Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Leo umehitimishwa uongoze wa Freeman Mbowe, baada ya kukaa kwenye nafasi ya juu ya chama kwa takribani miaka 21.
Miaka 21 ndani ya uongozi wa chama cha siasa cha upinzani, si jambo rahisi. Hiyo ni miaka ya mara jela, mara mahakamani, mara kuharibiwa biashara, mara kufungiwa account, na mengine mengi magumu.
Kwa kazi kubwa aliyoifanya Mbowe, na baadhi ya wanaCHADEMA ambao wengine wamepoteza mpaka maisha yao, michango yao haiwezi kutwezwa wala kudhihakiwa, bali itakuwa msingi imara wa kuendeleza mapambano ya kuitafuta haki na demokrasia ya kweli kwa nchi yetu.
Uongozi mpya, uboreshe na ulete matumaini mapya, bila ya kuyapiga teke mazuri ya msingi yaliyofanywa na watangulizi hawa.
Mbowe anatoka kwenye nafasi ya uongozi wa chama akihitimisha kwa kutoa elimu ya bure ya demokrasia kwa CCM ambayo haijawahi kuwa na uchaguzi, zaidi ya maigizo ya uchaguzi ambayo huitikiwa na wajumbe wa mkutano mkuu, kwa kusema tu NDIYO, bila ya ushindani.
CCM imepelekwa darasani, kufundishwa maana ya uchaguzi. Je, wana akili ya kufundishika au ni mbumbumbu wa kudumu, tusubiri kuona watafanya nini juu ya maamuzi yao waliyoyafanya siku za karibuni DODOMA yanayokiuka hata kanuni zao wenyewe.
WanaCCM walioudhiwa na mambo yasiyo ya kidemokrasia ndani ya CCM yaliyofanyika pale Dodoma, nendeni CHADEMA mkaifaidi demokrasia ya kweli.
Hongera sana Lisu, Hongera sana Heche, mmebeba matumaini ya watanzania wengi wenye dhamira njema na Taifa hili.
CHADEMA MOJA, TAIFA MOJA, LENGO MOJA DHIDI YA WALIOPORA MAMLAKA YA UMMA.