Binafsi naamini ubunge ni ajira ndio maana kuna mishahara na mafao
Kinachonisikitisha ni kuwa viongozi wa CHADEMA kuzuia ajira za wenzao kisa wao hawakushinda. Wanataabisha familia zao maana walikuwa na faraja angalau wapate ubunge. Kwa kujali sana maslahi yao hawathamini kutaabika kwa wengine. Nimefurahi sana kumuona yule mbunge wa. CHADEMA bungeni, familia yake inamtazama yeye na sio chama, akilala njaa sina imani kama chama kitawajibika. Binafsi sioni tofauti ya mbunge wa CHADEMA, CCM,ACT au CUF kwani wote wamefuata shibe tu bungeni ila ninavyoona wapinzani wamekuwa wakiamini katika kupiga kelele na kupotosha umma kwa manufaa yao binafsi.