu kuliko ya Kenya.

Wachina, Wasomali, Warundi, wWanyarwanda na Wahabeshi hawajui kuongea kiingereza lakini wametapakaa nchi nyingi za dunia. Wakenya hawajui kiswahili kizuri lakini wako wengi Tanzania kuliko watanzania walioko Kenya.

Hii ni kuonyesha kuwa kinachowapeleka wakenya wengi nchi za nje kuliko watanzania sio kujua kiingereza kuliko watanzania bali kuna sababu nyingine za maana kuliko kujua kuzungumza kiingereza. Na sababu hizo ni pamojana na hizi zifuatazo:

1. AMANI: Mtanzania anao uhakika wa kuiona kesho na kuwaona wajukuu zake kabla hajafa. Hii ni tofauti na mataifa mengine yanayotuzunguuka. Kila mtu anatamani kuja tz na sio kuondoka Tanzania.

2. ARDHI: Tanzania kuna ardhi kubwa ya bure kwa kila mtanzania inayomwezesha kulima, kufuga, kuvua, kujenga na kuchimba bila bughuza na kujipatia kipato. Kenya hakuna ardhi kwa watoto wao. Kenya ardhi kubwa iko mikononi mwa watu wachache na wazungu. Hapa tz mtaji wa kijana ni nguvu zake mwenyewe tu baasi.

3. UHOLELA: Tanzania kila kitu ni holela tu. Unalima, unafuga, unavua, unafanya biashara, unachimba na kujenga kiholela tu, hata kodi haikusanywi kivilee, watu hawana leseni za biashara wala za kuuza pombe, lakini wanauza tu popote. Hata leseni za udereva unapatiwa tu wakati wowote, magari mabovu yako barabarani na polisi ni washikaji tu mitaani. Hali kama hii huwezi kuipata popote pale ni tz tu. Kijana wa kitanzania hawezi kukubali kuachana na maisha kama haya aende akaparangane na maisha ya kitumwa na kimanamba huko ulaya na marekani. Siku uholela huu ukiisha hapa nchini vijana watafunguka wenyewe kwenda kokote duniani bila kujali kujua kiingereza wala kifaransa. Hapa tz utakutana na kundi la mbuzi katikati ya majiji wanazurura na kukatiza barabara, majogoo wanawika hata mitaa ya oyster bay, masaki na kwamtogole. HOLELA TU kila kitu.

4. Elimu bure: Wakenya wanapata elimu kwa gharama kubwa sana. Wazazi wanauza kila kitu kumsomesha mtoto, hii inasababisha msukumo mkubwa wa kijana na wazazi kulazimisha mtoto apate ajira kokote na yoyote ile ili kurejesha gharama za elimu. Kwetu huku elimu ni bure haina thamani, sio lazima upate ajira kwa udi na uvumba. Unaweza kusoma na ukaenda kutandika bidhaa zako katikati ya barabara kwa jina la machinga na kupata pesa.

5. Taasisi za umma. Tz kuna taasisi nyingi za umma/ujamaa. hata kama mfanyakazi akiwa mvivu, mzembe, mwizi na goigoi atalipwa tu mshahara. Kule kenya kazi nyingi ni wa wazungu na watu binafsi, unalazimika kuwa mchapakazi, hodari, na mwaminifu ili udumu kazini. Vijana wetu wanapenda maisha haya ya kuleana, kuvumiliana na undugunization. Hii haina uhusiano na ubora wa elimu wa kijana, bali ni umakini wa mwajili na sheria na taratibu zetu za kazi.

6. Vyakula vingi. Tz hakuna ukame, vyakula tele. Kijana anaweza kula na kulala bure kabisa kwa wazazi, shangazi, mjomba, kaka, shemeji. Kule kenya na ulaya hakuna maisha kama hayo. Kijana wetu aende wapi kuyaacha maisha kama haya?

Maisha haya ndiyo yanasababisha hata vijana wetu wanasoka washindwe kwenda kucheza mpira nje ya Tanzania.

Hivyo tusipotoshe watu kuwa elimu ya kenya iko juu zaidi ndio maana wanakwenda wengi nje kuliko watanzania. Ukweli ni kwamba maisha kenya ni magumu sana kuliko Tanzania.
 
Nampinga Mbowe kwa mengi ila hili la lugha kasema ukweli. Hata kufeli kwa watoto wetu ni sababu ya kiingereza. Tunashukuru wakati wa Mkapa shule nyingi za medium zilianzishwa. Chukuwa nchi tatu za Africa Mashariki ya zamani, Watanzania tupo nyuma sana sababu ya lugha. Akija muwekezaji haangalii umetoka wapi anataka ufaulu interview. Mwisho unakuta Wakenya na Waganda wanachukiliwa wengi. Mtanzania unalalamika nini na hujui kiingereza? Basi zingatia ya Mbowe. Big up!
 
Danganya toto !wanae wapo nje wanasoma ilia aje kuwakabidhi chama, wawe competent kweny lugha ili kufanya international negotiations.
 
Wewe unajifananisha na Mbowe , ebu mtazame mtoto anayesoma shule za kata ambaye hajui kingereza na unadhani anatoboaje? Usijiangalie wewe tu.
Mzee huyo Mboye nia na dhumuni lake hao wanae waje kutawala hawa maskani akiwa anajifanya kwamba kingereza sio kitu maana kibongobongo anayejua kingereza anaonekana msomi kinadharia japo sio kweli.

Kwa nn yeye asisomeshe wanae hapa nchini shule za kata..Kingine tambua mizizi ya elimu ipo kingereza ndo tumerithi sasa unafikiria tutfanyaje.

Kwa maarifa mtu anaweza kuwa nayo ila kweny mitihani ni kingereza je utawezaje kufikisha hayo maarifa yako kama hujui kingereza maana mtego tushaingia hatuwezi kutoka Tena.
 
Acha upotoshaji wewe. Kiingereza ni kikwazo sana kwa watanzania kupata kazi nje. Mbowe yuko sahihi.
 
Mzee huyo Mboye nia na dhumuni lake hao wanae waje kutawala hawa maskani akiwa anajifanya kwamba kingereza sio kitu maana kibongobongo anayejua kingereza anaonekana msomi kinadharia japo sio kweli.

Kwa nn yeye asisomeshe wanae hapa nchini shule za kata..Kingine tambua mizizi ya elimu ipo kingereza ndo tumerithi sasa unafikiria tutfanyaje.

Kwa maarifa mtu anaweza kuwa nayo ila kweny mitihani ni kingereza je utawezaje kufikisha hayo maarifa yako kama hujui kingereza maana mtego tushaingia hatuwezi kutoka Tena.
Mboe ni muhuni Sana na mjanja mjanja lakini kwa hii argument yupo sahihi Nampa 💯% live long Mbowe. Hi lugha ya kingereza kwa sisi Hustler wataftaji imeua dreams zetu I remember mwaka flani nilishindwa kufanya Kazi na mchina , kwa sababu huyo mchina alikua hajui kingereza so hi lugha muhimu Sana hata hawa wajinga wachina wanapambana kuijua no way.
 
Anakosea maana anaongea kinafiki wao kutwa wapo nje ...haya mkiwapa nchi wazungu watahamia hapa kabisa
 
Anakosea maana anaongea kinafiki wao kutwa wapo nje ...haya mkiwapa nchi wazungu watahamia hapa kabisa
Hizo Akili zako za kiccm ndo zinakufanya uone kuwa hii nchi inabidi kuongozwa na Ccm that why Mimi naona vijana brainwashed mpo wengi Sana hasa kuamini ujinga Kama huu umeandika hii nchi sio mali ya Ccm
 
Back
Top Bottom