Freeman Mbowe kapaki basi, kaamua kuwa mlinzi zaidi ya mshambuliaji

Freeman Mbowe kapaki basi, kaamua kuwa mlinzi zaidi ya mshambuliaji

Huyu mzee nachelea kusema anazeeka vbaya
Haya ni mawazo yako binafsi, yaheshimiwe, japo yamejaa hisia zaidi ya uhalisia..!!

Mbowe kumsifia Samia kutaonekana jambo la ajabu kwa walio waoga, wale wachanga wa siasa, wanaodhani umaarufu wa Chadema uliojengwa kwa miaka mingi, unaweza kufutwa kwa tukio moja la Mbowe kumsifia Samia..

Hapa naomba pia niruhusu nikuite mnafiki, kwasababu pale juu umeandika siasa za confrontation hazina maana, pengine kwenye uzi mwingine ukaandika; "Samia akifanya jema asifiwe", sasa hapa iweje kwako Mbowe kumsifia Samia ionekane ni asante ya kutolewa gerezani, na sababu nyingine nyingi ulizoandika zisizo na maana kama michango kwa chama?
 
Hawa nao Wata jificha kwenye kichaka cha kumsema alie tangulia badala ya aliepo wanazani watanzania hatuna akili ..yaliyo pita haya tuhusu kwa sasa
 
Baada ya kuondolewa zuio haramu la mikutano ya kisiasa, alichokifanya Mbowe katika ufunguzi kwa kumsifia Rais Samia badala ya kujikita katika hoja za kushambulia ni mkakati wa kisiasa wa aina yake.

Ukitizama vizuri baada ya mkutano wa kwanza wa CHADEMA Mwanza, MATAGA ndilo kundi linaloonekana kuchukizwa zaidi kuliko watu wengine katika hizi hatua za awali.

Nawaelewa mataga, kwamba walitaka Mbowe na CHADEMA wafanye kazi ya mashambulizi ya jukwaani kwa Samia na CCM asilia, Mbowe kajiepusha na hilo na sasa wamefura.

Sababu kubwa ya kufura kwa MATAGA ni kwa kuwa wao MATAGA hawana jukwaa la wazi la kuelekeza mashambulizi kwa CCM asilia na hasa Rais Samia. Jukwaa walilo nalo ni mitandao ya kijamii tu wakiwa katika ID za kujificha na hivyo kubaki kuwa "keyboard warriors". Walitegemea kazi hiyo kufanywa na Mbowe zaidi hivyo amewaangusha sana.

Mbowe inawezekana kang'amua shauku ya MATAGA, wote wasiopenda maridhiano na wanafuika wa siasa za uhasana na hivyo kawaacha CCM wacheze wenyewe katika nusu yao ya kiwanja huku yeye "akipaki bus" kwa matumaini watafanya makosa wenyewe wajifunge au CDM watafanya shambulizi la kushitukiza na kuwafunga.
Umezoea shari siyo. Ulitaka atumie lugha ya kuudhi arudi ndani? Jaribu wewe, nyie kazi yenu ni km uchochezi sijui mmeshiba amani. Ulisubiri lugha za matusi. We una mapepo ukaombewe
 
Asante kwa uzi huu, huu ni mwanzo wa politics of reconciliation badala ya politics of confrontations. Mtu ukabiliwe na kesi mbaya, mahakama isikilize preliminary hearing, ukutwe na prima facie, ila mara DPP aifute kwa Nolle!. Unatoka gerezani a free man unakwenda Ikulu kushukuru!. Huko Ikulu unaulizwa unashida gani?

Unalia shida, fedha za uendeshaji, fedha za vikao, fedha za trips za mamtoni na mambo mengine madogo madogo, unapewa!. Vikao vinafanyika, unapiga trips, usikute hata gharama za kuanza upya mikutano ya hadhara umelipiwa!. Kwanini usipaki gari?
P
Huyu kiazi ndio ameandika haya!!!!.

Mayalla kweli ni njaa
 
Back
Top Bottom