Freeman Mbowe ni Kinyonga Mwenye sura Mbili, Wazee wa Machame wamuonya, Saashisha apewa heko

Freeman Mbowe ni Kinyonga Mwenye sura Mbili, Wazee wa Machame wamuonya, Saashisha apewa heko

NAKUANDIKIA SAASHISHA MAFUWE, UMETUHESHIMISHA

Naandika Manka Lema, Mwananchi wako wa kata ya Muungano.

Kaka kwashaa, Nakiri sikukupigia kura mwaka 2020, najuta,naumia lakini sitarudia kosa. Watu watakuwa wanajiuliza Kwanini najuta? Ngoja niwaoneshe, Sisi wananchi wa jimbo la hai tumesumbuka na shida ya maji miaka nenda rudi, wamekuja wabunge na viongozi wengi wenye mbwembwe za kila namna wakaahidi na kuleta janjajanja za kisiasa wakitutumia kufanikisha ajenda zao za kujaza matumbo yao lakini hawakufanikiwa hata theluthi ya kutibu kero ya shida ya maji jimboni kwetu.

Najuta kwasababu juzi tarehe 12.08.2022 Mbunge wetu wa sasa Saashisha Mafuwe amefanikisha tiba ya kero ya maji kwa kuwasha umeme katika mradi wa maji kikafu jambo lililoshindikana kwa miaka nenda rudi, Bila mbwembwe wala mikogo wala matamko ya kihuni Saashisha Kaleta Bilioni 3.3 kwajili ya wananchi wa hai wapate maji hii ni historia, hakika mizimu ya mababu kuanzia Boma, Muungano, KIA, Bondeni, masama kusini inashangilia uko iliko, ubarikiwe sana KAKA.

Kwasasa niseme sisi wananchi umetugusa kwenye vilindi vya mioyo yetu, hatutaacha mtu akuguse, hatutaacha mjinga akutukane, tutamdhibiti kikaragosi yeyote na kibaraka yoyote atakaekusogelea.

Endelea kutupambania sisi wanyonge wa hai maana wewe ndio mtu sahihi, umekuja kwa wakati sahihi.
Maji yako wapi? Muungano bado hakuna maji,mhhh
 
Mtoa mada tulia kwanza,maji yatakapoanza kutoka kila eneo ndo uje hapa.
Vipi Barbara alizoahidi kushighulikia?
Vuta subira Wana Hai wenyewe watasema km wataona kazi ya huyo kiongozi
Akizubaa Mbowe atarudi chap,time will tell
 
Aina hii ya watu Ni hatari kwa maendeleo ya Taifa:

Labda ungesema kuwa unamshukuru mbunge kwa kupush agenda za maendeleo na kusimamia serikali katika kutekeleza majuku yake ya kuwaletea maendeleo ungeeleweka kidogo, Bali kusema mbunge ametoa fedha ni ujinga uliopitiliza kwani hujui wajibu wa mbunge, wajibu wa Serikali kwa mwananchi halikadhalika matarajio ya wananchi kwa serikali Yao!

Mbunge Hana instruments za kukusanya Kodi Wala mapato, Hana machinery za kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo Leo anapataje uwezo wa kutoa fedha? Pathetic
 
Ngoja waje chawa wa gaidi Nkurunzinza wa Hai. Aka Baba Juisi Mkia.
 
Ama Kweli Kuna Watu waongo. Mimi nimezaliwa na kukulia Hai Miaka ya 60+ todate. Hatukuwahi kuwa na shida ya Maji. Yalikuwepo ya Mfongo, ya Chemchemi, ya Mito na Ya Bomba aliyoleta Elinawinga.

Machame na Masama yote hatukuwahi kupungukiwa na Neema ya Maji. Bomangombe na KiA na Kule umasaini, Kwa kushirikiana na KKKKT na Wabunge waliokuwepo na Serikali Kuu tukapata Maji ya Losaa /Lukani yatumikayo Leo.

Kazi ya Wabunge bikaws nyepesi wakatuombea Barabara za Lami Sadala- Kalali ikapatikana. Na Mengineyo yaliyokuwa ndani ya Uwezo wao kuyadai kabla ya kuzibitiwa. Mbungw was Sasa alitakiwa aitishe Kikao na Watu wa Hai popote walipo awafuate,vaelezwe matatizo ya iuwasilisha Bungeni. Hafanyi hivyo.

Kuna Vijana wanapotea Kwa Ulevi Kwa Kukosa Ajira, hawana Mitaji. HAI inakuwa jangwa Miti haipandwi aje na Strategy za kuondoa jangwa Barafu irudi Kibo Peak. Mashamba yaliyotaifishwa Enzi za Mwalimu yanafanya Nini na yako wapi? Yanazalisha Nini? Matatizo ya Soko la Mula tunayatatua Vipi?

Shule za Serikali za Primary na Secondary zilizozeeka tuna zikarabati Vipi? Ziko ngapi na Wapi. Hospital na Zahanati zilizopo zinatoa Huduma safi?

Na mengineyo. Siyo kusifia Vitu Utopolo sifia Vitu vya Haki. Hai hakuna Machawa Kuna wataka maendeleo Kwa yeyote atakayetuwakilisha.
 
Unazungumzia hai IPI? Hai hii mpya ya Saashisha Mafuwe imeshabadilika, barabara, madaraja, viwanda na maji yameshaanza kufanyiwa kazi

Mbunge anakaa vikao kila kona kuanzia losaa hadi soko la mula, Upareni hata shirimigungani

Wewe unazungumzia hai ile ya ufalme uliofitinika.

Kwa sasa wananchi wa hai tuko proud ya kuwa na kiongozi mchapakazi.
Ama Kweli Kuna Watu waongo. Mimi nimezaliwa na kukulia Hai Miaka ya 60+ todate. Hatukuwahi kuwa na shida ya Maji. Yalikuwepo ya Mfongo, ya Chemchemi, ya Mito na Ya Bomba aliyoleta Elinawinga. Machame na Masama yote hatukuwahi kupungukiwa na Neema ya Maji. Bomangombe na KiA na Kule umasaini, Kwa kushirikiana na KKKKT na Wabunge waliokuwepo na Serikali Kuu tukapata Maji ya Losaa /Lukani yatumikayo Leo. Kazi ya Wabunge bikaws nyepesi wakatuombea Barabara za Lami Sadala- Kalali ikapatikana. Na Mengineyo yaliyokuwa ndani ya Uwezo wao kuyadai kabla ya kuzibitiwa. Mbungw was Sasa alitakiwa aitishe Kikao na Watu wa Hai popote walipo awafuate,vaelezwe matatizo ya iuwasilisha Bungeni. Hafanyi hivyo.
Kuna Vijana wanapotea Kwa Ulevi Kwa Kukosa Ajira, hawana Mitaji. HAI inakuwa jangwa Miti haipandwi aje na Strategy za kuondoa jangwa Barafu irudi Kibo Peak. Mashamba yaliyotaifishwa Enzi za Mwalimu yanafanya Nini na yako wapi? Yanazalisha Nini? Matatizo ya Soko la Mula tunayatatua Vipi? Shule za Serikali za Primary na Secondary zilizozeeka tuna zikarabati Vipi? Ziko ngapi na Wapi. Hospital na Zahanati zilizopo zinatoa Huduma safi? Na mengineyo. Siyo kusifia Vitu Utopolo sifia Vitu vya Haki. Hai hakuna Machawa Kuna wataka maendeleo Kwa yeyote atakayetuwakilisha.
 
NAKUANDIKIA SAASHISHA MAFUWE, UMETUHESHIMISHA

Naandika Manka Lema, Mwananchi wako wa kata ya Muungano.

Kaka kwashaa, Nakiri sikukupigia kura mwaka 2020, najuta,naumia lakini sitarudia kosa. Watu watakuwa wanajiuliza Kwanini najuta? Ngoja niwaoneshe, Sisi wananchi wa jimbo la hai tumesumbuka na shida ya maji miaka nenda rudi, wamekuja wabunge na viongozi wengi wenye mbwembwe za kila namna wakaahidi na kuleta janjajanja za kisiasa wakitutumia kufanikisha ajenda zao za kujaza matumbo yao lakini hawakufanikiwa hata theluthi ya kutibu kero ya shida ya maji jimboni kwetu.

Najuta kwasababu juzi tarehe 12.08.2022 Mbunge wetu wa sasa Saashisha Mafuwe amefanikisha tiba ya kero ya maji kwa kuwasha umeme katika mradi wa maji kikafu jambo lililoshindikana kwa miaka nenda rudi, Bila mbwembwe wala mikogo wala matamko ya kihuni Saashisha Kaleta Bilioni 3.3 kwajili ya wananchi wa hai wapate maji hii ni historia, hakika mizimu ya mababu kuanzia Boma, Muungano, KIA, Bondeni, masama kusini inashangilia uko iliko, ubarikiwe sana KAKA.

Kwasasa niseme sisi wananchi umetugusa kwenye vilindi vya mioyo yetu, hatutaacha mtu akuguse, hatutaacha mjinga akutukane, tutamdhibiti kikaragosi yeyote na kibaraka yoyote atakaekusogelea.

Endelea kutupambania sisi wanyonge wa hai maana wewe ndio mtu sahihi, umekuja kwa wakati sahihi.
Kwanza hata wewe unashangaa kuwa mbunge was kuoewa na mwendazake.
 
MBOWE ALIPENDWA KWA HADAA ZA MANENO YAKE, SAASHISHA ANAPENDWA KWA UHALISIA WA MATENDO YAKE

Na Manka Lema, Mwananchi Wa Jimbo la Hai

Leo katika pitapita zangu na ka-starlet kangu nilitembelea kiwanda chenye historia kubwa mkoani kilimanjaro kiwanda cha Machine Tools kujionea uwekezaji mkubwa ukiofanywa mahali pale hakika nimefurahishwa na niliyoyaona baada ya kushuhudia ufufuaji wa kiwanda kile ukiendelea na kubwa zaidi ajira zinaenda kupatikana kwa wananchi wa jimbo la hai hasa vijana na wakina mama, hongereni wahusika.

Unajua bhana, kwa watu walioko nje ya Hai huwa hawajui sisi wazawa huwa tunampenda kiongozi kwa zama, zama zake zikiisha tunamweka kando na ndicho kilichotokea hivi karibuni na mbaya zaidi tukiona wewe kiongozi ni msanii huwa tunakupotezea kabisa, na hii imemtokea bwana Mbowe lakini wafuasi wake wanalazimisha aonekane bado yuko mioyoni mwetu jambo ambalo limeshindikana maana hata wananchadema wenzie walioko wilayani hai hawamtaki ndio maana hata 2020 walipanga kumsimamisha mgombea Helga Mchomvu na sio Mbowe lakini makao makuu wakafosi awe mbowe lakini wananchi walimfunza adabu.

Mbowe alipendwa zama zake kwa hadaa za maneno lakini vitendo vilikuwa sifuri kabisa, mbowe huyu ni mbinafsi aliwahi kununua magari ambulance na gari la taka kwa fedha za mfuko was jimbo lakini akayasajili kama magari ya kampuni yake binafsi ya HAI INITIATIVE DEVELOPMENT na wananchi tukawa tunatozwa elfu moja kila wiki kuyahudumia jambo lililotukera wengi na kuamua kumwadhibu vikali 2020, Mbowe amewahi kupanda miti katika barabara ya KIA akaiwekea vibao kuwa ni Mali ya kampuni yake ya KILIMANJARO GREEN VEGETABLES AND ENVIRONMENTAL yaani Mbowe hakuwai kufanya jambo akaliacha Kwa wananchi wa Hai ndio maana wananchi walisusa kazi zake hizo chache na zikafa, magari yote yalikufa, miti ilikufa kwasababu ya ubinafsi wake. Can you imagine mbowe amekuwa mbunge wetu for 15 years lakini hakuwahi kusimamia ujenzi wa kitu chochote kama mbunge pamoja na kuwa na mfuko wa mbunge, kuna muda huwa anajigamba juu ya shule ya harambee lakini anasahau imejengwa kwa fedha za vyama vya ushirika.

Mbowe pamoja na kuwa na mfuko wa jimbo lakini alishindwa kabisa kuja jimboni kuzipangia matumizi pesa hizo hadi zikawa zinarejeshwa wizarani, aibu kubwa hii.

Leo wananchi wa hai tumepata afueni, tumepata kijana mdogo aliebobea kwenye utumishi wa umma, mwenye malezi ya kiimani, mshika dini, asiekuwa na mawaa wala makuu, asiekuwa na majigambo wala matambo, Mtu mtaratibu aliejikita kwenye kujenga hoja bungeni na kuzifutilia, tumeanza kuona matokeo na kula matunda kwani tayari madaraja yanajengwa, barabara zinapitika hadi zile ambazo mbowe aliziita barabara za kupitisha ng'ombe, mashule yanaboreshwa kwa wingi, shule chakavu zinapungua kwa kasi jimboni kwetu.

Tatizo la maji bomang'ombe linaenda kuwa historia baada ya mbunge kupambania mradi wa kikafu kuwashwa umeme, kiwanda cha machine tools mbunge kakipigania bungeni kimefufuliwa, zao la kahawa mbunge kalipigania bungeni sasa limeanza kupata mwangaza, mazao ya kimkakati wa kibiashara mbunge anayapambania kila kukicha, vituo vya afya vinajengwa kwa kasi, leo hii hadi wananchi wa tambarare wanapata huduma pale longoi hospital, hakika SAASHISHA MAFUWE ndio masihi aliesubiriwa kwa muda mrefu na wananchi wa hai.

Utofauti wa saashisha na mbowe ni kuwa Mmoja ni MTU wa vitendo lakini mwingine ni mtu mbinafsi na hadaa nyingi zisizokuwa na kichwa wala miguu. Mbowe tulikupenda sana ila ubinafsi wako na hadaa zako zikufanya ujisahau ukadhani mahaba yetu kwako ni kwajili ya siasa zako chama chako ukasahau hisitoria yetu ya kupenda vitendo zaidi ya mboyoyo, tunakuomba uje polepole jimboni maana tayari tumepata masihi wetu anaetusikiliza na kufanya kwa vitendo matamanio yetu, fujo zako zitakutokea puani, tunajua unataka kurejea kwenye enzi lakini ufalme wako ulikwisha fitinika kaa pembeni uhudumiwe kama mwananchi wa makoa.

Saashisha chapa kazi Kaka maana wewe ndio tegemeo letu kwa sasa, endelea kujikita kwenye vitendo, makelele waachie hao watu wa hadaa.
 
Mbowe anaweza kugombea jimbo lolote Tanzania hii na akashinda bila shida yoyote ile.

Jimbo unalolisemea la Hai kwanza GDP yao tuu haijakaa kinjaa njaa kama ya kwenye jimbo lako hilo la Singida Magharibi. Ni jimbo lililojitosheleza, hawana shida ya maji,umeme wala barabara. Lami mpaka vijijini, kila raia ana uhakika wa maisha.

Hivi nyie wa kijani mnadhani dunia ya sasa inaenda kwa swaga za sijuu maendeleo, sijui barabara, sijui maji, sijui viwanda, sijui elimu bure, sijui afya blaa blaa? Hakuna mjinga dunia ya sasa. Hizo siasa pelekeni huko ndani ya chamq chenu ila siyo kwetu wananchi.
 
Wewe hapo hai hakuna anayekujua,zaidi ya kuoewa ubunge wa viti maalumu.

2025 ugombee wewe na chadema waweke picha ya jiwe au nyani,watu wa hai watachagua Jiwe au Nyani Lakini siyo wewe, uzuri namba yako ninayo 0754980805
 
MBOWE UMEZEEKA SASA, ACHA KUTENGENEZA ZENGWE JIMBONI HAI, WANANCHI WALISHAAMUA KWENDA NA SAASHISHA MAFUWE

Na Rogan Swai, Narumu Blog


Habari za Siku nyingi Mwenyekiti wa kudumu wa Chama chetu Cha Ufipa, natambua unaendelea na matibabu Kwasasa baada ya afya yako kuzorota Kwa muda Fulani, pole sana Kwa yote yaliyokukumba lakini tumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa huruma zake Leo tuko na wewe mtaani vinginevyo tungekuwa tunazungumza mengine.

Ndugu Mwenyekiti nimeandika ujumbe huu baada ya tafakuri ya muda mrefu juu ya mambo unayoyafanya kitaifa na mengine unayoyafanya nyuma ya pazia Jimboni Hai, hakika wewe ni kinyonga. Kitaifa unataka maridhiano lakini Jimboni Hai ambako yupo Mbunge kamili Ndugu Saashisha Mafuwe unamtengenezea mazengwe Kila pakikucha, bahati mbaya sana Saashisha Mafuwe ni mstaarabu mno Ila ingekuwa mtu mwingine mngeshaumizana tena.

Ndugu Mbowe umeunda kundi la wahuni machame linalozunguka kuleta sintofahamu na ghasia ukijua kabisa huu ni uchokozi, sijui unapima nguvu ya vyombo vya usalama au unapima uvumilivu wa Saashisha? Mimi natambua malezi aliyoyapata Saashisha Mafuwe kuanzia nyumbani hadi kanisani hatothubutu kukujibu Kwa fujo Bali Kwa kupiga goti, Ila sisi wananchi tusiofungamana na chama chochote, ila tunahitaji maendeleo tutakujibu Kwa njia unayoitaka maana Sasa imekuwa too much na ndio njia ulioizoea.

Juzi umeagiza watu walete fujo na kupandikiza chuki baina ya wananchi wa vijiji vya uduru na nshara juu ya mipaka ya vijiji vyao, umemtuma James Mbowe aandae wahuni kina Samson Kwayu na Jonas Lema kwenda kwenye mkutano wa Kijiji Cha nshara kuhamasisha fujo na kumtukana Mhe Mbunge Saashisha tumekuangalia tu, Leo tena umemtuma James Mbowe aandae fujo Narumu hakika hatutakubali.

Ndugu Mbowe, umekuwa bingwa wa kuvaa vinyago, ukiwa mbele ya camera unajiita mwanamaridhiano, ukiwa nyuma ya camera unaandaa fujo na ghasia Jimboni Hai ili tu Jimbo lisitawalike, nakuhakikishia hatutakuacha salama awamu hii.

Ndugu Mbowe nakusihi Pumzika Ulee wajukuu, umri wako Sasa huwezi kupambana na vijana ambao damu zao zinachemka utaishia kulialia kwenye Media, nakuomba Linda kaheshima kadogo ulichobakiwa nacho walau kakulinde uzeeni, hata wazee wenzio wa makoa wamekusihi acha kijana mwadilifu, mnyenyekuvu na mchapakazi Saashisha Mafuwe afanye kazi yake kwasasa kama ulivyoachwa wewe ufanye miaka 15 iliyopita maana hili ni Jimbo la wananchi wote wa hai na sio ufamle wako, umewadharau Sasa ukijibiwa Kwa njia unazotumia usije kulalamika na kutafuta huruma ya kitaifa maana vijana wameapa round hii kisusio Cha mtu kitaruka.

Ndugu Mbowe nakupa taarifa tu kuwa huna hatimiliki ya kuwa Mbunge wa hai milele, nakukumbusha wale kina mama wa machame uliowahi kuwaambia Hawana matumbo ya kuzaa Mbunge wameamua kumzaa Saashisha Mafuwe awapooze machungu ya maneno yako machafu, wale Wana-Narumu uliowahi kuwatukana kuwa barabara Yao niya ng'ombe wanakuonya usithubutu kukanyaga Kwenye hiyo barabara tena maana Saashisha Mafuwe kashaikarabati Kwa kiwango Bora sana.

Tunajua unazunguka maofisi ya Makatibu wakuu kuzuia Maendeleo na miradi inayofanyika Jimboni Hai lakini unapuuzwa, najua unaumia kuona bidii ya Mbunge wa Sasa, wewe ulishateleza na kuanguka inuka taratibu bila kumsumbua mtu lakini sio staili hii unayotumia.

Alamsiki
Hoja ya tokea tarehe 2 June 2022 hadi leo hakuna hata mtu kabonyeza kitufe cha like kukuunga mkono?
Umejua ni kwa nini? Umeandika upumbavu mtupu
 
Back
Top Bottom