Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Baada ya kuondolewa zuio haramu la mikutano ya kisiasa, alichokifanya Mbowe katika ufunguzi kwa kumsifia Rais Samia badala ya kujikita katika hoja za kushambulia ni mkakati wa kisiasa wa aina yake.
Ukitizama vizuri baada ya mkutano wa kwanza wa CHADEMA Mwanza, MATAGA ndilo kundi linaloonekana kuchukizwa zaidi kuliko watu wengine katika hizi hatua za awali.
Nawaelewa mataga, kwamba walitaka Mbowe na CHADEMA wafanye kazi ya mashambulizi ya jukwaani kwa Samia na CCM asilia, Mbowe kajiepusha na hilo na sasa wamefura.
Sababu kubwa ya kufura kwa MATAGA ni kwa kuwa wao MATAGA hawana jukwaa la wazi la kuelekeza mashambulizi kwa CCM asilia na hasa Rais Samia. Jukwaa walilo nalo ni mitandao ya kijamii tu wakiwa katika ID za kujificha na hivyo kubaki kuwa "keyboard warriors". Walitegemea kazi hiyo kufanywa na Mbowe zaidi hivyo amewaangusha sana.
Mbowe inawezekana kang'amua shauku ya MATAGA, wote wasiopenda maridhiano na wanafuika wa siasa za uhasana na hivyo kawaacha CCM wacheze wenyewe katika nusu yao ya kiwanja huku yeye "akipaki bus" kwa matumaini watafanya makosa wenyewe wajifunge au CDM watafanya shambulizi la kushitukiza na kuwafunga.