1. Nimemsikiliza mwamba kwa hizo dakika 20 za mahojiano yake. Sijaona hoja yoyote ya maana aliyotoa zaidi kutetea kutokuwa na umuhimu wa ukomo wa madaraka ya uongozi ndani ya CHADEMA...
2. Kingine ambacho ni very funny ni kuwa, katinga kwenye mahojiano na katiba ya chama. Lakini mpaka anamaliza mazungumzo yake ameishia kuonesha gamba la katiba hiyo tu badala ya kuitumia kujengea hoja....
3. Mimi nikafikiri kuwa angetoa mifano ya hoja za Tundu Lissu ambazo zinavunja/kiuka ibara au kipengere chochote cha katiba. Hakufanya hivyo na badala yake kaishia kumshambulia tu mpinzani wake na kumtishia na kauli ya "mwisho wa siku tutarudi na kuangalia katiba inasemaje!"
4. Kingine ktk mantiki ya majibu yake ktk interview hii cha kushangaza ni kuwa, ni kama kwamba Freeman Mbowe hajui kuwa wako kwenye kipindi cha uchaguzi wa kidemokrasia huku yeye akiwa mgombea pia. Na ni kama hatambui kuwa ana wapinzani wanaokitaka kiti chake cha uenyekiti wake aliokaa hapo miaka 21. Najiuliza tu, kuwa, kwanini anafikiri hawa wapinzani wake watafanya kampeni zao kwa kumsifia yeye badala ya kueleza udhaifu na mapungufu yake binafsi na ya uongozi wake wa miaka 21 ndani ya chama? Mbowe hajui hili kweli? Je, huku ndo kuvunja au kukiuka katiba ya chama kunakosemwa? Mimi simuelewi kabisa huyu mzee..!!
5. Kwa nilivyomtazama, kumuona na kumsikiliza Mwamba, haina shaka kuwa jamaa ana hofu kubwa sana na uchaguzi ndani ya chama chake anachokiongoza. Na kusema ukweli ana haki ya kuwa na hofu kwa sababu ni yeye mwenyewe kufanya fyongo kwa kushindwa kuzitambua ishara za nyakati na majira kuwa haziko upande wake. AMECHELEWA KUCHUKUA MAAMUZI SAHIHI, YA HEKIMA NA BUSARA ya kupumzika na kulea chama...!
6. Hivi Freeman Mbowe anadhani anaweza kumtoa Tundu Lissu katika mstari kirahisi tu kama alivowahi kufanya kwa Chacha Wangwe, Zito Kabwe na wenzake, Cecil Mwambe kila walipojaribu kuutaka uenyekiti?
7. Au anadhani anaweza kumfukuza Tundu Lissu chamani kirahisi tu kama alivyofanya kwa wengine? Kwa hoja na sababu zipi hasa? Aisee wafanye kazi ya ziada sana ambayo Mimi sioni hiyo ziada...!
I don't see that possibility at least for now.....