Freeman Mbowe umeacha alama. Wewe si mnyonge bali ni Shujaa

Freeman Mbowe umeacha alama. Wewe si mnyonge bali ni Shujaa

Umeongea vizuri sana. Kipimo cha kwanza cha uongozi mpya ni watawafanyia nini wale ambao waliomuunga mkono Mbowe. Watalipa visasi? Watawabeza? Au watawapa heshima wanayostahili?
Kwa yale ambayo nimeyaona kutoka kwa wafuasi wa Lissu ni kuwa wanataka damu lazima imwagike.
Mimi naamini bado kuwa haya ndio matokeo ambayo CCM waliyataka. Watakuwa wamefurahi sana.

Amandla...
Kwamba CcM walitaka Lissu ashinde!!!??? Mmechange gear ghafla hivi!? Kifupi Lumumba tumbo joto maana sasa watalazimika kufanya siasa na si maigizo
 
I wish angesikiliza maoni ya watu kipindi kile, yaliyomtaka kutogombea tena hiyo nafasi! Ila ndiyo hivyo tena; wapambe wake wakaamua kumpoteza.
Jasusi mwitu alimjaza vibaya sana na akakubali kujaa!!! Wamepiga mkwanja wake na mwisho wa siku kastaafishwa kwa aibu!
Yote kwa yote Mbowe ni shujaa wa demokrasia ya nchi hii na ni hazina kubwa kwa Chadema, tutaendelea kumuheshimu.
 
Kumpongeza Mbowe ni ujinga mkubwa.

Angejiweka pembeni kwa heshima tungeamini haya unayoyasema ni adili.

Amepoteza kila kitu mpaka heshima yake
Mbowe anastahili pongezi haikuwa rahisi kwa hili,maana alikuwa na uwezo wote wa kuharibu uchaguzi.
 
Leo umehitimishwa uongoze wa Freeman Mbowe, baada ya kukaa kwenye nafasi ya juu ya chama kwa takribani miaka 21.

Miaka 21 ndani ya uongozi wa chama cha siasa cha upinzani, si jambo rahisi. Hiyo ni miaka ya mara jela, mara mahakamani, mara kuharibiwa biashara, mara kufungiwa account, na mengine mengi magumu.

Kwa kazi kubwa aliyoifanya Mbowe, na baadhi ya wanaCHADEMA ambao wengine wamepoteza mpaka maisha yao, michango yao haiwezi kutwezwa wala kudhihakiwa, bali itakuwa msingi imara wa kuendeleza mapambano ya kuitafuta haki na demokrasia ya kweli kwa nchi yetu.

Uongozi mpya, uboreshe na ulete matumaini mapya, bila ya kuyapiga teke mazuri ya msingi yaliyofanywa na watangulizi hawa.

Mbowe anatoka kwenye nafasi ya uongozi wa chama akihitimisha kwa kutoa elimu ya bure ya demokrasia kwa CCM ambayo haijawahi kuwa na uchaguzi, zaidi ya maigizo ya uchaguzi ambayo huitikiwa na wajumbe wa mkutano mkuu, kwa kusema tu NDIYO, bila ya ushindani.

CCM imepelekwa darasani, kufundishwa maana ya uchaguzi. Je, wana akili ya kufundishika au ni mbumbumbu wa kudumu, tusubiri kuona watafanya nini juu ya maamuzi yao waliyoyafanya siku za karibuni DODOMA yanayokiuka hata kanuni zao wenyewe.

WanaCCM walioudhiwa na mambo yasiyo ya kidemokrasia ndani ya CCM yaliyofanyika pale Dodoma, nendeni CHADEMA mkaifaidi demokrasia ya kweli.

Hongera sana Lisu, Hongera sana Heche, mmebeba matumaini ya watanzania wengi wenye dhamira njema na Taifa hili.

CHADEMA MOJA, TAIFA MOJA, LENGO MOJA DHIDI YA WALIOPORA MAMLAKA YA UMMA.
Mwamba Ameonesha ukomavu wa kisiasa!!!!
 
Kwamba CcM walitaka Lissu ashinde!!!??? Mmechange gear ghafla hivi!? Kifupi Lumumba tumbo joto maana sasa watalazimika kufanya siasa na si maigizo
Huwezi kuelewa. Mimi siku zote nimekuwa nikisema CCM wanataka Lissu ashinde. Kada wa CCM mkubwa alikuwa anamfanyia kampeni ya waziwazi.
Sasa ameshinda, yetu macho.

Amandla...
 
Kumpongeza Mbowe ni ujinga mkubwa.

Angejiweka pembeni kwa heshima tungeamini haya unayoyasema ni adili.

Amepoteza kila kitu mpaka heshima yake

ushindani ni mzuri. Demokrasia imeonekana hadharani. ushindi wa mezani hauna ladha na furaha kama wa uwanjani.
 
Huwezi kuelewa. Mimi siku zote nimekuwa nikisema CCM wanataka Lissu ashinde. Kada wa CCM mkubwa alikuwa anamfanyia kampeni ya waziwazi.
Sasa ameshinda, yetu macho.

Amandla...
Lumumba buku jero ona aibu. Lissu huyuhuyu mnayempinga daily ndo mlitaka ashinde!? Nape, Kigwangala n.k wote walishusha mabandiko yao kuonesha namna Mbowe anastahili kuwa mwennyekiti badala ya mbowe leo hii mmepigwa usoni mnachange gear!!! Aibu
 
Umeongea vizuri sana. Kipimo cha kwanza cha uongozi mpya ni watawafanyia nini wale ambao waliomuunga mkono Mbowe. Watalipa visasi? Watawabeza? Au watawapa heshima wanayostahili?
Kwa yale ambayo nimeyaona kutoka kwa wafuasi wa Lissu ni kuwa wanataka damu lazima imwagike.
Mimi naamini bado kuwa haya ndio matokeo ambayo CCM waliyataka. Watakuwa wamefurahi sana.

Amandla...
Huwezi kuwa positively kwa Lissu na timu yake tupe ushahidi baada ya ushindi nini kimefanywa kuthibitisha dhana yako, otherwise you are a bad looser
 
Kumpongeza Mbowe ni ujinga mkubwa.

Angejiweka pembeni kwa heshima tungeamini haya unayoyasema ni adili.

Amepoteza kila kitu mpaka heshima yake
Tatizo wapambe wake na kuziamini zile kauli ya yeye ndiye Alfa na Omega. Ametoka ukumbini kwa aibu
 
Kwamba CcM walitaka Lissu ashinde!!!??? Mmechange gear ghafla hivi!? Kifupi Lumumba tumbo joto maana sasa watalazimika kufanya siasa na si maigizo
Huyu jamaa hajitambui mapenzi yake kwa Mbowe yamemtia upofu wa akili, chuki, kinyongo na hasira za Lissu kushinda amebaki kubwabwaja tu, hakuna points
 
Huwezi kuelewa. Mimi siku zote nimekuwa nikisema CCM wanataka Lissu ashinde. Kada wa CCM mkubwa alikuwa anamfanyia kampeni ya waziwazi.
Sasa ameshinda, yetu macho.

Amandla...
Haya ni maoni yako ya ndoto, kuanzia humu jf makada wengi wa CCM walikuwa wanampigia kampeni Mbowe. Tuonyeshe kwa huo ushahidi wa waziwazi wa kada wa CCM kumpigia Tundu Lissu kura? You are a bad looser
 
Lumumba buku jero ona aibu. Lissu huyuhuyu mnayempinga daily ndo mlitaka ashinde!? Nape, Kigwangala n.k wote walishusha mabandiko yao kuonesha namna Mbowe anastahili kuwa mwennyekiti badala ya mbowe leo hii mmepigwa usoni mnachange gear!!! Aibu
Hivi kwa ufahamu wako unadhani Nape wa goli la mkono na Kingwangala walidhani kuwa wanachama wa Chadema watafuata ushauri wao? Au kwa kufanya hivyo, watu wataamini CCM wanamtaka Mbowe na hivyo watampigia kura Lissu?

Nitakwambia kwa nini CCM wanafurahia matokeo ya uchaguzi wenu. Mbowe ni pragmatic na anaona mbali. Lissu ni mtu wa mihemuko. Kama mlivyosema wakati wa busara sio huu. Atawaambia hamna kuingia kwenye uchaguzi mpaka Katiba Mpya imepatikana. CCM watasema hewala na wataendelea na uchaguzi bila CDM. Act Wazalendo watashinda viti vya ubunge na udiwani. Zitto atakuwa kiongozi wa upinzani bungeni. Kwa sababu CDM haitagombea haitapata kura za kuwawezesha kupata ruzuku. CDM itategemea michango lakini hata hiyo watagundua haitoshi kuendesha chama. CDM kwishnei. Wakina Nape wamewawekea mtego na nyinyi mkaingia jumla.

Nawatakia kila la kheri chini ya uongozi wa Lissu, Heche na Lema.

Amandla...
 
Back
Top Bottom