Pre GE2025 Freeman Mbowe: Sina tabia ya kumshambulia kiongozi mwenzangu hata napokuwa siridhiki, Katiba kumbana Lissu

Pre GE2025 Freeman Mbowe: Sina tabia ya kumshambulia kiongozi mwenzangu hata napokuwa siridhiki, Katiba kumbana Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Akijibu swali la Salim Kikeke Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe amekiri kuwa mara kadhaa amekuwa akikaa na Makamu wake, Tundu Lissu na kujadili mambo yanayohusu Chama na baadae anakuja kuzisikia taarifa hizo zimetoka nje.
View attachment 3191703


Soma, Pia: Freeman Mbowe: Shutma za Lissu dhidi yangu ni za uongo

Kayajua je hayo? Si asubiri tunaomwona tuseme? Kwani nyani huona kundule? Au jambazi ajua yeye jambazi?

Kazi kweli kweli!
 
Kweli tabia za Lissu zimemkera mno Mh.Mbowe.

Retired Lusungo JokaKuu zitto junior

Kwamba Mbowe ni mheshimiwa Mungu?

GfMNLpyXYAA8ucg.jpeg
 
..Ni janga la kitaifa.

..Watanzania hatujadili kabisa hoja, hata zinapokuwepo mbele yetu.

Ni kawaida ya chawa kujadili watu.

Kumbuka chawa wako kimaslahi zaidi.

Chawa wanajua Lissu madarakani uchawa hauna nafasi tena CDM.

Wajadili hoja vipi chawa hao?
 
Katika kitu Mbowe kajaaliwa ni kariba ya kuelezea jambo, anaweza elezea jambo gumu kwa lugha rahis na wote mkamwelewa!

NB; Sultan Mbowe astaaafu inatosha aruhusu damu changa
Mbona mi sinamwelewa sasa
 
1. Nimemsikiliza mwamba kwa hizo dakika 20 za mahojiano yake. Sijaona hoja yoyote ya maana aliyotoa zaidi kutetea kutokuwa na umuhimu wa ukomo wa madaraka ya uongozi ndani ya CHADEMA...

2. Kingine ambacho ni very funny ni kuwa, katinga kwenye mahojiano na katiba ya chama. Lakini mpaka anamaliza mazungumzo yake ameishia kuonesha gamba la katiba hiyo tu badala ya kuitumia kujengea hoja....

3. Mimi nikafikiri kuwa angetoa mifano ya hoja za Tundu Lissu ambazo zinavunja/kiuka ibara au kipengere chochote cha katiba. Hakufanya hivyo na badala yake kaishia kumshambulia tu mpinzani wake na kumtishia na kauli ya "mwisho wa siku tutarudi na kuangalia katiba inasemaje!"

4. Kingine ktk mantiki ya majibu yake ktk interview hii cha kushangaza ni kuwa, ni kama kwamba Freeman Mbowe hajui kuwa wako kwenye kipindi cha uchaguzi wa kidemokrasia huku yeye akiwa mgombea pia. Na ni kama hatambui kuwa ana wapinzani wanaokitaka kiti chake cha uenyekiti wake aliokaa hapo miaka 21. Najiuliza tu, kuwa, kwanini anafikiri hawa wapinzani wake watafanya kampeni zao kwa kumsifia yeye badala ya kueleza udhaifu na mapungufu yake binafsi na ya uongozi wake wa miaka 21 ndani ya chama? Mbowe hajui hili kweli? Je, huku ndo kuvunja au kukiuka katiba ya chama kunakosemwa? Mimi simuelewi kabisa huyu mzee..!!

5. Kwa nilivyomtazama, kumuona na kumsikiliza Mwamba, haina shaka kuwa jamaa ana hofu kubwa sana na uchaguzi ndani ya chama chake anachokiongoza. Na kusema ukweli ana haki ya kuwa na hofu kwa sababu ni yeye mwenyewe kufanya fyongo kwa kushindwa kuzitambua ishara za nyakati na majira kuwa haziko upande wake. AMECHELEWA KUCHUKUA MAAMUZI SAHIHI, YA HEKIMA NA BUSARA ya kupumzika na kulea chama...!

6. Hivi Freeman Mbowe anadhani anaweza kumtoa Tundu Lissu katika mstari kirahisi tu kama alivowahi kufanya kwa Chacha Wangwe, Zito Kabwe na wenzake, Cecil Mwambe kila walipojaribu kuutaka uenyekiti?

7. Au anadhani anaweza kumfukuza Tundu Lissu chamani kirahisi tu kama alivyofanya kwa wengine? Kwa hoja na sababu zipi hasa? Aisee wafanye kazi ya ziada sana ambayo Mimi sioni hiyo ziada...!

I don't see that possibility at least for now.....
Ndugu The Palm Beach , kongole kwa mchango mzuri sana wa uchambuzi wa mahojiano ya Mbowe na Kikeke.

Umeandika ukweli na uhalisia wa yaliyomo kwenye mahojiano na yale ambayo yapo kwa Mbowe kutokana na uchaguzi huu.

Ningetamani huu uchambuzi wako uwe laminated na "ugandishwe" pale juu Jukwaa la Siasa.
 
Back
Top Bottom