Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe: Uchaguzi Mkuu wa 2020 CHADEMA hatukuwa na wagombea sahihi

Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe: Uchaguzi Mkuu wa 2020 CHADEMA hatukuwa na wagombea sahihi

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amekiri kuwa kushindwa kwa CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulitokana na kuweka wagombea dhaifu kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo uraisi na hivyo wamejifunza na uchaguzi ujao wataweka wagombea wenye nguvu na ushawishi watakaozunguka nchi nzima kunadi sera na ajenda za wanachi.
Hivi kweli kwa kuweka mtu ambaye dishi limeyumba kiasi hicho kugombea urais, hivi walitegemea ushindi kweli? Yani sisi watanzania na akili zetu timamu kweli tuchague chizi kuwa rais? Hivi nyie chadema huwa mnatuonaje?
Na jamaa asivyo na akili timamu, keshajitangazia 2025 lazima anagombea, mtegemee kupigwa tena na mama. Yani yule jamaa hazimo kabisa.
 
Amemzungumziaje aliyekuwa mgombea wa ubunge Hai kwa tiketi ya Chadema?
Lisu anapambana na Diamond kumbuka Diamond ameajiri maelfu ya watu huku Lisu akiwa hana legacy nchini na hata jimboni kwake alipowahi kuwa mbunge kwa miaka kumi.Lisu kwa sasa amefugwa na Amsterdam Ubelgiji.
Umeelewa swali nililouliza?
 
Wanasiasa wote ni wanafiki sana. Unafiki na uongo ndiyo sifa za kwanza za mtu kuwa mwanasiasa.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amekiri kuwa kushindwa kwa CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulitokana na kuweka wagombea dhaifu kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo uraisi na hivyo wamejifunza na uchaguzi ujao wataweka wagombea wenye nguvu na ushawishi watakaozunguka nchi nzima kunadi sera na ajenda za wanachi.

Mbowe amesema Chadema haijawahi kuishiwa ajenda za kupambana na CCM.

My take.

Watakiri yote waliyomsingizia mwendazake laana ya kumtukana imeanza kuwatafuna.

Kumbe waliweka wagombea dhaifu alafu wakasingizia wameibiwa kura na mwendazake. Hovyo kabisa.

=====

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amekiri kuwa walikuwa na baadhi ya wagombea ambao hawakuwa wakikubalika kwenye maeneo waliyogombea nafasi mbalimbali ikiwemo ubunge na madiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Pia, amesema kwa sasa falsafa zake za kisiasa zinakwenda sawa na zile za aliyekuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Marekani, Thomas "Tip" O'Neil Jr.

Amesema O'Neil kupitia kitabu chake cha 'All Politics is Local' amesema siri za ushindi za chama cha siasa ambazo ndizo anazutimia kuongoza mapambano ya kushika dola nchini.

Amezitaja falsafa hizo kuwa ni chama kupata mgombea sahihi na nayekubalika kwa wapiga kura.

"Nikiri kuna maeneo mengi tulikuwa na wagombea sahihi, lakini kuna maeneo kadhaa tulikuwa na wagombea dhaifu, huo ni ukweli na haupingiki kwa sababu waswahili wanasema wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani," amesema Mbowe.

Ametaja jambo la pili kuwa ni chama kuwa na ajenda ya kuwashawishi wanachi kukichagua, ambapo kwa upande wa CHADEMA, Mbowe amesema hakijawahi kukosa ajenda ya kushindana na Chama tawala-CCM.

"Ilani yetu ya uchaguzi ilikuwa bora kwa sababu imefanyiwa utafiti," amesema.

Mambo mengine ambayo Mbowe ameyataja ni kuwa na uongozi imara na rasilimali fedha ambapo kwa sasa chama kinatengeneza miundombinu rafiki ikiwemo kuwekeza kwa vijana na kukuza teknolojia kutoka analojia kwenda dijitali.

"Sasa hivi wanachama wa CHADEMA ni ambao hawazidi umri wa miaka 45 hii ni dalili nzuri kwamba, upinzani utakuwa imara zaidi lakin pia tunapambana kuhakikisha kila kitu tunachokifanya kinafanyika kidijitali," amesema Mbowe.

Kiongozi huyo amesema kikao cha Kamati ya Utendaji ya CHADEMA Kanda ya Victoria kimeafiki kuwa kila Jumamosi kuwa siku ya kuvaa sare ya Chama hicho kwa wanachama wake.

"Tunatambua kuwa wana CHADEMA walikuwa wameshaanza kusahau hadi kuvaa sare, lakini sasa wanachama wa CHADEMA watavaa sare kila Jumamosi ili kuongeza motisha na idadi ya wafuasi wetu," amesisitiza.

Chanzo: Mwananchi
Kuna harufu za uongo kwenye hii threads
 
Kama hakuna bifu basi tutamsikia tena ndugu Freeman kwenye kipindi cha utangazaji cha Antipasu cha mitandaoni akihojiwa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hivi kumbe Lisu sasa hivi ana ka tv kake ka mkononi!
 
Nilishasema kuna bifu Kati Lisu na mwenyekiti wake haya sasa wale wapambe nuksi njoeni tena. Utabiri wangu Mbowe atadondoshwa na Lissu maana Ile mashine sio mchezo.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom