Mikutano imeruhusiwa na Mama lakini mchague kwa makini nini mtakwenda kuwaambia wananchi kwenye majukwaa ya kisiasa. Mbowe aliwaambia wananchi wanaomsikiliza kuwa Watanzania hawawezi kwenda kutafuta kazi nchi za nje zikiwemo Ulaya na Marekani kwakuwa hawajui kuongea kiingereza kama ushahidi wa elimu yetu mbovu kuliko ya Kenya.
Wachina, Wasomali, Warundi, wWanyarwanda na Wahabeshi hawajui kuongea kiingereza lakini wametapakaa nchi nyingi za dunia. Wakenya hawajui kiswahili kizuri lakini wako wengi Tanzania kuliko watanzania walioko Kenya.
Hii ni kuonyesha kuwa kinachowapeleka wakenya wengi nchi za nje kuliko watanzania sio kujua kiingereza kuliko watanzania bali kuna sababu nyingine za maana kuliko kujua kuzungumza kiingereza. Na sababu hizo ni pamojana na hizi zifuatazo:
1. AMANI: Mtanzania anao uhakika wa kuiona kesho na kuwaona wajukuu zake kabla hajafa. Hii ni tofauti na mataifa mengine yanayotuzunguuka. Kila mtu anatamani kuja tz na sio kuondoka Tanzania.
2. ARDHI: Tanzania kuna ardhi kubwa ya bure kwa kila mtanzania inayomwezesha kulima, kufuga, kuvua, kujenga na kuchimba bila bughuza na kujipatia kipato. Kenya hakuna ardhi kwa watoto wao. Kenya ardhi kubwa iko mikononi mwa watu wachache na wazungu.
3. UHOLELA: Tanzania kila kitu ni holela tu. Unalima, unafuga, unavua, unafanya biashara, unachimba na kujenga kiholela tu, hata kodi haikusanywi kivilee, watu hawana leseni za biashara wala za kuuza pombe lakini wanauza tu popote. Hata leseni za udereva unapatiwa tu wakati wowote, magari mabovu yako barabarani na polisi ni washikaji tu mitaani. Hali kama hii huwezi kuipata popote pale ni tz tu. Kijana wa kitanzania hawezi kukubali kuachana na maisha kama haya aende akaparangane na maisha ya kitumwa na kimanamba huko ulaya na marekani. Siku uholela huu ukiisha hapa nchini vijana watafunguka wenyewe kwenda kokote duniani.
4. Elimu bure: Wakenya wanapata elimu kwa gharama kubwa sana. Wazazi wanauza kila kitu kumsomesha mtoto, hii inasababisha msukumo mkubwa wa kijana na wazazi kulazimisha mtoto apate ajira kokote ili kurejesha gharama za elimu. Kwetu huku elimu ni bure haina thamani, sio lazima upate ajira kwa udi na uvumba.
5. Taasisi za umma. Tz kuna taasisi nyingi za umma/ujamaa. hata kama mfanyakazi akiwa mvivu, mzembe, mwizi na goigoi atalipwa tu mshahara. Kule kenya kazi nyingi ni wa wazungu na watu binafsi, unalazimika kuwa mchapakazi, hodari, na mwaminifu ili udumu kazini. Vijana wetu wanapenda maisha haya ya kuleana, kuvumiliana na undugunization. Hii haina uhusiano na ubora wa elimu wa kijana, bali ni umakini wa mwajili tu.
6. Vyakula vingi. Tz hakuna ukame, vyakula tele. Kijana anaweza kula na kulala bure kabisa kwa wazazi, shangazi, mjomba, kaka, shemeji. Kule kenya na ulaya hakuna maisha kama hayo. Kijana wetu aende wapi kuyaacha maisha kama haya?
Maisha haya ndiyo yanasababisha hata vijana wetu wanasoka washindwe kwenda kucheza mpira nje ya Tanzania.
Hivyo tusipotoshe watu kuwa elimu ya kenya iko juu zaidi ndio maana wanakwenda wengi nje kuliko watanzania. Ukweli ni kwamba maisha kenya ni magumu sana kuliko Tanzania,