Freeman Mbowe: Iundwe Tume ya kijaji kuchunguza kifo cha Ali Kibao, Polisi hawawezi kujichunguza

Freeman Mbowe: Iundwe Tume ya kijaji kuchunguza kifo cha Ali Kibao, Polisi hawawezi kujichunguza

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amemwambia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni kuwa amfikishie salamu Rais Samia Suluhu Hassan kuwa anatakiwa kuunda Tume ya Kijaji ya Mahakama kuchunguza matukio ya utekaji na mauaji Nchini.

Amesema Tume hiyo ambayo itachunguza pia tukio la mauaji ya aliyekuwa Mwanachama wa CHADAME, Ali Mohamed Kibao, akiongeza kuwa kuruhusu Polisi kufanya uchunguzu huku wao wakiwa wanashutumiwa halitakuwa jambo lenye manufaa.

Amesema hayo alipokuwa msibani Tanga, leo Septemba 9, 2024

Pia soma: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
 
Ki uhalisia tuu utekaji ni mipango ya within in chadema ili kinyamazisha Wana mapinduzi...ila. Inafanyika Kwa usiri mkubwa sana na. Kwa mgongo wa kutumia udhaifu wa Dola...ila ki ukweli ni ndani Kwa ndani wanauana maana pesa juu ya pesa na uongozi
 
Mmmmh Chadema wamefkia pabaya sana !! Kama wanaweza sumamisha basi mchana kweupe na wakaingia wakamchukua mtu na kumvalisha pingu huku watu wanashuhudia bas wamefkia pabaya sana,,hata jeshi la polisi haliwez kabsaa kuwaambia kitu
 
Akizungumza kwenye Mazishi ya Mzee Ally Kibao Mjini Tanga, Freeman Mbowe amekataa mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kutaka vyombo vya dola vya Tanzania kujichunguza vyenyewe ili kumfahamu aliyemuua Mzee Ally Kibao.

Mbowe amemtaka Rais Samia kuunda Haraka Tume ya Kijaji ya Kimahakama itayochunguza na kuwabaini Watekaji ambao wanatajwa kuwa sehemu ya vyombo vya dola.

Mbowe amesema hawatakuwa Tayari kutoa ushahidi wao mbele ya vyombo vya Dola wanavyovituhumu maana kufanya hivyo ni sawa na kupoteza muda wao maana haitawezekana vyombo hivyo vijitie hatiani .

Screenshot_2024-09-09-09-19-29-1.png
 
Ki uhalisia tuu utekaji ni mipango ya within in chadema ili kinyamazisha Wana mapinduzi...ila. Inafanyika Kwa usiri mkubwa sana na. Kwa mgongo wa kutumia udhaifu wa Dola...ila ki ukweli ni ndani Kwa ndani wanauana maana pesa juu ya pesa na uongozi
Mkuu wanachadema Wana uwezo wa kumteka mtu kwenye bus???
Think wide mzee.....it's obvious watekaj walkua Wana shield inayowapa hiyo courage.....to me sidhan kama chadema wamehusika at all
 
Back
Top Bottom